Monday 16 May 2016

Faida ya Papai Kwa Afya ya Mwili na Tiba ya Magonjwa

Image result for picture of pawpaw fruitPapai husaidia kuyeyusha chakula mwilini kutokana na kuwa na kimeng'enya kiitwacho 'papain'. Tunda hili pia lina vitamin A na C (antioxidants). Mbali na faida hizo kwa mwili wa binadamu tunda hilo pia ni tiba kwa magonjwa mbalimbali. Mathalani, mbegu za papai hutibu kuharisha (dysentery) na minyoo kwenye njia ya mfumo wa chakula (gastrointestinal tract). Pia mizizi ya papai hutibu gono (gonorrhea).

Kadhalika watu wanaosumbuliwa na maumivu ya viungo (Arthritis) na magonjwa au matatizo mengine kama mzio (allergy) asthma, hypertension, maumivu ya jino, na watu wenye tatizo la kupatwa na wasiwasi (chronic anxiety), tatizo la kinga ya mwili kuwa ndogo (low immunity), mwili kukosa nguvu, na uchovu (chronic fatigue) wanashauriwa kula papai kila siku au mara kwa mara. Kwa maneno rahisi watu wenye matatizo hayo walifanye papai kuwa rafiki yao wa karibu. Wanashauriwa kula papai asubuhi kabla ya kula chakula chochote, au watumie kijiko kidogo cha unga wa mbegu za papai baada ya kula chakula.

Tunda hili pia kusaidia kupona haraka kwa watu wenye matatizo ya vidonda (wounds), na pia ni msaada kwa watu wenye kansa ya ngozi. Watu hao wanashauriwa kutwanga majani ya mpapai na kupaka sehemu ya mwili iliyoathirika.

Monday 28 December 2015

Tengeneza Na Kunywa Juisi Hii Kwa Ngozi Yenye Afya na Mng'ao Mzuri


Image result for beautiful black skin photoKila mtu hasa wanawake wanapenda kuwa na ngozi nzuri yenye afya na mng'ao angavu! 

Bila kupoteza muda kwa maneno mengi, tengeneza mojawapo wa aina hizi za juisi:

MOJA: Chukua karoti 4 zimenye na katakata vipande vipande, Chukua kiazisukari (beet root) kimoja na kikate vipande vipande na robo inchi ya mzizi wa iliki (ginger root). Weka vitu vyote hivyo kwenye blenda, kisha saga juisi. Jenga mazoea ya kunywa juisi hii utaona faida yake kwa ngozi yako.

PILI: Chukua vipande vya nanasi kiasi cha kikombe kimoja, Menya embe moja na kata vipande vipande, Menya tango moja na kata vipande vipande na nusu limao (usilimenye). weka vitu vyote hivyo kwenye blenda na saga juisi. 

Friday 25 December 2015

Unajua Madhara ya Dawa za Kusimamisha Uume Kwa Muda Mrefu?

bizarre potato stock photoKuna baashi ya wanaume wanatamani wakati wakiwa wanafanya mapenzi na wenzi au wapenzi wao basi mboo zao ziwe zinasimama muda mrefu mathalani masaa matatu au manne au zaidi huku wakimwaga shahawa eti tu wawaridhishe wenzi wao au ili waonekane ni wanaume waliokamilika. Wanaume wengine wamekuwa wakitumia dawa za kusimamisha mboo kama vile viagra au dawa za asili na zingine maarufu kama dawa za kimasai! Napenda nikwambie kwamba hizo dawa zina madhara makubwa kwa urijali wako na uko hatarini kuupoteza hata huo urijali mdogo uliosalia!



Kusimamisha mboo kwa muda mrefu na mara nyingine kiasi cha kufikia mboo inaanza kuuma kutokana na kusimama muda mrefu tayari ni ugonjwa. Kwa maneno rahisi ni kwamba umetumia dawa za kuongeza nguvu ili kuua nguvu chache ulizokuwa nazo. Kitalaamu hali hiyo ya mboo kusimama muda mrefu na kuuma inaitwa 'Priapism'. Priapism hutokea pale mboo inapopoteza uwezo wake wa kuondoa damu iliyoko kwenye mboo hiyo (ambayo hufanya isimame) ili isinyae (in order to become flaccid). Hiyo hali ikidumu kwa muda wa masaa manne husababisha seli za damu iliyoko kwenye mboo kukosa hewa ya oksijeni, hivyo kupelekea tishu katika mboo kufa. Na kadri hali hiyo inavyoendelea hupelekea damu kwenye mboo kuwa na asidi na hivyo kukosa uwezo wa kusafiri au kutembea kwenda sehemu zingine za mwili hususan kwenye moyo! Hapo hali inakuwa mbaya sana!

Kuna wanaume wengine wanaji-overdose viagra au madawa ya kienyeji ili wawe wanaume shababi kwelikweli kumbe ndio wanaua mboo zao. Ndio maana watu wanaotumia madawa hayo baada ya muda fulani hali zao za kiume zinakuwa mbaya zaidi afadhali ya jana! Ndio maana humu katika blog nimesisitiza sana matumizi ya vyakula na viungo kama tiba ya tatizo la ngivu za kiume! Siwashauri kutumia hayo madawa, otherwise, keep using them for your own risk!

Bahati mbaya au vyovyote vile kama umesimamisha mboo masaa kadhaa hakikisha katika kipindi cha ndani ya masaa manne tafuta tiba haraka kwa daktari! Wengine baada ya kutumia hayo madawa na mboo kusimama kama msumari masaa mengi wao hudhani dawa ni kufanya mapenzi masaa mengi na mwanamke ili kuondokana na hali hiyo! Tena wengine ndo hufurahia eti 'leo mwanamke fulani nitamfaidi kweli...'. My brother you are killing yourself'!!! Hutoweza kumkomoa mwanamke kwa kufanya mapenzi! Matibabu ya tatizo hilo ni kunyonya damu kwa kutumia sindano itakayochomwa kwenye mshipa wa damu uitwayo vein kwenye mboo yako! Mwisho nakushauri kula sana vyakula vya asili kama matunda na mboga za majani. Usisahau mazoezi ya viungo. Next time tutaona namna ya kukabiliana na tatizo la nguvu za kiume ingawa nimegusia gusia katika bloga hii katika mada kadhaa!

Sunday 29 November 2015

Tengeneza na Tumia 'Herbal Facial Mask' Kwa Ngozi Nyororo

Nimekuwa nikipokea maswali mengi hususan kutoka kwa akina dada kuhusu namna ya kufanya laini au nyororo ngozi zao za uso na kuondokana na chunusi (acne) au mikunjo ya ngozi (wrinkles) au miwasho. Najua wengi wamehangaishwa na chunusi, miwasho au mikunjo ya ngozi usoni na wametumia mafuta au madawa mbalimbali, yamkini mengine yenye kemikali.

