- Je umetumia njia mbalimbali kuondoa tatizo la unene au uzito mkubwa lakini umeshindwa?
- Usikate tamaa, fahamu ni kwa nini umeendelea kuwa na fetma.
Takribani zidi ya asilimia 75 ya watu wanaoishi
Amerika wanakabiliwa na tatizo la kuwa na uzito uliopitiliza (Overweight). Ni
ukweli usiopingika kwamba waamerika ni watu wanene zaidi kuliko watu wa mataifa
mengine yote Duniani. Tatizo la unene au uzito uliopitiliza limekuwa ni tatizo
linalowakabili watu wengi Duniani ikiwemo nchi zinazoendelea kama Tanzania.
Tatizo hilo linaendelea kuongezeka kwa kasi kubwa kadri miaka inavyoendelea.
Nimewahi kumsikia daktari mmoja wa hospitali ya Taifa ya Rufaa ya Muhimbili nchini
Tanzania akiongelea kuhusu tatizo la uzito mkubwa kwenye kituo cha luninga
ambapo alisema kwamba tatizo hilo hivi sasa linakuwa kwa kasi kubwa katika
jamii yetu kuliko hata ugonjwa wa ukimwi!
Tatizo la kuzidi uzito au unene huweza kumpata mtu
yeyote wa jinsia yoyote na katika kipindi chochote cha maisha yake. Kimsingi
tatizo hili hutokana na mwili kuhifadhi mafuta yanayotokana na ulaji wa vyakula
vyenye kalori nyingi kuzidi mahitaji ya mwili (over eating or intake of excess
calories). Vile vile ulaji wa vyakula visivyostahili (wrong foods) hupelekea
mwili kupatwa na shida ya kuwa na asidi ambayo hupelekea damu kuwa katika
hatari ya kuwa na asidi (Acidification of the blood’s acid-alkaline pH). Ili
kuepusha damu kuwa na asidi mwili hubadiri asidi (acetic acid) kuwa seli za
mafuta na kuhifadhiwa mwilini hivyo mtu kupatwa na tatizo la uzito mkubwa. Pia
tatizo hili huwapata wanawake baada ya kuwa na ujauzito. Mjamzito huongezeka
takriban kilo 12 wakati akiwa katika hali ya ujauzito. Uzito huo unaozidi
huondoka mara baada ya kujifungua mtoto. Hata hivyo wanawake wengine huendelea
kubaki na kiasi fulani cha uzito huo hivyo kupelekea kuwa na uzito mkubwa (Overweight)
na uzito huo huendelea kuongezeka kadri mwanamke anavyoendela kuzaa watoto
wengine.
Tatizo la kuzidi uzito au unene kitalaam Fetma
(obesity) ni tatizo kubwa sana la kiafya kwani mafuta yaliyozidi na kuhifadhiwa
mwilini huleta shida kwenye moyo, figo, ini na kwenye pingili za mwili
(joints). Mtu mwenye tatizo la fetma hukabiliwa na magonjwa kama vile moyo
kushindwa kufanya kazi (heart failure), shinikizo la damu lililo juu (high
blood pressure), ‘coronary thrombosis’, kisukari (diabetes), maumivu ya viungo
(Arthritis), ‘gout’ na magonjwa ya figo na moyo. Kadhalika matatizo ya uzazi,
wanawake kupatwa na tatizo la kushindwa kushika ujauzito na wengine kupotewa na
hisia za mapenzi, na wanaume kupatwa na tatizo la nguvu za kiume.
Watu wengi wenye tatizo la uzito au unene
uliopitiliza wamejitahidi kuliondoa tatizo hilo kwa kutumia njia mbalimbali
lakini jitihada zao zimekuwa zikigonga mwamba. Wamekuwa wakinunua na kusoma
vitabu kadhaa kuhusu tatizo hili, wamekuwa wakifanya ‘diet’, wamekuwa wakifanya
mazoezi ya viungo, wamekuwa wakijinyima kula au kuepuka ulaji wa vyakula vya
mafuta, wamekuwa wakitumia madawa ya kupunguza unene, nk. Pamoja na juhudi zote
hizo watu wengi hawajapata mafanikio yoyote na wengine wamekata tama na kuamua
kujiachilia na kuridhika na hali waliyonayo ya fetma (obesity). Napenda
kukutia moyo kwamba usikate tamaa kwani unaweza kuondokana na tatizo hilo tena
kwa asilimia 100 kwa njia salama. Nitakwenda kueleza namna ya kupunguza uzito
au unene tena kwa njia salama yenye gharama ndogo sana. Najua watu wengine
wamekuwa wakitumia pesa nyingi sana kuondokana na tatizo hili.
