Balungi (Grapefruit) ni tunda ambalo lina wingi wa asidi ya citric, potassium na calcium. Unapokula tunda hili usiku wakati wa kwenda kulala hukufanya upande usingizi mnono. Unywaji wa juisi ya tunda hili asubuhi kabla ya kula chakula chochote hutibu tatizo la kutopata haja kubwa (constipation). kadhalika ulaji wa tunda hili hupunguza homa itokanayo na mafua makali (colds and flu). Uchachu uliomo kwenye tunda hili husaidia tumbo kuachilia kwa wingi vimen'genya vinavyosaga chakula (digestive enzymes).
Vilevile ulaji wa balungi kabla ya kula chakula huongeza hamu ya kula na husaidia uyeyushaji wa chakula mwilini.
Baada ya kuangalia faida hizo za tunda la balungi sasa hebu tuliangalie tunda hili kama dawa ya tiba kwa magonjwa mbalimbali.
- Kutokupata Haja Kubwa (Constipation): Asubuhi kabla hujala chakula chochote kunywa juisi ya balungi kiasi cha nusu glasi ikiwa umeweka chumvi kidogo.
- Kukosa Usingizi (Sleeplessness): Wakati wa kulala usiku kunywa juisi ya balungi glasi moja ikiwa umewekwa sukari kijiko kidogo (teaspoon).
- Kukosa Hamu ya Chakula na Radha (Loss of Appetite and Taste): Kunywa juisi ya balungi nusu glasi ikiwa imewekwa kiasi kidogo cha chumvi (pinch of black salt).
- Kupunguza Rehamu (Cholestral levels) na Kiharusi (Strokes), Kukarabati Mishipa ya Damu ya Vein na Kusaidia Damu Kutembea Mwilini, na Kupunguza Unene: Kula nusu kipande cha tunda la balungi wakati wa kifungua kinywa (breakfast) na dakika 30-60 baada ya chakula cha mchana (lunch) kunywa juisi ya balungi iliyoongezwa maji kiasi cha glasi moja.
- Vidonda vya Koo (Sore throat), Harufu Mbaya ya Kinywa na Mafua (Flu): Kila baada ya saa moja fyonza robo kipande cha tunda la balungi ili kupata vitamins na asidi zilizomo kwenye tunda hilo na weka kipande hicho kwenye ulimi ili kupunguza wingi wa bakteria walioko kinywani na pia kupunguza harufu mbaya ya mdomoni.
No comments:
Post a Comment