Ngoja nitoe maelekezo ya jinsi ya kutengeneza 'herbal facial mask' isiyo na kemikali yoyote zenye madhara kwa mwili wa binadamu.  Haya fanya haya yafuatayo:
- Changanya unga wa tangawizi (powdered ginger) vijiko viwili vidogo na vijiko vinne vya asali (kama una ngozi kavu - dry skin) au juisi ya ndimu freshi (kama ngozi yako ni ya mafuta mafuta).
- Koroga kutengeneza paste.
- Paka usoni, ukiwa makini na maeneo ya mdomo na macho.
- Kwa matokeo mazuri zaidi acha mask ikae kwa dakika 15. Baada ya hapo safisha uso wako wa maji vuguvugu. 
- Baada ya hapo unaweza kutumia 'Papaya exfoliant' kulainisha zaidi ngozi. Papaya exfoliant unachukua uji uji wa nyama ya ndani ya papai. Paka usoni na uiache kwa dakika 15 kisha uoshe uso. 
Hakika ngozi ya uso wako itakuwa murua haswaaa...   

Saturday 28 November 2015

Hii Ni Chai Ya Ajabu Inayosafisha TakaSumu Mwilini na Kutibu Magonjwa Mbalimbali


Miili yetu inaathiriwa na taka sumu (toxins) kutokana na vyakula tunavyokula, mabaki ya vyakula mwilini baada ya chakula kuyeyushwa na sumu zilizopo katika mazingira tunayoishi au kufanya kazi. Sumu hizi huendelea kuongezeka kiwango kadri muda unavyopita na hatimaye kupatwa na magonjwa makubwa kama vile shinikizo la damu, miguu kuuma, saratani, nk.
Dalili za watu wengi wenye matatizo yatokanayo na mwili kulemewa na sumu mwilini ni hizi:



  1. Tatizo sugu la choo kigumu (constipation)
  2. Kichwa kuuma kwa muda mrefu,msongo wa mawazo,hasira za mara kwa mara,ukosefu wa usingizi nk
  3. Misuli kuuma sana na uchovu usio ambatana na dalili za msingi za magonjwa ambukizi kama malaria UTI nk
  4. Tumbo kujaa gesi
  5. Vichocheo vya kike kuvurugika na kupelekea kupata ugumba
  6. Kukosekana na nguvu za kiume
  7. Kutopungua uzito hata pale unapukuwa unafuata mlo sahihi
  8.    Sukari,presha kutoshuka bila kujali upo kwenye matibabu
  9. Allergy na vyakula mbalimbali na mafua ya muda mrefu
  10.  Magonjwa sugu ya ngozi kama pumu ya ngozi,psoriasis,vertiligo nk
Inaweza kuwa hauna dalili hizo lakini ni busura kujua kuwa upo katika mazingira hatarishi na inaweza kuwa ukawa na kiwango flani cha sumu hizi ambapo kiwango tu kinachohitajika kuleta dalili hakijafikiwa,kikifikiwa dalili utaziona.

 Nina habari njema kwako mpendwa. Tunayo Chai ya Ajabu (Detox Tea) yenye faida tiba mbalimbali mwilini kama hizi:
  • Hutoa(flush out) taka sumu mwilini kupitia figo. Umewahi kusikia tatizo la figo kufeli yaani kushindwa kufanya kazi? Tatizo lilianza na mlundikano wa taka sumu kwenye figo.
  • Hutibu tatizo la choo kigumu au kukosa choo na chakula kushindwa kuyeyuka mwilini (Poor digestion).
  • Hutibu maumivu ya viungo na maumivu ya miguu au miguu kuwaka moto.
  • huepusha kupatwa na saratani (Cancer).
  • Husaidia kuondoa tatizo la kukosa usingizi (insomnia).
  • Hushusha blood pressure (BP) iliyopanda
  • Hutibu maumivu ya tumbo kwa watoto.
  • Hutibu maambukizi ya kibofu na njia ya  mkojo, kama vile UTI.
  • Huchochea afya ya mfumo moyo na mishipa ya damu (cardiovascular system).
  • Hutibu tatizo la tumbo kujaa gesi (bloating)
  • Ina antioxidants na bioflavonoids nyingi sana.
  • Haina caffeine.
Chai hii inafaa kwa mtu yeyote kwani sio mpaka usubiri upatwe na tatizo ndio uhangaike kutafuta tiba kwenye taasisi za afya tena kwa gharama kubwa yamkini. 

Bei ni Nafuu Sana Kulinganisha na Faida zake Lukuki.

Nipigie kwa simu: +255 688 30 88 40   

Sunday 8 November 2015

Juisi ya Limao na Iriki kwa Tiba ya Baridi Yabisi (colds), Mafua (Flu) na Vidonda vya Koo



Umewahi kupatwa na Baridi yabisi (Colds), Mafua (Flu) au Vidonda vya Koo (Tonsillitis)? Mara moja utawaza kukimbilia duka la madawa kununua dawa! Lakini mbona jikoni kwako kuna dawa? Jikoni kwako au katika kibanda cha jirani kunapatikana limao (lemon) na iriki (ginger) ambavyo ni ingredients nzuri kwa kutengeneza juisi inayoitwa 'Hot Ginger Lemonade' ambayo ni tiba nzuri sana kwa magonjwa au matatizo hayo!
Jinsi ya Kutengeneza: Katakata Iriki vipande vipande kiasi cha kujaza kikombe kidogo. Weka vipande hivyo kwenye maji lita moja na chemsha kwa dakika 10 hadi 15. Kisha ipua na miminia juisi ya limao uliyoikamua (fresh-squeezed lemons) na weka asali kwa ajili ya utamu. Nyunyizia unga kidogo wa pilipili (cayenne pepper). Dawa yako iko tayari. KUNYWA! Unaweza kutumia mara tatu kwa siku hadi upone.

Thursday 5 November 2015

MWANAMKE FANYA MAZOEZI YA KUKAZA MISURI YA UKE

black is beautiful 6 Black is Beautiful (36 Photos)
Kama ilivyokuwa kwa baadhi ya wanawake kuwasema na kuwacheka wanaume wenye “vibamia” hali kadhalika na wao huwa wanacheka na kusema wanawake wenye “Kuma” kubwa/pana wakidai kuwa hawafurahii kwa vile haibani na kupoteza ule msuguano ambao ndio chanzo cha raha na hatimae utamu.

Natambua kuwa ni jambo linalotia aibu kama ilivyokua kwenye suala zima la ngono lakini hili ni tatizo ambalo linasumbua wanawake wengi. Hili tatizo mara nyingi hutokea au kujitokeza mara baada ya kuzaa watoto 2 na kuendelea.
Hakuna sababu ya wewe kuona aibu ikiwa una tatizo hili hasa pale unapokwenda kumuona daktari wako kwani wanatambua kabisa nini huwa kinatokea baada ya kuzaa.
Ukiwa mtu wa kufanya mazoezi au ulikuwa mtu kwa kufanya mazoezi kabla hujapata mtoto huwa rahisi kurudisha u-tight wa misuli ya uke wako kwa kufanya mazoezi ya kukaza misuli ya tumbo pamoja na yale maalumu kabisa yanayoitwa Kegel.

