Sunday 29 November 2015

Tengeneza na Tumia 'Herbal Facial Mask' Kwa Ngozi Nyororo

Nimekuwa nikipokea maswali mengi hususan kutoka kwa akina dada kuhusu namna ya kufanya laini au nyororo ngozi zao za uso na kuondokana na chunusi (acne) au mikunjo ya ngozi (wrinkles) au miwasho. Najua wengi wamehangaishwa na chunusi, miwasho au mikunjo ya ngozi usoni na wametumia mafuta au madawa mbalimbali, yamkini mengine yenye kemikali.

Ngoja nitoe maelekezo ya jinsi ya kutengeneza 'herbal facial mask' isiyo na kemikali yoyote zenye madhara kwa mwili wa binadamu.  Haya fanya haya yafuatayo:
- Changanya unga wa tangawizi (powdered ginger) vijiko viwili vidogo na vijiko vinne vya asali (kama una ngozi kavu - dry skin) au juisi ya ndimu freshi (kama ngozi yako ni ya mafuta mafuta).
- Koroga kutengeneza paste.
- Paka usoni, ukiwa makini na maeneo ya mdomo na macho.
- Kwa matokeo mazuri zaidi acha mask ikae kwa dakika 15. Baada ya hapo safisha uso wako wa maji vuguvugu. 
- Baada ya hapo unaweza kutumia 'Papaya exfoliant' kulainisha zaidi ngozi. Papaya exfoliant unachukua uji uji wa nyama ya ndani ya papai. Paka usoni na uiache kwa dakika 15 kisha uoshe uso. 
Hakika ngozi ya uso wako itakuwa murua haswaaa...   

No comments:

Post a Comment