Baada ya kuangalia sababu ambazo huwafanya watu kuwa wanene au wenye uzito unaozidi katika mada ‘Fetma (Obesity): Kwa Nini Watu Wanakuwa Wanene Kupita Kiasi?’ sasa tuangalie namna ambavyo watu wanene wanavyoweza kupunguza uzito na kuendelea kuwa na uzito unaoendana na urefu wa miili yao (Body Mass Index – BMI). Kabla sijaeleza mambo muhimu ya kufanya ili kuondokana kabisa (100%) na Tatizo la Fetma au Unene uliozidi napenda nitoe angalizo kwa wale wanaovutiwa na madawa au programu zinazotangazwa kibiashara kwamba zitawawezesha kupunguza uzito mkubwa katika kipindi kifupi. Hiyo ni HATARI kwa afya yako. Watalaamu wa Afya wanashauri kupungua uzito kilo 1 - 1.5 tu kwa wiki na sio zaidi ya hapo. Haya sasa tuangalie mambo muhimu ya kufanya ili kutokomeza kabisa tatizo la Fetma (Obesity) na Uzito mkubwa (Overweight):-
- Mara tu unapoamka asubuhi kabla ya kula chakula chochote kunywa glasi moja ya maji vuguvugu. Unaweza kukamua ndimu moja na kumimina juisi ya ndimu kwenye hayo maji. Unywaji wa maji asubuhi kabla ya kula chakula chochote hufanya mwili kujiweka tayari kwa ajili ya kuanza ‘process’ ya uyeyushaji chakula.
- Kula chakula cha kutosha asubuhi (big breakfast). Asilimia 80 ya watu wanene hula kiasi kidogo cha chakula. Hii ni kinyume chake kwa watu wembamba ambao asilimia 80 hula kiasi kikubwa cha chakula wakati wa kifungua kinywa. Hakikisha kifungua kinywa kiwe cha vyakula vya asili (organic foods) kama vile matunda: tufaha (apples), pears, nanasi, mabalungi (grapefruits), plums, peaches, prune, mkate, siagi mbichi (not pasteurized and not homogenized), maziwa, plain yogurt (no sugar or fruits in it), nyama , kuku, viazi (kiasi), kahawa, asali, nk.
- Kunywa maji glasi nane (8) kila siku. Maji huitajika mwilini kwa ajili ya kusafisha au kutoa uchafu mwilini.
- Fanya mazoezi ya kutembea kwa mguu angalau kwa muda wa saa moja kila siku.
- Usile chakula baada ya saa 12 jioni. Hii ina maana kwamba muda wako wa mwisho wa kula chakula cha jioni au usiku iwe saa 12 au kabla ya hapo. Usilale mpaka upitishe angalau masaa mawili tangu ule chakula cha usiku. Hii itasaidia kuupa mwili muda wa kuyeyusha chakula.
- Shughulikia tatizo la ongezeko au kuoteana kwa candida mwilini mwako. Kumbuka watu wanene hukumbwa na tatizo la kuoteana kwa wingi kwa fangasi aina ya candida. Kuoteana kwa candida hupelekea maambukizi mdomoni, kooni, kwenye njia ya mfumo wa chakula (digestive tract) na kwenye njia ya uke (kwa wanawake). Hivyo kupunguza uzito bila kwanza kuwashughulikia candida ni ndoto maana hata kama ukifanikiwa kupungua unene upo uwezekano mkubwa wa kurudiwa na unene.
Juisi ya
kutibu tatizo la candida (Candidiasis): Blendi kwa pamoja tango (gramu 50),
‘natural yourgut’ (90ml), maziwa (90ml) na majani 8-12 ya minti (mint leaves).
Weka chumvi kidogo kwa ajili ya radha na nyunyiza juisi ya limau, kisha kunywa. Yourgut husaidia kurejesha bacteria wa asili
hivyo kutibu maambukizi ya candida. Vitamin na madini yaliyomo kwenye matango
huimarisha kinga ya asili ya mwili iliyokuwa imeharibiwa. Majani ya minti yana
mafuta (essential oils) yanayodhibiti fangasi au bacteria (antifungal
properties). Juisi hii ni nzuri kwa wanawake ambao wamekuwa wakipatwa na tatizo
la fangasi aina ya Candida.
- Safisha utumbo mpana (colon). Kama huendi choo mara mbili au tatu kwa siku basi una tatizo la kukosa choo (constipation). Hivyo unahitaji kusafisha utumbo mpana kwa kuondoa taka (kinyesi) au sumu zilizojaa na kugandana humo.