Zoezi hili limepewa jina la Kegel baada ya Dr.Arnold Kegel ambae ni “Obstetrician” alietambulisha zoezi hili kama sehemu ya kuwasaidia akina mama wajawazito kuboresha na kukaza misuli ya uke ambao huwasababishia kuvunjwa kwa mkono pale wanapocheka, kohoa, piga chafya n.k. mara baada ya kujifungua.

Baada ya miaka michache imegundulika kuwa zoezi hilo lijulikanalo kama Kegel husaidia kurudisha “mnato” wa uke pia na wengi hufanikiwa kurudisha ule “u-tight” wa uke hali inayowafanya wajiamini wanapofanya mapenzi na vilevile kuwafanya wapenzi wao na wao wenyewe kufurahia kama ilivyokuwa awali (kabla ya kuzaa).

Misuli inayofanyiwa zoezi hili ni ile iliyozunguuka uke, njia ya mkojo na sehemu ya haja kubwa(mkundu).
Unajua unapokunya (toa haja kubwa) ile ngumu au hata ya kawaida huwa huliachii mpaka liwe reefu kama na mara nyingi unakata kimba hilo, ukilikata lile "javi " sehemu yako ya nyuma (mkundu) inakuwa kama vile ina "hema" au "inamwenyua-mwenyua" samba-mba na ile ya mbele....sasa unatakiwa kufanya hivyo mara nyingi uwezavyo ukiwa mahali popote na sio wakati unakunya. Lakini kumbuka ku-hold na kuachia....sio unafanya haraka-haraka ili uwahi kumaliza.

Hali hiyo ya mkundu na Kuma "kuhema" pia hujitokeza wakati ukisikilizia utamu wa kufanya mapenzi mara tu baada ya uume unapotolewa haraka ukeni pale unapofika.....hasa ikiwa Mpenzi anataka kumaliza lakini kwa nje.
Vilevile unaweza ukalifanya zoezi hilo kila unapokwenda kukojoa, jaribu kuzuia mkojo usitoke kwa kutumia misuli yako ya uke kwa muda wa dakika fulani....kwamba uzuie kisha hesabu 1....2....3....4...5...6 kisha uachie na rudia tena mpaka mkojo wote uishe.

Zoezi hili halifanywi na wenye uke mpana na wenye maji-maji mengu tu bali na mwanamke yeyote ili kuboresha maisha yake ya kingono na mpenzi wake.
Ikiwa unafanya haya mazoezi mara kwa mara yatakusaidia kumpatia mpenzi wako kilele cha maana kwa kubana-vuta na kukamua uume wake kila unapo ingia deep inside na vile vile kunaendeleza mnato wako na ikiwa wewe ni kati ya wale wanawake wenye maji-maji mengi basi unaweza kutumia misuli yako hiyo kuubana uume na kumpatia utamu na raha mpenzi wako ambayo hajawahi kuipata toka umaji-maji ujitokeze.

Nitajuaje kama nimepatia?
Ni rahisi, ingiza kidole kisha fanya Kegel na utahisi kidole chako kikibanwa na kuachiwa.
Fanya zoezi hili kila siku, mahali popote na utapata matokea(utaona mabadiliko) ndani ya miezi miwili hadi minne kwa wale wenye uke mpana.

Ikiwa wewe uke wako uko sawa (sio mpana)na unafanya Kegel ili kuongeza raha ya kufanya mapenzi basi itakuchukua wiki moja. Hakikisha unafanya zoezi hili kila wakati unapofanya mapenzi na hakikisha anapokaribia mbane-mwachie na kamua "cream" yote.

Pia Kegel inaweza ikafanywa kwa kulala chali, weka mikono huku nahuku kisha ipumzishe kwenye sakafu alafu kunja miguu yako sehemu ya magoti na vikanyagio viwe sambamba kwenye sakafu kisha inua kiwili-wili chako kwenda juu baki hapo juu (huku ukiwa umebana msuli ya uke kama vile unazuia mkojo usitoke) kwa muda kisha rudi chini na rudia tena kadiri uwezavyo.

Monday 2 November 2015

Kifafa cha Mimba (Preeclampsia, eclampsia)

Kifafa cha mimba ni ugonjwa unaohusiana na msukumo mkubwa wa damu (high blood pressure) wakati wa ujauzito pamoja na kuharibika kwa viungo muhimu mwilini kama vile figo na ini. Kwa kawaida ugonjwa huu hutokea baada ya nusu ya kwanza ya ujauzito kuisha (kuanzia wiki ya 20 au miezi mitano ya ujauzito).
Ugonjwa huu huweza kuwatokea hata wajawazito ambao hawakuwa na tatizo la msukumo mkubwa wa damu kabla ya ujauzito.

Ugonjwa wa kifafa cha mimba unaweza kuleta madhara makubwa kwa mjamzito na mtoto aliye tumboni. Kuharibika kwa viungo muhimu kama figo na ini la mjamzito kunaweza kuwa kwa kiwango kikubwa kichoweza kusababisha mjamzito kupoteza maisha iwapo hatapata huduma ya afya mapema. Vilevile mtoto aliye tumboni anaweza kuathirika kwa kukosa damu ya kutosha toka kwa mama na kushindwa kukua vizuri na iwapo hali hiyo ikiendelea muda mrefu anaweza kufia tumboni.

Kutokana na hatari kubwa ya ugonjwa huu kwa wajawazito na watoto walio tumboni, inashauriwa kila mjamzito awe anahudhuria clinic na kupimwa msukumo wa damu (blood pressure) na mkojo ili kuhakikisha kuwa yuko salama. 
Iwapo kipimo cha msukumo wa damu ni kikubwa kuliko 140/90 mmHg, ni muhimu kurudia kipimo hicho baada ya muda na kufanya vipimo vingine vya maabara vinavyoweza kujulisha uwepo wa kifafa cha mimba.


Kwa kawaida ugonjwa huu huwepo kwa muda fulani bila mjamzito kuona dalili zozote. Ghafla mjamzito anaweza kuanza kuona dalili kama maumivu ya tumbo juu ya kitovu, kutapika, macho kutokuona vizuri, kuumwa kichwa, mkojo kuwa na rangi tofauti na kawaida, kupumua kwa shida, uchovu na maumivu ya viungo au kupoteza fahamu na “degedege“. 
Kila mjamzito mwenye dalili hizi ni muhimu aonwe na mtaalam wa afya ili apimwe na kupewa ushauri.


Sababu ya ugonjwa huu kutokea hazijulikani mpaka sasa ingawa zipo nadharia mbalimbali zinazojaribu kuelezea kutokea kwake. Mojawapo ya nadharia hizo inaelezea kuwa ugonjwa huu hutokana na matatizo ya ukuaji wa kondo la nyuma (placenta). Mishipa ya damu inayounda placenta ikikosea jinsi ya kujikita kwenye ukuta wa kifuko cha uzazi husababisha mishipa hiyo kuwa na tabia tofauti na ile ya kawaida na kusababisha mjazito kupata msukumo mkubwa wa damu na kifafa cha mimba. Kwa vile ugonjwa huu huonekana kutokea zaidi kwenye familia fulani kuliko nyingine, inaaminika kuwa urithi pia huchangia kupata ugonjwa huu. Hii inamaanisha mjamzito ambaye mama yake aliwahi kupata kifafa cha mimba ana uwezekano mkubwa zaidi wa kupata kifafa cha mimba.