Awali ya yote tuangalie sababu kadhaa ambazo watu
wengi pamoja na kujitahidi kuondokana na tatizo la uzito au unene bado wamekuwa
wakiendelea kuwa na tatizo hio. Sababu hizo ni hizi zifuatazo:-
- Watu wanene hukumbwa na tatizo la kuwa na mfumo dhaifu wa uyeyushaji chakula mwilini (Low metabolism). Hii haina maana kwamba walizaliwa wakiwa na hali hiyo bali hali hiyo imejitokeza baada ya kuwa na tatizo la unene. Kufuatia kuwa na mfumo dhaifu wa uyeyushaji chakula, mtu mnene akila chakula hata kama ni kiasi kidogo chakula hicho hakiunguzwi mwilini kwa urahisi na badala yake kinageuzwa kuwa seli za mafuta na kuhifadhiwa mwilini. Hii ndio maana kujinyima chakula kwa watu wanene imekuwa haiwasaidii kuondokana na tatizo badala yake kujinyima chakula huweza kusababisha vidonda vya tumbo na matatizo mengine ya kiafya.
Katika mwili wa binadamu kuna tezi na viungo
vinavyosimamia usagaji na uyeyushaji chakula. Hizi ni pamoja na tezi ya thyroid
na viungo vya mwili kama kongosho (pancreas), ini, tumbo, utumbo mwembamba na
utumbo mpana. Ndio kusema kwamba kama mfumo wako wa usagaji na uyeyushaji
chakula ni dhaifu hii ina maana kwamba tezi na viungo hivyo havifanyi kazi zake
ipasavyo. Sasa jiulize ‘Nini kimesababisha uwe na hali hiyo?’ Swali hilo linajibiwa
kwa kutoa sababu zifuatazo:-
- Watu wanene wengi wao wana tezi ya thyroid isiyofanya kazi kwa ufanisi (under active Thyroid or hypoactive Thyroid). Mojawapo ya chanzo cha tatizo hilo ni madini ya fluoride yaliyomo katika maji unayokunywa. Katika nchi zingine madini hayo yalipigwa marufuku kuwekwa kwenye maji ya kunywa.
- Asilimia kubwa ya watu wanene, kongosho zao hazifanyi kazi ipasavyo. Kongosho huzalisha/hutoa nyongo (insulin). Watu wanene, kongosho zao hutoa nyongo nyingi zaidi kuliko watu wembamba. Sababu zipi hupelekea mwili wako kutoa nyongo kwa wingi? Hakuna mtu mwenye majibu sahihi. Hata hivyo sababu mojawapo ni ‘food additives’ zinazowekwa katika vyakula. Ulaji wa kiasi kikubwa cha sukari iliyosafishwa viwandani (refined sugar) pia husababisha tatizo hilo la kongosho kutokufanya kazi kwa ufanisi. Vyakula vingi katika nchi kama Marekani vina ‘refined sugar’ kuliko vyakula vya nchi yoyote duniani. Chunga sana vyakula vilivyosindikwa unavyonunua katika maduka ya vyakula au supermarkets hususan vile vinavyotoka nchi za nje.
- Asilimia kubwa ya watu wanene wana maini yaliyoziba au kujawa na sumu hivyo kushindwa kufanya kazi sawasawa (sluggish). Kazi ya ini ni kuondoa sumu mwilini (detoxifying organ). Ini linaposheheni sumu, mfumo wa kuyeyusha chakula mwilini huwa dhaifu. Nini husababisha ini kujawa na sumu? Ni utumiaji wa muda mrefu wa madawa ya tiba na vipodozi vyenye kemikali kali. Utumiaji wa madawa ya kupunguza rehemu (Cholosterol reducing drugs), utumiaji wa maji yenye chlorine na fluorine, ‘food additives’, ‘refined sugar’ na unga unaotokana na nafaka zilizokobolewa (white flour). Vitu vingine ni pamoja na vikoleza utamu (artificial sweeteners), ‘Monosodium glutamate (MSG)’ na kemikali za kuhifadhia vyakula au vinywaji (preservatives).
