Dalili za UTI: Njia ya mkojo kuuma wakati wa kukojoa. Maumivu hayo hujitokeza wakati wa kuanza kukojoa au katikati ya kukojoa. Kujisikia mkojo kutaka kutoka bila breki na kukojoa mara kwa mara. Mara nyingine UTI hufanya kujisikia homa, baridi na kutapika au maumivu ya mgongo au chini ya tumbo. Haipasi kupuuza dalili za maumivu ya mgongo au chini ya tumbo, ni dalili kwamba maambukizi yanaanza kushambulia figo. Hali ikifikia hivyo hiyo inamaanisha UTI imefikia hatua mbaya (a serious complication of a UTI).
Matibabu: Kuzuia au kutibu UTI, kunywa juisi ya Cranberry mili-lita 350 (sawa na ujazo wa chupa ya soda) kila siku. Au kunywa juisi ya blueberries mili-lita 125-250 kila siku. Juisi hizi hupatikana katika Health food store au Supermarkets. Au nunua Cranberry capsules katika maduka ya madawa hususan yake yanayouza herbs. Meza capsules mbili kwa siku. Kwa nini juisi hizi? Juisi hizi husababisha hali ya uterezi kwenye kuta za njia ya mkojo. Hiyo hufanya bacteria wasiweze kujishikiza kwenye kuta hizo huvyo kuwa rahisi kutolewa nje kwa njia ya mkojo (flushed out). Kadhalika ukipatwa na ugonjwa wa UTI tengeneza juisi ya nanasi, kunywa kila siku hadi upone. Juisi hiyo hutia hali ya asidi katika njia ya mkojo. Bakteria wa E.Coli hawasitahimili mazingira yenye asidi.
Kunywa maji ya ya kutosha angalau lita mbili kwa siku kila siku. Kadhalika wakati unatibu UTI, usitumie kahawa, viungo vikali (spices) na vileo. Tumia kitunguu swaumu katika chakula. Au nunua unga wa kitunguu swaumu, weka kiasi kwenye maji ya moto kunywa kama chai. Kitunguu swaumu hujenga kinga ya mwili inayopambana na magonjwa ikiwemo UTI.
Usafi: 1. Baada ya kujisaidia haja kubwa au haja ndogo tawaza taratibu kuanzia mbele kwenda nyuma na sio kuanzia nyuma kuja mbele. Hii huepusha kusambaza bacteria kutoka kwenye njia ya haja kubwa na kuwapeleka kwenye njia ya mkojo. 2. Usibane mkojo unapojisikia kukojoa. Kujoa husaidia ku-flush bacteria kabla hawajaingia ndani kabisa katika njia ya mkojo (urinary tract). 3. Osha viungo vyako vya siri (genital area). 4. Vaa chupi za pamba. Chupi au nguo zingine za ndani zilizotengenezwa kwa aina zingine za ‘materials’ hufanya mazingira ya joto ambalo ni mazingira mazuri ya bacteria kuishi.
Epuka: Wakati ukiwa kwenye matibabu ya UTI, epuka ulaji wa vyakula vyenye acid kama vile, juisi ya machungwa, juisi ya nyanya, na ulaji wa matunda kwa kiasi kikubwa mpaka utakapokuwa umepona.Epuka vinywaji vyenye caffeine kama vile kahawa, chai, chocolate, vinywaji baridi (soda). Epuka kufanya ngono mpaka upone. Kwa wanawake, epukeni kutumia sabuni zenye kemikali zitumikazo kusafisha ukeni (Vaginal soaps).
No comments:
Post a Comment