Saturday 22 August 2015

Usiteseke, Tiba ya Magonjwa ya Ngozi kwa Kutumia Mimea Hii Hapa!


Zipo aina mbalimbali za magonjwa ya ngozi yanayowapata binadamu. Magonjwa hayo ni pamoja na  chunusi (acne, pimples, blackheads), mabaka (blemishes), chunjwa (warts) na makunyanzi (wrinkles). Watu wengi wanapopatwa na magonjwa ya ngozi huwa wanafikiria kwa haraka kwenda hospitalini kutibiwa. Wengine wametibiwa lakini tiba za hospitalini hazijawasaidia. Lakini jambo la kustaajabisha ni kwamba tiba rahisi ya magonjwa ya ngozi tunayo lakini hatutambui kuwa tunayo. Ni tiba rahisi ambayo siyo ya gharama kubwa  tena ni tiba salama kwa maana kwamba haina madhara mwilini. Ni tiba inayotokana na mimea kwa maana ya matunda, mizizi au mjani ya mimea ambayo ni vyakula na viungo tunavyotumia kila siku bila kufahamu kuwa ni tiba kama tukiitumia kwa namna ipasayo. 

Nitakwenda kueleza tiba hizo kwa magonjwa mbalimbali ya ngozi kwa kutumia mimea ambayo ni vyakula. Ni rahisi sana kuvipata hivyo vyakula katika maeneo ya sokoni, magengeni au supemarkets. 

ACNE

  1. Tango (cucumber): Husaidia kusafisha damu hivyo ni tiba nzuri kwa tatizo la chunusi (acne).
  2. Kitunguu Swaumu (Garlic): Saga (mash) punje kadhaa za kitunguu swaumu na paka eneo la ngozi liliothirika na chunusi. Pia hutibu boils, corns kwenye miguu na warts.
  3. Chungwa: Saga maganda ya machungwa kisha changanya na maji halfu paka eneo la ngozi lililoathirika na pimples na acne.
BLACKHEADS, PIMPLES
  1. Chukua unga wa turmeric kijiko kidogo weka kwenye juisi iliyotengenezwa kutokana na majani ya coriander, tengeneza paste kisha paka hiyo paste kama face pack kwenye eneo la uso liliothirika kwa blackheads au pimples usiku kabla ya kwenda kulala. Asubuhi nawa uso wako kuondoa hiyo paste uliyopaka usiku.
  2. Kwa kutibu madoa meusi, mabaka na chunusi paka jusi ya ndimu eneo la ngozi liliothirika usiku kabla ya kulala. Asubuhi nawa eneo lililoathirika.
  3. Changanya unga wa mdalasini na sand wood oil (kiasi cha kijiko kikubwa) Paka hehemu ya ngozi. Tiba hii ni nzuri kwa wonye tatizo la ngozi (acne, blackheads na pimples).
  4. Kwa tatizo la pimples: Changanya kiasi sawa cha kungumanga (nutmeg), pilipili manga na sandwood na paka eneo lililoathirika. 
RASHES
  1. Tengeneza paste ya coriander na paka eneo lililoathirika.
  2. Bamia: Tengeneza paste ya bamia na paka eneo la ngozi lililoungua moto na pia rashes. 
MAKUNYANZI NA KUOTA MVI MAPEMA
  1. Loweka au weka (soak) tangawizi uliyoipondaponda kwenye asali. Kula asali hiyo kijiko kimoja kikubwa kila siku.
  2. Tengeneza paste ya viazi (potato) kisha paka kwenye eneo la ngozi lililoathirika. 
  3. Tengezeza paste ya viazi (raw potato paste na paka sehemu ya ngozi ilipoathirika.

4 comments:

  1. DAWA ASILI ZA CHUNUSI MAPUNYE ,,MAPELE.,PUMU..BP..KISUKARI,,BWAWASIRI..MVUTO..,NGUVU ZA KIUME ,,UGUMBA,,UTI SUGU,,MVUTO,,KUREFUSHA NA KUNENEPESHA UUME WASILIANA NA DR TIBA ASILI TOKA TANGA 0764839091

    ReplyDelete
  2. Dr me kun mafta nlikuwa natumia naona yamenchubua nlikuw naulzia kam kuna dawa inayoweza kunrudisha ktk NGOs yng asil

    ReplyDelete
  3. Mimi Dr. Nina vidoa doa vyeupe usoni ,, nitatibuje??

    ReplyDelete
  4. Blemishes inatibika kwa kutumia mmea gani

    ReplyDelete