Wanawake ambao wana tatizo la msukumo wa damu, kisukari, unene kupita kiasi, ugonjwa wa figo kabla ya ujauzito wana uwezekano mkubwa zaidi wa kupata kifafa cha mimba. Kwa sababu hii, wanawake wote wenye matatizo haya wanashauriwa kufuatiliwa kwa karibu na mtaalam katika kipindi chote cha ujauzito.

Mjamzito aliyepata kifafa cha mimba kwenye ujauzito uliopita, ana uwezekano mkubwa wa kupata tena.
Imegundulika kuwa iwapo mwanamke anazaa na mwanaume mwingine tofauti na aliyezaa naye awali, uwezekano wa kupata kifafa cha mimba huongezeka.
Ujauzito kwa mwanamke mwenye umri zaidi ya miaka 40 huongeza uwezekano wa kupata kifafa cha mimba.

Ingawa hakuna kinga ya uhakika ya kifafa cha mimba, wanawake walio kwenye makundi hayo yaliyoyotajwa hapo juu kuwa na uwezekano mkubwa wa kupata ugonjwa huu wanaweza kujikinga kwa kutumia vidonge vya aspirin na madini ya calcium. Kabla ya kutumia dawa hizi ni muhimu kupata ushauri wa kitaalam.
Tiba pekee ya kifafa cha mimba ni kumzalisha mjamzito. Hii ni kwa sababu ugonjwa huu husababishwa na kuwepo kwa kondo la nyumba ndani ya kifuko cha uzazi. Bila kutoa kondo la nyuma mgonjwa hawezi kupona.

Iwapo ugonjwa huu utagundulika kabla mtoto hajakomaa na kuwa tayari kwa kuzalishwa. 
Daktari anaweza kushauri mjamzito alazwe na kuangaliwa kwa ukaribu wakati ikisubiriwa kukomaa kwa mtoto. Vilevile daktari anaweza kushauri mjamzito apewe dawa ya kuharakisha kukomaa mapafu ya mtoto.


Iwapo hali ya mjamzito ikibadilika na kuwa mbaya, kumzalisha huweza kuwa ni lazima hata kama mtoto hajakomaa kwa sababu kuna hatari kubwa ya mama na mtoto kuathirika iwapo ujauzito utaendelea. 
Mojawapo ya hatari inayoweza kutokea iwapo ujauzito utaachwa kendelea ni mtoto kufia tumboni, kupoteza fahamu kwa mjamzito na kupata dalili za “degedege“, damu kupoteza uwezo wa kuganda na kusababusha mjamzito kupoteza damu nyingi, damu kuganda mwilini na kuziba mishipa, kondo la nyuma kujitenga na kifuko cha uzazi kabla ya mtoto kuzaliwa, figo za mjamzito kushindwa kabisa kufanya kazi, mjamzito kupata kiharusi (stroke) au mjamzito kupoteza maisha.


Kwenye kumzalisha mama mwenye kifafa ch mimba njia mbalimbali huweza kutumika kutegemeana na hali ya mjamzito. Kama hali sio mbaya sana na njia ya uzazi imeshaanza kufunguka, mjamzito anaweza kupewa dawa za kuanzisha uchungu na kujifungua kwa njia ya kawaida. 
Kujifungua kwa njia ya operesheni hulazimika kwa wajawazito wenye msukumo mkubwa sana wa damu na wale ambao hali zao sio nzuri au kunapokuwepo na sababu nyingine ya kujifungua kwa operesheni.

Kabla ya kujifungua, mjamzito mwenye msukumo mkubwa wa damu hupewa dawa za kupunguza msukumo wa damu.
Ili kuzuia uwezekano wa kupata “degedege“, daktari anaweza kushauri mgonjwa apewe madini ya magnesium kwa njia ya dripu.


Kwa sababu ugonjwa wa kifafa cha mimba huongeza uwezekano wa damu kuganda mwilini, daktari anaweza kushauri mgonjwa atumie dawa ya kuzuia damu kuganda.
Baada ya kujifungua, msukumo wa damu unategemewa kurudi kwenye hali yake ya kawaida katika muda wa masaa 24. Hata hivyo ni vizuri mama aliyejifungua katika hali hii kuangaliwa kwa masaa 48 kabla hajaruhusiwa kwenda nyumbani. Hii hutegemea na uwepo na nafasi ya kulaza wagonjwa kwenye hospitali.

Kwa vile upo uwezekano wa msukumo wa damu kuendelea kuwa juu moja kwa moja. Mzazi hushauriwa kupima msukumo wa damu mara kwa mara, iwapo baada ya wiki sita (siku 40) itaonekana msukumo wa damu unaendelea kuwa juu, basi hushauriwa kuendelea na matibabu ya msukumo mkubwa wa damu kama wagonjwa wengine wenye ugonjwa wa msukumo mkubwa wa damu.

Saturday 24 October 2015

Utafanya Nini kumsaidia Mama Aliyejifungua Anayevuja Damu Nyingi?


Wanawake ni mama zetu. Kila binadamu amezaliwa na mwanamke baada ya miezi tisa ya kukaa ndani ya tumbo la uzazi la mwanamke. Licha ya mwanamke kukabiliwa na kipindi kigumu cha kutunza ujauzito kwa miezi tisa hadi kujifungua lakini mwanamke anakabiliwa na hatari ya kuvuja damu nyingi wakati wa kujifungua. Katika hali ya kawaida ya kujifungua mtoto mwanamke hapaswi kuvuja damu zaidi ya vikombe viwili yaani 240ml ya damu.
Endapo itatokea mwanamke kuvuja damu nyingi msaidie kwa kufanya mambo yafuatayo:

  1. Chukua unga wa pilipili iitwayo kwa kiingereza 'Cayenne pepper' kiasi cha robo kijiko cha chai weka kwenye maji moto glasi moja. Tia asali na limao. Mnyweshe kila baada ya dakika kumi.
  2. Mfanyie masaji ya tumbo kwa upande wa chini. Fanya masaji hiyo kwa kuzungusha vidole au viganja kwenye tumbo kama unachora duara kwenye tumbo (firm but gentle circular motion). Hii itasaidia mji wa mimba (uterus) kuwa mgumu na hivyo kupungua uvujaji damu! 

Huduma Ya Kwanza Kwa Mtu Aliyekula Au Kunywa Sumu


Mtu anaweza kula au kulishwa sumu katika mazingira mbalimbali. Kuna watu wengine huamua kujaribu kukatisha maisha yao kwa kunywa sumu kutokana na sababu mbalimbali za kimaisha. Lakini vyovyote iwavyo katika maisha yako au ya ndugu, jamaa na rafiki kukatisha maisha kwa kula au kunywa sumu sio suluhisho la kukimbia matatizo ya maisha bali ni kuingia kwenye matatizo makubwa mno kwani huko roho itakapokwenda ni MAJUTO MAKUU!