- Viungo muhimu vya mwili vinavyohusika na uyeyushaji chakula katika miili ya watu wanene kama vile tumbo, utumbo mwembamba na utumbo mpana (colon) havifanyi kazi zake ipasavyo. Utumbo mwembamba na utumbo mpana wa mtu mnene havifanyi kazi zao sawasawa kutokana na kuoteana/kuongezeka kwa wingi (overgrowing) kwa fangasi waitwao ‘Candida’. Kwa nini waoteane kwa wingi? Kwa sababu ya matumizi ya dawa aina ya ‘antibiotics’. Kama uliwahi kutumia dawa hizo fahamu kwamba dawa hizo ziliua aina ya bacteria rafiki wanaoishi mwilini waitwao ‘friendly flora’ ambao wanaishi katika utumbo. Hali hiyo hupelekea kuongezeka au kuoteana kwa wingi candida katika utumbo mwembamba na utumbo mpana (colon), fangasi hao kujipenyeza kwenye kuta za seli za mwili, na hatimaye kupunguza uwezo wa mwili wa kusaga, kuyeyusha, kufyonza chakula na kutoa uchafu mwilini. Kadhalika, kitu chochote kile ulichoingiza mwilini mwako kupitia chakula ulichokula au namna nyingine yoyote ndicho kilichopelekea tatizo la udhaifu wa usagaji chakula katika mwili wako. Sumu hizo ni pamoja na madawa uliyomeza, mabaki ya kemikali zilizotumika katika kilimo cha chakula ulichokula, ‘artificial food additives’, kemikali katika maji ya kunywa hususan chlorine na fluoride. Sababu nyingine inayopelekea udhaifu wa mfumo wa usagaji chakula ni ukosefu wa mazoezi. Miili yetu imeumbwa kwa namna kwamba inahitaji kufanya mazoezi kama vile kutembea.
- Asilimia kubwa ya watu wanene au wenye uzito mkubwa hupenda kula chakula hata kama hawasikii njaa. Hali hii husababishwa na mambo mawili ambayo ni kuwa na hamu isiyozuilika ya kupenda kula na kupenda kula kama namna ya kupata faraja kutokana na kuwa na msongo wa mawazo (stress or emotional eating). Hamu ya kupenda kula husababishwa na ongezeko la candida mwilini.
- Asilimia kubwa ya watu wanene wana hamu kubwa ya kula (large appetite). Watu hao mara nyingi huwa na njaa hali ambayo hutokana tatizo la mwili kushindwa kufyonza chakula baada kuwa kimesagwa mwilini na badala yake chakula hicho kugeuzwa kuwa seli za mafuta ambazo huifadhiwa mwilini. Hali hii hufanya mwili kuwa na uhitaji wa chakula kwa kuwa unakosa ‘nutrients’. Pia tatizo hilo la kupenda kula huchochewa na wingi wa candida waliopo mwilini na baadhi ya ‘food additives’ zilizoongezwa kwenye vyakula ili kuongeza hamu ya kula. Vilevile ulaji wa vyakula visivyofaa (wrong foods) hususan wakati wa mchana (day time) hupelekea tatizo la mwili kuwa na taka za asidi (acid waste) kwa kiwango kikubwa nyakati za usiku. Hali hii husababisha tatizo la hamu kubwa ya kula. Hiyo hali hupelekea mtu kushindwa kulala au kuamka usiku kutoka kitandani na kula chakula chochote atakachokiona hata visivyo na manufaa kwa mwili (junk foods). Hali hii kitalaamu huitwa ‘Night Binging’. Hivyo namna nzuri ya kuondokana na tatizo la ‘Night Binging’ ni kuondoa tatizo la taka za asidi.
- Asilimia kubwa ya watu wanene wana tatizo la kutokuwiana kwa homoni (hormonal imbalance). Hii hutokana na mwili kuzalisha kwa wingi aina moja ya homoni kuliko aina nyingine ya homoni. Hali hiyo hutokana na ongezeko la sumu mwilini na pia mwili kukosa mazoezi.
- Asilimia kubwa ya watu wanene hula kiasi kikubwa cha chakula kuliko watu wembamba. Hii husababishwa na mwili kushindwa kufyonza chakula ilichosaga, hamu ya kula na kuwa na ‘stress’.