Tatizo
la kukosa choo husababishwa na kutokula matunda na mboga za majani zakutosha au
kutokula vyakula ambavyo havijakobolewa au kuondolewa uasili wake ambavyo kimsingi
vina nyuzi (fiber) zinazosaidia kusafisha utumbo mpana (Colon) na kwenda choo
ipasavyo. Pia kutokufanya mazoezi ya mwili na kunywa maji ya kutosha (angalau
glasi 8 kila siku).
Asilimia
takriban 70 ya magonjwa yote hutokana na tatizo la kutokusafishwa vya kutosha
kwa utumbo mpana (Colon). Usipopata choo wakati unakula kila siku basi fahamu
kwamba ndani ya colon kumegandamana uchafu na sumu za kutosha. Pia inashauriwa
mara tu ukisikia haja kubwa wahi haraka ukaitoe chooni. Kubana choo kwa muda
mrefu pia ina madhara kiafya kwani baadhi ya taka sumu ambazo zingepaswa
kutolewa nje kwa muda huo hufyonzwa tena na kuta za utumbo mpana na kurudi
mwilini ambapo nyingine huifadhiwa kama seli za mafuta.
Ili
kushughulikia tatizo la kutokupata choo ipasavyo ni vema kuanza na programu ya
kusafisha utumbo mpana (Colon) iitwayo ‘Salt
Water Flush Program’. Hii uifanywe siku ukiwa huna kazi na uko nyumbani. Chukua maji ya vuguvugu lita moja, weka weka
chumvi ya baharini (sea salt) ambayo inauzwa madukani au supermarkets. Sio
chumvi ya kuchimbwa ardhini bali iliyovunwa kutokana na maji ya bahari. Kunywa
hayo maji ndani ya kipindi cha dakika 45 tu.
Kisha lalia ubavu wa kushoto ili kuruhusu maji
yatoke tumboni kuingia kwenye utumbo mwembamba. Mara tu ukijisikia kwenda choo
nenda mara moja. Endelea kwenda choo mpaka hali ya kusikia choo itakapokoma.
Itakuchukua takribani masaa manne hivi.
Baada
ya zoezi hilo utafanya hatua ya pili ya Kusafisha utumbo kwa Juisi. Tengeneza
juisi yenye mchanganyiko wa
matunda matatu, manne au zaidi kati ya matunda haya: Apples, Oranges, Avocados,
Raspberries, Papai, Strawberries, Blackberries, Pears, Figs na Prunes. Kunywa
kila siku mpaka hali ya kutopata choo itakapoacha. Baada ya hapo sasa uwe na
mikakati mizuri ya ulaji chakula (balanced diet).
Juice ingine ukipenda kwa ajili ya tatizo la kukosa choo: Blend vipande vya nanasi (kikombe 1), nusu
chungwa na papai moja na mbegu zake (ila tu ulimenye). Blend kwenye blender na
kunywa.
Juice ingine: Blendi
mchanganyiko wa embe moja lilomenywa na kukatwakatwa vipande, matunda mawili ya
peaches yaliyomenywa na kukatwa katwa, zabibu nyeupe (gramu 100) na mdarasini
nusu kijiko kidogo.
Juice ingine: Blendi
karoti 3 kubwa na viazisukari (beetroots) ukubwa wa kati (medium-sized) 2.
Juice ingine: ndizi mbili
zilizoiva na kumenywa na kukatwakatwa vipande, unga wa tini (almonds) gramu 50,
juisi ya chungwa (fresh orange juice), ‘natural yourgut’ 150ml, asali kijiko
kimoja cha chakula na unga kidogo wa kungumanga (nutmeg).
- Tumia mafuta ya kula ya nazi (coconut cooking oil) ambayo ni ya asili na hayajawa ‘refined’ yaani ‘100% organic, virgin, unrefined coconut oil’.
- Fanya ‘infrared saunas’. Sauna huongeza kasi ya mfumo wa uyeyushaji chakula, hupunguza sumu, huongeza kasi ya kupungua uzito/unene na kuunguza mafuta mwilini. Fanya sauna kila siku ukiweza.
- Kula angalau barungi moja lililozalishwa kiasili (organic grapefruit) kila siku. Barungi lina vimeng’enya vinavyosaidia kuunguza mafuta mwilini (reduce cholestrol level). Pia husaidia kutibu tatizo la kiharusi (strokes) kwa wale wenye tatizo hilo au wako katika hatari ya kukumbwa na tatizo hilo.