Endapo itatokea mtu amekunywa sumu au amekula chakula chenye sumu muwahishe hospitali au kituo cha afya haraka kama utaona hali hizi: kuwa na kichefuchefu, kutapika au kuharisha, damu kwenye kinyesi, kukosa mkojo, mate kuwa machache mdomoni na yenye mnato au macho kuingia ndani.

Wakati unafanya harakati za kumpeleka kwenye kituo cha afya, mpe tiba mojawapo ya hizi: Pia ukiona sumu sio kali sana maana mara nyingine tunaweza kula chakula lakini baada ya muda fulani tunasikia matumbo yanauma au tunaharisha, tumia tiba hizi:

  1. Changanya siki aina ya 'Apple cider vinegar' kijiko cha chai (15ml) kwenye maji ya moto au vuguvugu kiasi cha kikombe kimoja (230ml) kisha mpe anywe. Rudia kila baada ya masaa 2 - 3.
  2. Saga mkaa kisha chukua kiasi cha unga wa mkaa (500mg - 1g) changanya kwenye maji kikombe kimoja (230ml) mpe anywe. Rudia kila baada ya masaa 2- 3.
Kwa tumbo linalouma kutokana na sumu au chakula chenye sumu alichokula mtu anywe chai iliki au peppermint ili kutuliza tumbo. peppermint au iliki ni viungo vya vyakula vinavyopatikana sokoni au suppermarket. Apple cider vinegar ina matumizi mengi sana katika maisha yetu ya kila siku hivyo ni bidhaa muhimu kuwa nayo nyumbani kwako!

Monday 12 October 2015

Faida za Unga na Mafuta ya Ubuyu



Unga wa ubuyu unaelezwa kuwa na vitamini na madini mengi kuliko matunda mengine. Inaelezwa kuwa unga wa ubuyu una Vitamin C nyingi kuliko hata machungwa na ina kiwango kingi cha madini ya kashiamu (Calcium) kuliko hata maziwa ya ng’ombe.
Aidha, unga wa ubuyu ni chanzo kikubwa cha madini mengine aina ya chuma (iron), Potasiamu (Pottasium) na manganizi (magnesium). Inaelezwa kuwa kiwangao cha Potasiamu kilichomo kwenye unga wa ubuyu ni mara sita zaidi ya kile kinachopatikana kwenye ndizi. Ubuyu ni muhimu sana kwa watu wenye matatizo ya figo.
Vile vile unga wa ubuyu una uwezo mkubwa wa kuongeza kinga ya mwili  (antioxidant) kutokana na kuwa na kiwango kikubwa cha virutubisho vya kuongeza kinga mwilini dhidi ya magonjwa nyemelezi. Kiwango chake kinazidi hata kile kinachotolewa na matunda mengine kama vile Krenberi, bluberi na blakberi. Ili upate faida za unga wa ubuyu zinazoelezwa hapa, lazima ule ubuyu halisi usiochanganywa na kitu kingine cha kuongeza ladha.


MAFUTA YA UBUYU
Mafuta ya ubuyu, ambayo hutengenezwa kutokana na mbegu zake, ni mazuri kwa kulainisha ngozi na kukarabati au kuponya ngozi iliyoathiriwa na magonjwa ya ngozi mbalimbali, ikiwemo fangasi, vipele na chunusi.
Mafuta ya ubuyu yana uwezo wa kuifanya ngozi kuwa nyororo na laini kutokana na kuwa na kiasi kingi cha mafuta aina ya Omega 3 na Omega 6 na ina kiasi kingi cha Vitamin A, D na E ambazo zote ni muhimu kwa ustawi na uimarishaji wa ngozi ya binadamu.
Mafuta ya ubuyu yanaelezwa kuwa na virutubisho vinavyoweza kuondoa mikunjo ya ngozi, mabaka, michirizi na hata makunyazi na kuicha ngozi kuwa mpya. Hutoa kinga dhidi ya uharibifu wowote wa ngozi unaoweza kujitokeza baadaye.


Kwa ufupi mafuta ya ubuyu yana Virutubisho vifuatavyo:
  • -Vitamin:  (Thiamin) vitamin B1, Riboflavin) B2, (Niacin) B3, kiasi kikubwa cha (Ascorbic Acid) Vitamin C, Vitamin A, Vitamin D, Antioxidant na Vitamin E (Tocopherol)
  • -Madini kama vile: – kiasi kikubwa cha Calcium, Manganese, Iron, Potassium, Zinc, Phosphorus, na Amino acids 

FAIDA ZAKE:- 

  • Yanakuongezea hamu ya kula na kukumbuka vizuri kwa ufasaha kutokana na kiwango kikubwa cha vitamin B complex zilizomo. kwa hiyo ni mazuri kwa wakubwa na watoto
  • Yanasaidia kunyonywa kwa vitamin B12 kwenye tumbo kutokana na kiwango kikubwa cha ascorbic acid, ambayo ni muhimu kwenye kutengeneza chembe hai nyekundu na kukuepusha na Anemia.
  • Yanasaidia kusafisha mfumo wa chakula na kufunga tumbo la kuhara zaidi kwenye unga  wa ubuyu kutokana na uwepo wa “roughage” nyingi.
  • Yanasaidia mtu  kuona vizuri kutokana na uwepo wa Vitamin A ndani yake.
  • Mazuri kwa Walemavu wa Ngozi kama (Albino) Kutokana na uwepo wa vitamin A, Vitamin D na Vitamin E (Tocopherol).
  • Ni mazuri pia kwa watoto wadogo na  wajawazito kwa ajili  ya kuimarisha mifupa hasa  kuanzia miezi sita hadi tisa ya ujauzito (third tremester), hiki ni kipindi ambacho mtoto anatengeneza na kuimarisha mifupa yake akiwa tumboni kwa mama yake, hii ni kwasababu ya kiwango kikubwa cha Calcium na vitamin D, na vitamin A.
  • Mafuta haya ni mazuri kwa kupunguza vitambi kutokana na uwepo wa Omega 3.
  • Hurekebisha kiwango cha sukari mwilini.
  • Hurekebisha shinikizo la damu (pressure).
  • Yanasaidia kuongeza kinga ya mwili yaani CD+4, zaidi kwa wagonjwa wa ukimwi, kansa, au watu waliougua kwa muda mrefu na wanawake wanapokuwa katika hedhi wanaweza kutumia.
MATUMIZI YA MAFUTA YA UBUYU:-Tumia vijiko viwili vya mafuta kwenye kijiko cha chai, kisha changanya kwenye glasi ya maji, juisi, maziwa,( yanaweza kuwa mtindi au freshi), soda, asali n.k, au unaweza kunywa bila kuchanganya na kitu kingine. Tumia hivyo  mara mbili kwa siku asubuhi na jioni kwa mafanikio mema na matokeo mazuri.
Mafuta ya ubuyu unaweza kuyatumia kwa kupaka usoni au mwili mzima moja kwa moja. Unaweza kuyatumia mafuta haya kwa kupaka sehemu tu iliyoathiriwa kama dawa. Unaweza pia kuchanganya na mafuta au losheni unayotumia.
Ili kupata matokeo unayotarajia, hakikisha unatumia mafuta halisi ya ubuyu ambayo hayajachanganywa na kitu kingine wakati wa kutengeneza.