- Watu wanene hupenda kutumia vyakula au vinywaji vya ‘diet’ kwa lengo la kupunguza unene bila kujua kwamba vyakula au vinywaji hivyo huwafanya kuwa wanene. Bidhaa zenye labels za ‘Diet’, ‘Low fat’, ‘Sugar free’, ‘Low calorie’, ‘Lite’, ‘Light’, ‘Low carbohydrates’, ‘Lean’, nk zimewekewa ‘artificial sweeteners’ na ‘chemical additives’ ambavyo huwafanya watu wawe wanene. Hizo ‘additives’ humfanya mtumiaji awe na hamu ya kula au kunywa zaidi bidhaa hizo kiasi cha mtumiaji kuwa ‘addicted’.
- Asilimia kubwa ya watu wanene wana sumu nyingi mwilini. Nyingi ya sumu hizo hukaa katika utumbo mpana (colon) na katika seli za mafuta (fat cells). Mwili ukiwa na sumu nyingi hutafuta namna ya kuziondoa au kuziyeyusha (dilute). Hii hufanya mwili kutunza au kuhifadhi maji (water retentation) kama njia ya kujaribu kuyeyusha sumu hizo. Hii ndio maana watu wanaotumia madawa kwa muda mrefu ambayo kimsingi yana kemikali za sumu ndani yake huwa wanene baada ya kipindi fulani cha matumizi ya dawa hizo. Bila shaka umewahi kusikia watu wanene kuwa na tatizo la maji mengi mwilini au pengine wewe ni mhanga wa tatizo hilo.
- Watu wanene huenda kulala muda mfupi tu baada ya kula chakula cha jioni au usiku. Unapolala uwezo wa mwili kuyeyusha chakula hupungua. Hivyo ukila chakula na kwenda kulala muda mfupi baada ya kula mwili haupati muda wa kuyeyusha chakula na matokeo yake chakula hicho hugeuzwa kuwa mafuta na kuhifadhiwa mwilini.
- Watu wanakuwa wanene pia kutokana na kuathiriwa na homoni za ukuzaji (growth hormone) zinazowekwa kwenye vyakula vya wanyama wanaofugwa kwa ajili ya uzalishaji wa nyama na maziwa. Wanyama na kuku wanaofugwa huwekewa homoni hizo kwenye vyakula wanavyopewa ili wakue kwa haraka kwa lengo la kuongeza uzalishaji wenye tija. Tunaingiza homoni hizo katika miili yetu tunapotumia bidhaa hizo na hivyo kupelekea miili yetu kuongezeka uzito au kuwa wanene. Hii ndio sababu ya watoto wanaozaliwa siku hizi kukua na kubalehe haraka tofauti na ilivyokuwa miaka ya nyuma.
- Ulaji wa vyakula kwa mtindo wa kujinyima baadhi ya vyakula au kula kidogo baadhi ya vyakula yaani kufanya ‘diet’ hupelekea baadhi ya watu kukumbwa tena na tena na tatizo la unene au uzito mkubwa. Mtu anapofanikiwa kutatua tatizo hilo kwa kufanya diet ‘genes’ za mwili hutafasri hali hiyo kuwa mwili umepatwa na shida ya ukosefu wa chakula (starvation). Hivyo ‘genes’ hizo hutoa taarifa kwa tumbo kuachilia homoni iitwayo ‘ghrelin’ ambazo husababisha hali ya kujisikia njaa kuongezeka. Hali hiyo hupelekea mtu huyo kula chakula kingi kuliko alivyokuwa akila awali na hivyo uzito kuongezeka tena. Hii inaeleza sababu ya kwa nini watu wengi wanaofanya diet huishia kushindwa kuendelea na diet na kurudiwa na tatizo la kupatwa na unene. Ufanyaji diet mzuri kitalaamu usiwe ni ule wa kupunguza ulaji wa vyakula vyenye kalori nyingi bali kula vyakula ambavyo ni rahisi kuyeyushwa na ambavyo vinapunguza tatizo la hamu ya kula na uchu wa vyakula (food cravings).Hali ya kupunguza uzito na baada ya siku au miezi kadhaa uzito au unene ukarudi huweza kupelekea mwili kupatwa na udhoofu wa kinga ya mwili.
- Watu wanene hujiona kuwa ni wanene. Kuna msemo kuwa ‘jinsi unavyojiona ulivyo ndivyo ulivyo’. Watu wanene hujiona ni wanene hivyo hutengeneza matokeo ya vile wanavyojiona walivyo.
No comments:
Post a Comment