Utafiti
uliofanywa na Shirika la Afya Duniani (WHO) nchini umeonyesha asilimia 20 ya
saratani ya koo husababishwa na ngono ya mdomo maarufu kama ‘Oral Sex”. Utafiti
huo unaonyesha saratani ya koo pia huambukizwa kupitia njia mbalimbali ikiwemo
ulaji wa vyakula vyenye pilipili, pombe kali, vitu vyenye uchachu pamoja na
kurithi kutoka kwa wazazi.
Utafiti
unaonyesha watu wengi hasa vijana wanamejiingiza kwenye vitendo hivi vya
kufanya ngono wakitumia midomo hasa ndimi, hivyo kuhatarisha uhai wao. Katika
utafiti huo wa hivi karibuni, ulibaini wanaume 747 na wanawake wakiwa 472
hugundulika kila mwaka kuwa na saratani hiyo huku wanaopoteza maisha kila mwaka
ni wanaume 444 wakifuatiwa na wanawake 270 kutokana na ugonjwa huo.
Utafiti
unabainisha kuwa asilimia kubwa ya vijana wenye umri kati ya miaka 20 hadi 45
wanatumia staili ya kuwanyonya wenza wao sehemu za siri lengo likiwa ni
kuwavutia wapenzi wao katika kushiriki ngono.
Vijana wenye umri huo ndio wahanga wakubwa kwa sasa kutokana na
ugonjwa huo kuonekana kuwaathiri kwa kasi, huku wengi wakiwa hawajui athari
zake. Baadhi hujisifia kwamba ni wajuzi, kumbe wanajitafutia kifo kwa kufanya
vitendo hivyo.
Utafiti unaonyesha kwa watu wazima walio wengi hawana muda wa
kufanya hayo wanayofanya vijana, hivyo kujikuta angalau wanakuwa salama na
kupatwa na saratani ya koo kwa njia hiyo inayoonekana kama ni chafu pia.
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Saratani kutoka Taasisi ya
Saratani ya Ocean Road, Dk Crispin Kahesa anasema saratani ya koo ni ya pili
katika mtiririko wa saratani zinazowapata wanaume nchini, ikiongozwa na ile ya
ngozi (Karposi’s Sarcoma) ambayo huambukizwa kwa njia ya kujamiana. Kuna
saratani aina zaidi ya 24 zinazoisumbua Tanzania.
Anasema mbali na staili hiyo pia, kuna baadhi ya watu hupata
saratani ya koo kwa kurithi kutoka kwa wazazi wao na wengine kuwa na umri
mkubwa ambao huchangia kupata tatizo hilo, lakini siyo kwa asilimia kubwa kama
ile ya ngono ya mgomo.
“Hali hii ya vijana wenye umri huo kuwanyonya wanawake inatokana
na ujana, wengine wanaiga kwenye mitandao, lakini mambo haya hayakuwepo zamani
tofauti na sasa. Utakuta wanaume ili aweze kumvutia mwanamke anamfanyia hivyo
sehemu za siri, lakini zamani staili hii haikuwepo kabisa,” anasema Dk Kahesa
na kuongeza.
“Kuna njia nyingi tu za kumvutia mwanamke lakini siyo hii bila kujua madhara yaliyopo, vijana wengi nchini wanaona njia rahisi ya kupendwa na mwanamke ni hiyo wakati kuna njia nyingi za kufanya. Nje ya hiyo wanawake wengine huwa na magonjwa mbalimbali, kwa jumla hakuna usalama wowote kwa wanaume kufanya kitendo hicho,”anaongeza
“Kuna njia nyingi tu za kumvutia mwanamke lakini siyo hii bila kujua madhara yaliyopo, vijana wengi nchini wanaona njia rahisi ya kupendwa na mwanamke ni hiyo wakati kuna njia nyingi za kufanya. Nje ya hiyo wanawake wengine huwa na magonjwa mbalimbali, kwa jumla hakuna usalama wowote kwa wanaume kufanya kitendo hicho,”anaongeza
Anasema staili ya maisha nayo imechangia kuongezeka kwa ugonjwa
huo, vijana wengi kwa sasa hutumia muda mwingi kuangalia video za ngono na
staili zinazofanywa na wenzetu wa nje na hivyo kuongezeka kwa matumizi ya ngono
ya mdomo.
Dk Kahesa anasema asilimia 12 ya wagonjwa wote wa saratani
nchini wanasumbuliwa na saratani ya koo, hivyo kuna kila sababu kwa vijana
kubadilisha tabia na kuepuka kuiga mitindo ya wenzetu wazungu ambayo mara
nyingi inapotosha mila na tamaduni za Kiafrika.