- Usitumie vyakula vilivyosindikwa na kutiwa ‘aspartame’ au vikoleza utamu visivyo vya asili (artificial sweeters) kwani huwafanya watu wawe wanene au waongezeke uzito. Jina jingine ambalo hutumika kwa ‘aspartame’ ni ‘NutraSweet®’. ‘Artificial sweeteners’ ni pamoja na ‘Saccharin’ na ‘Splenda®’. Hivyo kuwa makini unaponunua vyakula vilivyosindikwa na kufungwa kwenye vifungashio. Bahati mbaya watu wengi hatuna utamaduni wa kusoma labels za vyakula au bidhaa zingine ili kujua nini kilichomo ndani (ingredients).
- Usitumie vyakula vyenye ‘MSG (Monosodium Glutamate)’. MSG ni sumu ‘axcitotoxin) ambayo matumizi yake huwafanya watu waongezeke uzito au wawe wanene, pia husababisha matatizo ya kiafya (medical problems) na kuwafanya watu wawe na mfadhaiko (depressed). MSG mara nyingi huwa haiandikwi katika labels za vyakula zinazoeleza viambata (ingredients) vilivyomo ndani ya vyakula au kinywaji ulichonunua. MSG huandikwa kwenye labels kama ‘artificial flavoring’, ‘hydrolyzed vegetable protein’, etc. MSG pia hutiwa kwenye baadhi ya vyakula vinavyouzwa kwenye ‘Fast foos’ kama vile pizza au burger.
- Tumia vimeng’enya (enzymes) vinavyosaidia uyeyushaji wa chakula mwilini. Kama una tatizo la unene au uzito mkubwa upo uwezekano mkubwa kwamba mwili wako hauzalishi vimeng’enya vya kutosha kusaga na kuyeyusha chakula mwilini. Hali hiyo hukufanya uongezeke uzito, ‘feel bloated’, kuwa na gesi tumboni, shida ya kusaga na kuyeyusha chakula tumboni (indigestion) na kutokupata choo (constipation). Nunua vimeng’enya hivyo katka maduka maalum ya vyakula (health food store) au kwenye maduka ya madawa.
- Usipende kula vyakula ‘fast food’. Sina maana ya kuharibu biashara za wamiliki wa migahawa ya ‘fast food’, hapana bali kutoa ushauri wa kiafya tu. Vyakula vya ‘fast food’ huzalishwa au hutengenezwa kwa kuzingatia zaidi faida ya kibiashara kuliko afya ya walaji. Vyakula hivyo hutiwa kemikali huko katika nchi vinakotoka ili viweze kuhifadhiwa kwa muda mrefu bila kuharibika. Pia huwekwa ‘kemikali’ ili kuvifanya viwe vitamu kwa lengo la kuchochea hamu ya kula (appetite) ya mlaji hali ambayo humfanya apendelee kula vyakula hivyo na matokeo yake ni kuongezeka uzito au kuwa mnene.
- Kula tunda moja la ‘apple’ kila siku. Tunda hilo lina nyuzi (fiber) nyingi sana na unapolila husaidia kurekebisha sukari mwilini mwako kuwa katika kiwango cha kawaida (normal). Pia tunda hilo husaidia kupunguza hamu ya kula. Kumbuka watu wanene hukumbwa na tatizo la kupenda kula kutokana na hali fulani fulani zinazojitengeneza miilini mwao kama nilivyokwisha kueleza awali. Pia kabla ya kula chakula ili kukata njaa kali (hunger pangs) anza kwa kula vyakula vyenye radha ya uchachu (sour-tasting foods) kama vile yogurt, siki (vinegar) na juisi ya limao au ndimu. Kisha baada ya hapo ndipo ule mlo wako.
Epuka kula vyakula vilivyotiwa viungo vikali
(spices or herbs) kwani huchochea hamu ya kula chakula kingi.
- Kuwa mwangalifu na ulaji wa bidhaa za maziwa. Usitumie bidhaa za maziwa ambazo zimeondolewa katika hali yake ya uasili (not organic dairy products) kwa kuwa zimewekewa homoni za ukuzaji (growth hormone). Nunua bidhaa hizo baada ya kujiridhisha kuwa zimeandikwa ‘organic and raw’, au ‘not homogenized but pasteurized’, au ‘both homogenized and pasteurized’.
No comments:
Post a Comment