UPATIKANAJI WAKE
Bidhaa za ubuyu zimeanza kujipatia umaarufu nchini Tanzania na hivi sasa kuna makampuni na wajasiriamali binafsi wanaojishughulisha na utengenezaji na uuzaji wa bidhaa mbalimbali zitokanazo na ubuyu, hivyo upatikanaji wake ni rahisi iwapo utaulizia maeneo unayoishi.
Bidhaa zingine zinazoweza kutengenezwa kutokana na mti huu ni pamoja na majani yake ambayo hutumika kama dawa, mizizi na magamba yake pia. Kwa ujumla mti wote wa ubuyu una faida na hakuna kitu kinachotupwa kwenye mti huu ambao ni miongoni mwa miti yenye matunda bora yaliyopewa jina la ‘superfruit’.

Wednesday 30 September 2015

Tibu Ugonjwa wa Shinikizo la Damu Na Magonjwa Mengine Kwa Kitunguu Swaumu


Image result for garlic photos

Kitunguu swaumu (Garlic) mpaka sasa kimeripotiwa kuwa na matumizi 125 ya kitabibu kwa binadamu. Matumizi yafuatayo ya kitunguu swaumu ndio yamefanyiwa utafiti wa kitalaamu wa kitabibu:

  • Kupunguza tatizo la damu kuganda katika mishipa ya damu (reduce blood clotting) na ugonjwa wa shinikizo la damu (blood pressure): tafuna punje ya kitunguu swaumu kila mara au tumia unga wa kitunguu swaumu kwa kuweka kiasi kwenye maji ya moto au chai na kunywa.
  • Kuzuia Saratani ya Tumbo (Stomach cancer): Kula mara kwa mara kitunguu swaumu husaidia kuepusha kupatwa na saratani ya tumbo.
  • Kinga ya Mwili (Immune system): Ulaji wa kitunguu swaumu husisimua utendaji kazi wa macrophages utendaji kazi wa T cells.
  • Husaidia kukakamaa kwa mishipa ya damu ya Arteries (Atherosclerosis), kupunguza cholesterol (blood lipids) na tatizo la mzunguko wa damu mwilini (peripheral vascular disease): Tumia mafuta ya kitunguu swaumu au tafuna punje za kitunguu swaumu mara kwa mara.
  • Kutibu Minyoo aina ya Threadworms: Saga punje kadhaa na weka kwenye glasi ya maziwa ya vuguvugu/moto na kunywa asubuhi kabla hujala chakula chochote.
  • Miguu kufa ganzi (Leg numbness) na Sciatica pain relief: Saga punje kadhaa za kitunguu swaumu au chukua kisi kidogo cha mafuta ya kitunguu swaumu weka kwenye glasi ya maziwa moto. Kunywa mara 1 - 3 kwa siku hadi utakapopata nafuu.

Saturday 26 September 2015

Usiteseke na Jino linalouma, Tiba Hii Hapa!

Meno ni muunganiko wa mfupa wa jino, Fizi na Mishipa. Maranyingi watu wengi huwa pale wanapoumwa na jino wanakimbilia kung’oa jino eti dawa ya jino kuling’oa jambo ambalo si kweli.
Tambua ndugu yangu kuwa unapokwenda kung’oa jino unang’oa Mfupa sio Fizi wala mishipa ambayo hakuna madhara kwa bakteria anaesababisha jino kuuma.
Tambua kuwa kwenye kinywa cha mwanadamu kuna bakteria wanaoishi mdomoni wanaitwa NORMAL FRALER. Bakteria hawa ndio wanaotengeneza ute wenye Acid unaolainisha chakula kwa haraka mdomoni. Na ndio kazi yao. Lakini wanasababisha ugonjwa unaoitwa GINGIVAITES, ugonjwa huu husababisha fizi kutoa damu haswa unapopiga mswaki, lakini ukiachwa ukawa sugu unasababisha ugonjwa wake kuwa sugu na hujulikana kama MACHODIFECE ugonjwa huu husababisha na hufanya meno kuoza, ama kutoboka kutokana na bakteria AFINOTOBALASAD ndio wanaosababisha na huwa wanaingia ndani kwenye fizi kwa ajili ya kula damu. Hapo ndipo mtu hupatwa na tatizo la  kuumwa na jino au meno.
 Ili kuondoa tatizo hili, ni lazima uwaue hao bakteria na si kong’oa jino kwani wadudu hao walivyo unapong’oa jino moja wao huwa wanahamia jino jingine.
Tiba rahisi ya jino au meno yanayouma bila kung'oa wala kutumia dawa za hospitali tumia mojawapo kati ya hizi hapa:
  1. Tengeneza na kunywa juisi ya bilinganya (Bringal).
  2. Jino linalouma au fizi zilizovimba: Ponda ponda tangawizi mbichi kisha itie chumvi. Weka kwenye jino linalouma au fizi ilipovimba.
  3. Saga majani makavu ya mint kutengeneza unga wake, kisha tia chumvi na weka kwenye jino linalouma.
  4. Saga karafuu kuwa unga. Weka kiasi cha unga huo kwenye jino linalouma. Pia kama una mafuta ya karafuu, chukua nyuzi za pamba (cotton wool) chovya kwenye mafuta hayo na weka wool hiyo kwenye jino linalouma.
Tiba hizi tunazo majumbani kwetu tunamoishi lakini tumekuwa hatujui kuwa ni tiba, badala yake huwa tunakimbilia kung'oa meno yanayouma! CHANGAMKA!



Friday 18 September 2015

Tatua Tatizo la Kunuka Kinywa Chako


Image result for white teeth photos
Afya ya mtu huanzia kwenye harufu ya mwili wake. Hakuna harufu inayoonyesha jinsi gani ulivyo msafi kama harufu ya kinywa. Je ulishawahi kuongea na mtu na ghafla ukajikuta unakosa hamu ya kuendelea sababu kinywa kinatoa harufu mbaya? Nafahamu kero hii inavyokuwa.

Kinywa ni muhimu kufanyiwa usafi wa hali ya juu ili kuhakikisha unapunguza harufu mbaya ya kukinaisha. Harufu ya kinywa, inakera na kuudhi. Kwa bahati mbaya huwa hatujui kama midoyo yetu inatoa harufu mbaya, bali wale tu wanaopata kuvuta hewa itokayo midomoni mwetu. Hii inakuwa ngumu kutatua tatizo sababu unaweza kudhani kila kitu kiko vizuri, kumbe unawapa watu wakati mgumu wakati wa mazungumzo. Harufu mbaya haifurahiwi, hasa ikiwa inatoka kwenye vinywa vyetu. Je nini kinasabisha vinywa kutoa harufu mbaya kiasi hiki? Hizi hapa sababu chache za kufanya kinywa kutoa harufu mbaya.