Anasema katika mtiririko wa saratani zinazoongoza nchini
saratani ya koo inashika nafasi ya tano, wagonjwa wengi wanaopatwa na ugonjwa
huo ni watu wenye umri mkubwa wa miaka 60 na kuendelea hiyo inaonyesha kuwa
wengi wao walianza ngono ya mdomo muda mrefu wakati wakiwa bado wadogo.
“Asilimia kubwa ya wagonjwa wanaopatikana na kansa ya koo
nchini, inawapata watu wenye umri wa kuanzia miaka 60 na kuendelea kutokana na
wengi wao kuanza mapema vitendo vya ngono kwa njia ya mdomo wakati bado wadogo
au wengine kurithi kutoka kwa wazazi wao,” anasema Dk Kahesa.
Aina ya
kansa ya koo
Tafiti zinaonyesha kuna aina mbili za saratani ya koo; aina ya
kwanza ni “Oesophagus Carcinoma na Squamous cell carcinoma, zote hutofautiana
wakati zinapimwa kwenye darubini lakini matibabu yake yanafanana.
Aina hizo ndizo zilizopo nchini na huanza mapema kuharibu seli
ambazo zipo katika utandu uliopo katika ukuta wa koo kabla ya kuenea katika
maeneo mengine ya koo.
Visababishi
vya kansa ya koo:
Moja kati ya vitu vinavyosababisha kansa ya koo ni mwenendo wa maisha
yetu kwa kula vyakula vyenye asidi, vyakula vichachu, vyakula vyenye pilipili,
pombe kali na vyakula vigumu ambavyo hukwaruza koo na hivyo kusababisha
saratani.
Anasema asilimia 90 ya wagonjwa wanaopokelewa katika Taasisi ya
Saratani ya Ocean road wanakuwa na historia ya kutumia vikali kama pombe kali,
kuvuta sigara kwa kupindukia, kula pilipili kwa wingi na kutumia vitu vyenye
uchachu.
Dalili za saratani ya koo
Dalili za saratani ya koo
Moja kati ya dalili za mgonjwa wa saratani ni chakula kukwama
kwenye koo, siku za mwanzo mgonjwa anaweza kushindwa kumeza chakula kigumu
kisha cha majimaji na baadaye akashindwa kumeza hata mate.
Ugonjwa huo unachukua muda mrefu kugundua na kuona viashiria
kwani mwanzo mgonjwa huanza kupata shida kumeza chakula na kwamba wagonjwa
wengi wanaofika katika Taasisi hiyo ya Saratani wanakuwa tayari wamechelewa
kwani wanakuwa katika hatua ya mwisho.
“Unaweza usionyeshe dalili lakini kadri siku zinavyokwenda ndiyo
kunakuwa na dalili zinajitokeza pia katika kipindi hicho mtu anakuwa na maumivu
wakati wa kumeza chakula, maumivu katika kifua na mgongo na hata kupungua uzito
pamoja na kikohozi kikavu kinachoweza kudumu mwezi mmoja,” anasema.
Njia ya
kuzuia saratani ya koo.
Kwanza mtu mwenye ugonjwa huo anapaswa kuwahi hospitali ili
aanze matibabu mapema kutokana na ukweli kwamba mgonjwa anayewahi kupata
matibabu ana uwezekano wa kupona kuliko yule ambaye amechelewa kugundulika na
kuanza matibabu.
Kama saratani hiyo itakuwa imeshambulia viungo vyote vilivyopo
jirani na koo na hadi kufika katika tezi au kiungo kingine cha mwili, mgonjwa
anaweza kutibiwa kwa njia ya upasuaji, kutumia mionzi na hata kifaa maalumu
ambacho ni kemikali.
Tafiti
zilizofanywa nchini
Wataalamu mbalimbali nchi wamefanya tafiti zinazohusiana na
ugonjwa huo na kusema kuwa kati ya mwaka 1983 hadi 1992 kulikuwa na kati ya
watu 546 waliopimwa, wanaume 430 na wanawake 116 waligundulika kuwa na ugonjwa
huo.
Utafiti huo ulishirikisha watu wenye umri wa miaka 21 hadi 90,
ulibaini kuwa wagonjwa wengi walikuwa wenye umri wa miaka 50-59 tofauti na hali
iliyopo sasa ugonjwa wa kansa ya koo unawaathiri vijana wenye umri wa miaka 40.
Dk Kahesa anasema katika kipindi cha miaka saba iliyopita
takwimu za taasisi yake imeongezeka kutoka kutoka wagonjwa 167 hadi kufikia
wagojwa 277. Hali inaonekana huenda ikaongezeka kutokana na ukweli kwamba wengi
wa watu wanaonekana kuendeleza tabia hatarishi zikiwemo hizo za kutumia midomo.
Magonjwa mengine sehemu za siri
Miongoni mwa magojwa ambayo yanaweza kumpata mtu ambaye ananyonya au kulambana sehemu hizo ni pamoja na gonjwa wa gonoreha, ambapo ugonjwa huu huanzia katika koo na mwanzoni huhisi kama ni ukavu wa kifua au maradhi ya kawaida ya kifua, ila baadaye hushuka na kuelekea katika viungo vya uzazi.
