Monday, 3 August 2015

Mambo Muhimu Ya Kufanya Kuondokana na Tatizo la Fetma (Obesity)...Part 2


Image result for obesity photos before and after

Hii ni mwendelezo wa mada ya 'Mambo Muhimu Ya Kufanya Kuondokana na Tatizo la Fetma (Obesity) Part One'.

1.   Safisha ini lako. Kama wewe ni mnene ni dhahili kwamba ini lako limejaa sumu ambazo hupaswa zitolewe ili kufanya ini lifanye kazi yake ipasavyo. Vile vile taka asidi (acid waste) zikikaa kwenye ini hubadirishwa kuwa mafuta na kuhifadhiwa kwenye ini. Ndio maana watu wengine wamefanyiwa vipimo na kuambiwa wana mafuta mengi kwenye ini. Kusafisha ini tumia Detox Programu iitwayo ‘blackstrap lemon drink’. Kuandaa, changanya sukari guru kimiminika (blackstrap molasses) vijiko vikubwa viwili na juisi ya limao moja kwenye glasi ya maji moto. Kunywa kinywaji hiki tu bila kinywaji kingine chochote kwa muda wa siku tatu. Rudia tiba hii kila baada ya miezi michache.

2.   Kula kiasi kikubwa cha saladi wakati wa chakula cha mchana na wakati wa chakula cha jioni. Wakati wa mlo anza kwanza kula saladi. Saladi inyunyizie limau (fresh lemon) au siki (organic vinegar) na uitie mafuta ya kula ya mzeituni (organic olive oil). Iwekee chumvi ya baharini (sea salt), pilipili iliyosagwa (fresh ground pepper) au iliki kwa ajili ya kutia ladha.
3.   Tumia ‘organic apple cider vinegar’. Hii inaondoa seli za mafuta mwilini. Kunywa vijiko viwili vya hiyo siki kabla ya chakula na utaona matokeo yake.
4.   Jenga tabia ya kufanya mazoezi kwani husaidia kuunguza mafuta mwilini. Pia fanya mazoezi ya kuruka juu (Rebound).  Tumia ‘Rebounder’ kama unayo nyumbani kwako au nenda mahali ilipo. Mara nyingi rebounder huonekana kama ni kwa ajili ya michezo ya watoto lakini sivyo kwani ina faida kubwa sana kiafya. Kujirusha juu chini taratibu kwenye rebounder kwa muda wa dakika kumi kila siku hufanya mfumo wa ‘lympantic system’ kusisimka na hivyo kuongeza usagaji na uyeyushaji chakula mwilini.
5.   Funga kula chakula na badala yake kunywa juisi tu kwa siku kadhaa kulingana na hali ya kiafya ya mwili wako. Hii husaidia kuondoa sumu na seli za mafuta mwilini.
6.   Epuka kula chakula kama huna njaa. Watu wanene hukumbwa na tatizo la kuwa na hamu ya kula. Ulaji wa apples husaidia kutibu tatizo hili.Pia unaweza kutengeneza juisi matunda matatu ya apple (Granny Smith apples) na weka unga wa mdarasini kijiko kimoja cha mdalasini (cinnamon). Juisi hii licha ya kukata hamu ya kula wakati huna njaa pia husaidia kupunguza uzito wa mwili.
7.   Kula vyakula vya nyama yaani nyama, kuku na samaki vilivyozalishwa kiasili yaani visivyo na homoni za ukuzaji (growth hormones), antibiotics au insecticides. Ulaji wa nyama inayotokana na wanyama waliokuzwa kwa kula nyasi (grass-fed animals) huweza kukufanya upunguze uzito wa mwili wako kwa asilimia 20!
8.   Kula vyakula vyenye madini ya calcium na zinc kwani vinasaidia kupunguza uzito.  Utafiti uliofanywa na Dr. Robert P. Heaney, Professor of Medicine katika Chuo Kikuu cha Creighton huko Omaha, Nebraska alifanya utafiti na kugundua kwamba milo mitatu kwa siku iliyosheheni madini ya calcium hupelekea kupunguza uzito kwa (15 pounds) kwa mwaka. Milo hiyo isijumuishe maziwa kwa kuwa sio nzuri katika kupunguza uzito.
9.   Dhibiti matumizi ya sukari nyeupe (white sugar) na unga mweupe (white flour). Unga mweupe ukichanganywa na maji hufanya pasta na hukufanya uwe mnene. Tumia unga ambao haujakobolewa (whole grain flours that have not been processed or stripped of the fibers). Badala ya sukari nyeupe tumia asali. Sukari nyeupe iwe ni chaguo la mwisho kabisa (last choice option) kama utakosa asali au aina nyingine ya sukari.
10.  Epuka matumizi ya caffeine. Mfumo wa uyeyushaji chakula huanza na huzidi kushindwa kuyeyusha caffeine kadri mtu anavyopita umri kufuatia unywaji wa kahawa au chai zaidi ya vikombe viwili kwa siku. Unywaji wa kahawa, chain a soda zenye caffeine yaani ‘Colas’ hufanya chakula katika njia ya chakula (digestive tract) kuwa katika hali ya asidi hali inayopelekea kusikia njaa. Kadri umri wa mtu unavyoenda ndivyo anavyozidi kupenda kunywa kahawa au chai.
Endapo utapenda kunywa kahawa au chai unashauriwa kuondoa caffeine kabla hujaitumia. Loweka ‘tea bag’ au ‘coffee grounds’ kwenye maji ya moto kidogo kwa muda wa sekunde 30 kisha kamua (squeeze) ‘tea bag’ au ‘coffee grounds’ kwa kugandamiza kwenye ukuta wa chombo au kikombe kwa kutumia kijiko. Kisha mwaga maji. Hii huondoa asilimia 90 ya caffeine.
11.  Unguza mafuta yaliyohifadhiwa ndani ya ngozi ya mwili wako kwa kufanya yafuatayo:-

  • Kula chakula kiasi kidogo kwa wakati na ule mara kwa mara badala ya kula mlo mmoja mkubwa kwa wakati mmoja. Hii itasaidia mwili kuunguza chakula ipasavyo badala ya chakula kingine kuhifadhiwa kama mafuta mwilini.
  • Kunywa maji baridi glasi moja (ice water) kabla ya kula chakula. Maji ya baridi hushusha joto la mwili hivyo utakapokula chakula mwili huunguza chakula hicho haraka ili kurejesha joto lililopotea.
  • Kunywa mafuta ya nazi (coconut oil) vijiko vikubwa viwili kila siku. Kwa kipindi cha miezi miwili au mitatu unywaji wa mafuta ya nazi pekee yake utapunguza uzito wa mwili wako kwa kilo 6.75 hadi 9.
  • Fanya mazoezi ya viungo. Mazoezi mazuri kiafya kufanya ni kutembea kupanda na kushuka kilima au ngazi (stairs) au kwenye eneo tambarare. Tumia saa moja kila siku kwa siku tano kwa wiki. Mazoezi mengine sio mazuri sana kwa mwili (unhealthy forms of exercises) kama kukimbia (jogging) na mengine ambayo huathiri pingili(cartilage), misuli na mifupa ya mwili.

No comments:

Post a Comment