Kutosafisha vizuri kinywa vizuri

Kwa kawaida unatakiwa kusukutua kinywa chako angalau mara mbili kwa siku - asubuhi na usiku kabla ya kulala. Wakati wa kusafisha kinywa, hakikisha umesugua vizuri ulimi. Meno na fizi havina tatizo sana, bali ulimi ndio sehemu kubwa ambapo bakteria wanajijenga. Vilevile, ni ulimi unaosababisha kinywa kunuka. Ni vizuri kama utasafisha vizuri ulimi ili kuondoa harufu.

Ni vizuri kufahamu kuwa mswaki unatakiwa kubadilishwa kila baada ya muda - angalau kila mwezi. Usitumie mswaki kwa muda mrefu, maana hauwezi kusafisha kinywa chako kwa ufasaha kama inavyotakiwa maana wengine wanatumia mswaki kwa mwaka na zaidi. Je utaacha kunuka kinywa? 

Kutokula chakula vizuri

Harufu ya kinywa inaashiria kutokula chakula na kinywaji kwa muda mrefu. Kuwa na njaa husababisha mdomo kuwa mkavu. Mara nyingi harufu mbaya ya kinywa hupotea mara tu baada ya kula chakula kizuri na mdomo ukiwa una mate ya kutosha. Acha kutumia vyakula na vinywaji vinavyoongeza harufu kali mdomoni na kukupunguzia maji mwilini – mfano pombe, viungo kama kitunguu maji au kitunguu saumu.

Kinywa kikavu

Bakteria hushamiri kwenye kinywa kikavu. Kama hupendi kunywa maji mengi na kinywa chako kinakuwa kikavu mara nyingi basi jua kuwa kunuka kinywa kwako ni jambo la kawaida.

Jinsi ya kutatua tatizo

Hakikisha mdomo haukauki

Kwa kawaida mdomo mkavu hutoa harufu mbaya. Hii ndio sababu kuwa kinywa chako kinanuka sana asubuhi sababu mdomo wako unatengeneza mate machache sana ukiwa umelala. Mate ni adui wa harufu mbaya mdomoni siyo tu sababu inaondoa bakteria na masalia ya chakula, bali mate yana vimengenyo vinavyoua na kuzuia kuzaliana kwa vijidudu kwenye kinywa. Ili kuzuia kunuka, jaribu kufanya haya
  • Kunywa maji mengi ili kuondoa masalia ya chakula na bakteria
  •  Tafuna bazoka, sababu bazoka inasababisha mdomo kuwa na mate mengi. Kuwa makini katika kuchagua bazoka zisizo na sukari.  Sukari ni adui mkubwa wa kinywa chenye afya.

Piga mswaki kabla ya kulala

Kupiga mswaki ni muhimu, lakini wengi tunasahau kuwa mswaki ni lazima kupiga angalau mara mbili kwa siku haswa usiku naasubuhi.  Kupiga mswaki asubuhi ni muhimu ili kuondoa uchafu uliojijenga usiku kucha na hivyo harufu mbaya - lakini siku nzima mdomo unatengeneza mate na kuwa laini.  Hii ni tofauti na usiku. Usiku mdomo hubaki mkavu na mate kidogo, hivyo kuwa rahisi kwa vijidudu kuzaliana na kuharibu mazingira ya mdomoni kwako. Hivyo, ni afya zaidi kupiga mswaki usiku ili kuzuia kushamiri bakteria waharibifu wanaosababishwa na masalia ya bakteria kwenye kinywa chako.  Njia hii itasaidia kuzuia bakteria kuharibu meno na fizi, hivyo kutokuwa na harufu mbaya ya masalia wakati ukiamka.

Kula ndizi au apple

Ndizi au apple husaidia kuondoa harufu mbaya kinywani, lakini ni kwa muda mfupi sana. Ukiwa unahisi mdomo unanuka na unahitaji njia ya haraka, tafuta ndizi au apple, na hapo utakuwa umetatua tatizo kwa muda.

Kula Tango

Maji ya tango yana kemikali zinazozuia kukua kwa bakteria kwenye kinywa. Baada ya mlo mzuri wenye viungo vyenye harufu kali, kata kipande kidogo cha tango, kigandishe kwenye ukuta wa juu wa mdomo wako kwa sekunde 30 huku ukikandamiza na ulimi. Zoezi hili litasaidia kuua bakteria na kuacha kinywa chako kikiwa na afya na harufu nzuri.

Jenga Tabia ya Kupia Mabusu (Kissing)

Ni ukweli kuwa ukifanya kitu chochote kinachosababisha kutoa mate basi unazuia kunuka kinywa. Kissing ni mojawapo ya njia mbadala za kuzuia harufu mbaya mdomoni. Kiss mara nyingi uwezavyo ili kufanya mdomo wako uwe na mate mengi, na hivyo kuzuia kunuka kinywa.

Harufu ikizidi, kamuone daktari

Je harufu yako ya kinywa ni ugonjwa? Basi kamuone daktari. Wakati mwengine harufu ya kinywa hutokana na kuwa na matatizo mwilini na huwezi kuondoa kwa kutumia njia tulizozieleza hapo juu.

Wednesday 16 September 2015

Jinsi ya Kushughulikia Tatizo la Ugumba kwa Mwanamke kwa Njia ya Asili


Ugumba kwa mwanamke ni tatizo la mwanamke kushindwa kushika mimba licha ya kushiriki kufanya mapenzi na mwanamume bila kutumia kinga. Tatizo la kutoshika mimba kwa kipindi angalau mwaka mmoja huku mwanamke huyo akishiriki kikamilifu ufanyaji mapenzi na mwanamume huitwa ugumba (Sterility). Ugumba kwa mwanamke (Sterility) sio sawa au haina maana sawa na tatizo la mwanamke kutojisikia au kutokuwa na hisia za kufanya mapenzi yaani ‘Frigidity’.

Zipo sababu nyingi zinazoweza kufanya mwanamke awe mgumba. Mwanamume pia anaweza kuwa chanzo cha ugumba kwa maana kwamba hana uwezo wa kutungisha mimba. Hivyo, ndio kusema mwanaume kamwe hapaswi kumlaumu mwanamke anayeshirikiana naye kimapenzi kuwa ndiye ‘mgumba’ wakati mwanamume na mwanamke kwa pamoja wana asilimia sawa za kuwa chanzo cha ugumba. Ndio maana mwanamume na mwanamke wanapooana na wakashiriki ngono kikamilifu kwa kipindi cha mwaka mmoja lakini hakuna dalili za mwanamke kuwa mjamzito, basi wote wawili wanapaswa kwenda kwa pamoja kwa watalaamu wa masuala ya afya ya uzazi ili kuchunguzwa kwa kufanyiwa vipimo.