Miongoni mwa magojwa ambayo yanaweza kumpata mtu ambaye ananyonya au kulambana sehemu hizo ni pamoja na gonjwa wa gonoreha, ambapo ugonjwa huu huanzia katika koo na mwanzoni huhisi kama ni ukavu wa kifua au maradhi ya kawaida ya kifua, ila baadaye hushuka na kuelekea katika viungo vya uzazi.
Ugonjwa mwingine ni kaswende ambao huambukizwa kirahisi zaidi
kupitia mdomo na hasa pale inapotekoa mdomo unapokutana na kiungo chenye athari
hizo.
Vile vile ugonjwa wa chlamydia ni moja wapo kati ya magonjwa ya
zinaa ambao huambukizwa kwa bakteria na kwamba ugonjwa huu pia huambukizwa
kupitia mdomo, ingawa waathirika wanaweza wasijijue maana huwa hauna dalili kwa
muda mrefu.
Hepatitis
A: Hiki ni ni kirusi kinachopatikana katika kinyesi cha binadamu,
kirusi hiki huwaingia wale wanaopenda kunyonya na kulambana sehemu za haja
kubwa. Ni kwamba kwa ugonjwa huu mtu anaweza akaharibika macho hadi kupofuka.
Hepatitis
B: Ugonjwa huu huambukizwa kama virusi vya Ukimwi kwa sababu
virusi vyake hukaa katika majimaji yanayotoka katika sehemu za siri na damu.
Mtu akiwa na ugonjwa huu, mwili wake unakuwa na vipele vingi na hata majipu ambayo
huwa magumu kupona na wapo wanaokufa.
Vile vile ugonjwa wa Hepatitis
C: ni ugonjwa ambao hupatikana pindi damu inapotoka maana vijidudu vyake
vinakaa katika damu. Ugonjwa huu humfanya mtu kuvimba viungo na hata kukatika.
Hata hivyo kupitia staili hii yaupeana raha kwa kunyonyana
sehemu za siri, kuna uwezekano wa kupata maambukiz ya virusi vya Ukimwi kwa
uchache lakini kwa nchi zilizoendelea wamebuni aina ya kondom ambazo huvaliwa
katika mdomo wa binadamu na hivyo kupunguza hatari ya kupata madhara hayo.
JE NGUVU ZA KIUME ZINACHANGIA?
Dk Kahesa anasema hakuna utafiti wa moja kwa moja unao onyesha
kuwa baadhi ya wanaume wanaofanya ngono kwa njia ya mdomo wanakuwa na upungufu
wa nguvu za kiume.
“Utafiti wa mtu mmoja hautoshi kuonyesha kuwa baadhi ya wanaume
wanafanya ngono kwa njia ya mdomo wanakuwa na ukosefu wa nguvu za kiume, hivyo
kinachotakiwa ni kufanya utafiti wa kina ili kubaini kama tatizo hilo lipo
licha ya kuwepo kwa kesi nyingi zinazodaiwa kuwa baadhi ya wanaume hawana nguvu
za kiume na wapenzi wao huwafichia siri kwa kufanya nao mapenzi kwa njia yam
domo”anasema.
NINI KIFANYIKE:
Wataalamu wa masuala ya ndoa na saikolojia wanasema kuna njia
nyingi za kuandaana wakati wa tendo la ndoa tofauti na kunyonyanyana sehemu za
siri.
Wataalamu hao wanasema sio sahihi kwa mwanaume au mwanamke kunyonyana sehemu za ndoa mwenzake na kwamba staili hizo ni staili za wanzetu wa nje lakini kitu kinachosababisha kukua kwa kasi kwa staili hiyo ya kunyonyonyana sehemu za siri au kufanya mapenzi kwa njia ya mdomo ni kutokana na kasi ya utandawazi.
Wataalamu hao wanasema sio sahihi kwa mwanaume au mwanamke kunyonyana sehemu za ndoa mwenzake na kwamba staili hizo ni staili za wanzetu wa nje lakini kitu kinachosababisha kukua kwa kasi kwa staili hiyo ya kunyonyonyana sehemu za siri au kufanya mapenzi kwa njia ya mdomo ni kutokana na kasi ya utandawazi.
Wadadisi wa mambo wanadai kuwa baadhi ya watu huiga staili hizo
kutoka katika mitandao bila kujali kuwa kuna zina madhara makubwa, hivyo ni
jukumu la kila mtu kulinda afya yake na ya mwenza wake.
Sio kila kitu kinachowekwa katika mitandao ya kijamii kina
manufaa la hashaa! vitu vingine vinachangia kuhatarisha maisha.
No comments:
Post a Comment