Watu wengi wamekuwa wakifikiria sana na kuwa na hofu juu ya hali ya uzee kwa maana ya kwamba wanawaza namna watakavyoishi wakiwa wazee. Wanawaza namna ambavyo baadhi ya wazee wasivyoweza hata kutembea kwa miguu yao kiasi cha kulazimika kubebwa. Kutokana na hofu hiyo na pengine hasa watu kutopenda hali ya uzee wengine wamekuwa wakitafuta namna ya kuchelewesha kuwa wazee kwa kutumia madawa yanayofanya miili ionekane kama vijana. Pamoja na madawa hayo watu wengine wamekuwa wakitafuta namna ya kubadiri mfumo wao wa maisha.
Katika mada hii nitaeleza mambo mbalimbali ya kufanya kuhusiana na mfumo wa maisha (life style) ambayo unapaswa kuyafanya ili upate kuwa na mwonekano wa ujana au kuchelewesha kuwa na hali ya uzee licha ya kuwa na umri mkubwa hapo baadaye. Mambo hayo muhimu ni pamoja na haya yafuatayo:
- Kunywa chai ya mimea japo aina mbili kwa siku (Two antioxidant herb teas a day). Aina hii ya chai ina kemikali ambazo huvunja nguvu ya free radicals mwilini. Chembe hai zinazojenga mwili wa binadamu zinakabiliwa na hatari kubwa tatu. Kukosa chakula, kushambuliwa na vijidudu vya maradhi na kuteketezwa na kemikali za free radicals.Free radicals ni chanzo kikubwa cha magonjwa sugu kama vile saratani na magonjwa ya moyo.Bila ya kupenda, mwili huzalisha free radicals pale chakula kinavyotumika kuzalisha nishati, chakula kinavyo mengenywa tumboni, hewa inavyoingia mwilini na jua linavyopiga katika ngozi na macho. Badala ya kupendelea kunywa kahawa au chai ambayo ina caffeine kunywa herb teas za oregano, rosemary, bee balm, lemon balm, peppermint, sage, spearmint na tyme. Unaweza kuchagua kati ya herbs hizo japo mbili na kuzichanganya kwa kiwango sawa na kisha kunywa kama chai. Unaweza kupata herbs hizo kwenye maduka ya vyakula au supermarkets.
- Kula japo mlo mmoja mkubwa wa saladi kwa siku. Mboga kijani za majani (green leafy vegetables) zina kiwango kikubwa cha antioxidant nutrients ambazo huupa mwili askari wa kupambana na free radicals, kama vile maji yanavyozima moto. Askari hao ni pamoja na vitamini C, vitamini E, beta-carotene, madini ya selenium na manganese. Nutrients hizo hukinga mwili dhidi ya magonjwa kama saratani, magonjwa ya moyo na magonjwa mengine ambayo hutuwapata binadamu kadri umri unavyosonga.
- Kula mbegu za alizeti (sunflower seeds) kiasi cha mkono mmoja (a handful) na nuts zingine. Mbegu za alizeti zina vitamin E na ni rahisi kupatikana na bei yake ni nafuu.
- Kula broccoli spear (broccoli mkuki) moja, karoti moja na shina moja la celery (celery stalk) kila siku. Mboga hizi zina nyuzi (fiber) nyingi. Broccoli na karoti zina beta-carotene nyingi ambayo ni antioxidant. Celery ina kemikali nyingi aina ya apigenin ambayo husaidia kutanua (dilates) mishipa ya damu mwilini hivyo kuepusha mtu kupatwa na high blood pressure.
- Kunywa fruit smoothie kila siku. Itengeneze kwa kutumia tunda lolote kadri upendavyo. Matunda hayo ni pamoja na apples, machungwa, ndizi, balungi, tikiti au berries. Itengeneze kwa kutumia blender na sio juicer ili kuhakikisha smoothie yako inakuwa fiber ambayo ni nzuri katika kuwezesha uyeyushaji wa chakula mwilini. Ukipenda pia kwenye smoothie yako unaweza kuweka pia yogurt na unga wa mdalasini.
- Tumia mafuta ya mizeituni kwenye saladi yako.
- Kula matunda na mboga za majani aina mbalimbali.
- Fanya mapenzi mara kwa mara na yule umpendaye.
- Fanya zoezi la matembezi angalau nusu saa kila siku. Epuka kufanya matembezi kwenye jua kali.
- Epiuka kuvuta sigara na kunywa pombe.
- Usiotee jua (Don't sunbathe).
No comments:
Post a Comment