Ili mwanamke apate ujauzito mwanamume hukojoa shahawa kwenye uke wa mwanamke. Shahawa husafiri kwenye uke wa mwanamke kupitia mirija ya uzazi (fallopian tube) kwenda kurutubisha yai la mwanamke (ova). Sasa ili mbegu za kiume (sperms) ziwe salama wakati zinasafiri katika uke wa mwanamke lazima majimaji katika uke yawe katika hali ya nyongo (alkaline fluid). Kama majimaji ya uke yakiwa hayako katika hali ya nyongo yaani ni tindikali (acid) mbegu za kiume zitakufa na hakutokuwa na urutubishwaji wa yai la mwanamke.

Ili majimaji ya uke wa mwanamke yawe katika hali inayotakiwa ya alkaline mambo mawili ni muhimu sana. Moja, mishipa ya neva katika uke wa mwnamke iwe inafanya kazi zake sawasawa. Mwanamke mwenye mawazo sana (nervous) sio rahisi kupata ujauzito. Hivyo ili neva ifanye kazi sawasawa mwanamke hapaswi kuwa mtu mwenye mawazo au mwenye kuudhiwa, anapaswa kula milo kamili na anapaswa kuwa na muda wa kupumzisha akili yake (adequate rest and relaxation). Jambo la pili, mwanamke anapaswa kula vyakula vinavyotengeneza alkali katika mwili ambavyo ni mboga za majani na matunda, pia kuepuka kula kwa wingi vyakula vinavyoleta asidi katika mwili.

Sasa tuangalie visababishi vya tatizo la ugumba kwa mwanamke. Visababishi hivyo ni pamoja na mapungufu ya viungo vya uzazi vya mwanamke (physical defects or structural abnormalities of genitals and reproductive organs). Mwanamke anaweza kuwa ama amezaliwa na mapungufu hayo katika mji wa mimba (womb) au njia ya uzazi (fallopian tubes) au aliyapata kutokana na ajari. Sababu nyingine huitwa ‘Physical debility’ yaani mwanamke kutokuwa na afya bora ya mwili kutokana na magonjwa yaliyompata na yakadumu katika mwili wake wa kipindi kirefu (magonjwa sugu). Magonjwa hayo ni pamoja na magonjwa ya zinaa. Kadhalika upungufu wa damu (Anaemia), kukosa choo ipasavyo (constipation) au mwanamke kuwa na uzito mkubwa (obesity) au uzito mdogo ambao hautakiwi kitalaamu yaani kwa vipimo vya Body Mass Index (BMI) huweza kufanya mwanamke asipate ujauzito.

Visababishi vingine ni mwili wa mwanamke kutokuzalisha homoni muhimu za uzazi na kutokupata mzunguko mzuri wa hedhi (lack of normal menstrual cycle) sanjari na matatizo ya kisaikolojia hususan mwanamke anapoudhiwa au anapokuwa na mawazo kutokana na kutokuzaa mtoto mapema (emotional stress, tension, mental depression, anxiety, and fear).

Matibabu kwa visababishi aina ya ‘physical defects’ mwanamke anapaswa kwenda kufanyiwa vipimo na watalaamu wa masuala ya afya ya uzazi na kushauriwa ipasavyo mambo ya kufanya. Matibabu kwa visababishi aina ya ‘physical debility’ huweza kutibika kwa njia za kawaida tu kwa kula vyakula vinavyotakiwa, kujijali na kuuheshimu mwili (yaani usafi na kujikinga na maambukizi) na kufuata sheria za asili (laws of nature).

Mwanamke mwenye tatizo la ugumba ambalo sio la mapungufu katika viungo vya uzazi anashauriwa kuanza matibabu kwa njia ya asili. Kwanza aanze kwa kufunga bila kula kwa siku mbili huku akitumia maji ya kutosha kwa ajili ya kusafisha taka katika mwili. Baada ya hapo ale mlo kamili ambao takriban asilimia 70-80 ya vyakula viwe havikupikwa (in their natural uncooked states) kwa sababu upikaji wa vyakula hupunguza au huaribu viinilishe (nutrients) vilivyomo kwenye vyakula. Mlo uwe na vyakula vya mbegu (seeds, nuts and grains), mboga za majani na matunda. Katika milo hiyo tumia pia maziwa na asali. Mafuta unayotumia katika vyakula yawe yale ya mimea (vegetable oils).

Ili mwanamke awe na mwili wenye afya njema nashauri afuate ratiba hii ya milo. Asubuhi akiamka, anywe glasi moja ya maji vuguvugu yaliyotiwa limao. Kifungua kinywa (breakfast) ijumuishe matunda (fresh fruits) kama apples, chungwa, ndizi, zabibu, na balungi na maziwa glasi moja. Chakula cha mchana ale mboga za majani zilizochemshwa kiasi (zisiive kabisa) na ziungwe kwa mafuta ya mimea au siagi na chumvi kiasi, chapatti mbili au tatu na maziwa (a glass of buttermilk). Katika kipindi cha kati ya mlo wa mchana (lunch) na mlo wa jioni/usiku (dinner) anywe juisi ya matunda (fresh) au juisi ya mboga za majani. Chakula cha usiku, ale saladi nyingi inayotokana na mboga za majani (fresh vegetables) kama nyanya, karoti, viazi sukari (beetroots), na vitunguu na maharage au jamii ya maharage yalipikwa. Wakati wa kwenda kulala, ale apple au maziwa glasi moja.

Mwanamke aepuke kula vyakula vyenye mafuta mengi, viungo vikali, chai iliyokolea sana majani, kahawa, sukari nyeupe (white sugar) na unga mweupe uliokobolewa (white flour). Unywaji wa pombe na uvutaji sigara viepukwe.
Matibabu mengine ambayo husaidia kutibu tatizo la ugumba kwa mwanamke ni kutumuia mzizi wa mti uitwao ‘banyan’. Chukua mzizi huo na ukaushe sio kwa kuuweka juani bali kivulini mpaka ukauke. Baada ya hapo unausaga kuwa unga. Changanya unga huo na maziwa na tumia usiku wakati wa kwenda kulala kwa siku tatu. Usitumie pamoja na chakula au kinywaji chochote wakati wa usiku. Unaweza ku-google ili kuujua mti uitwao banyan. Namna ya kuchanganya: pima kwa uzito, unga wa banyani uwe na uzito mara tano ya uzito wa maziwa.


Tiba nyingine ni mwanamke kula bilinganya (eggplants) zilizopikwa. Ale pamoja na maziwa buttermilk kila siku kwa mwezi mmoja au miezi miwili hivi. Mlo huu huongeza mwilini homoni ya uzazi iitwayo progesterone na pia huongeza uwezo wa mwili kutumia vitamin E inayopatikana kwenye chakula anachokula. Bila kusahau mwanamke ahakikishe anakuwa na uwiano wa uzito na urefu wa mwili unaostahili.