Tatizo hili
husababishwa na kutokula matunda na mboga za majani zakutosha au kutokula
vyakula ambavyo havijakobolewa au kuondolewa uasili wake ambavyo kimsingi vina
nyuzi (fiber) zinazosaidia kusafisha utumbo mpana (Colon) na kwenda choo
ipasavyo. Pia kutokufanya mazoezi ya mwili na kunywa maji ya kutosha (angalau
glasi 8 kila siku).
Usipopata choo
(angalau mara mbili au tatu kwa siku) au hata kama ni mara moja lakini choo
kingi, utakabiliwa na magonjwa mbalimbali. Asilimia takriban 70 ya magonjwa
yote hutokana na tatizo la kutokusafishwa vya kutosha kwa utumbo mpana (Colon).
Usipopata choo wakati unakula kila siku basi fahamu kwamba ndani ya colon
kumegandamana uchafu na sumu za kutosha. Pia nakushauri mara tu ukisikia haja
wahi haraka ukaitoe chooni. Kubana choo kwa muda mrefu pia ina madhara kiafya.
Sasa kwa tatizo hilo ni vema kuanza na program ya kusafisha utumbo mpana (Colon) iitwayo ‘Salt
Water Flush Program’. Hii uifanye siku ukiwa huna kazi na uko nyumbani. Chukua
maji ya vuguvugu lita moja, weka weka chumvi ya baharini (sea salt) ambayo
inauzwa madukani au supermarkets. Sio chumvi ya kuchimbwa ardhini bali
iliyovunwa kutokana na maji ya bahari. Kunywa hayo maji ndani ya kipindi cha
dakika 45 tu.
Kisha lalia ubavu wa
kushoto ili kuruhusu maji yatoke tumboni kuingia kwenye utumbo mwembamba. Mara
tu ukijisikia kwenda choo nenda mara moja. Endelea kwenda choo mpaka hali ya
kusikia choo itakapokoma. Itakuchukua takribani masaa manne hivi.
Baada ya zoezi hilo
utafanya hatua ya pili ya Kusafisha utumbo kwa Juisi. Tengeneza juisi yenye
mchanganyiko wa matunda matatu, manne au zaidi kati ya matunda haya: Apples,
Oranges, Avocados, Raspberries, Papai, Strawberries, Blackberries, Pears, Figs
na Prunes. Kunywa kila siku mpaka hali ya kutopata choo itakapoacha. Baada ya
hapo sasa uwe na mikakati mizuri ya ulaji chakula (balanced diet).
Juice ingine ukipenda
kwa ajili ya tatizo hilo: Blend vipande vya nanasi (kikombe 1), nusu chungwa na
papai moja na mbegu zake (ila tu ulimenye). Blend kwenye blender na kunywa.
VERY HELPFUL BLOG. ASANTE
ReplyDeleteSure Ismail. You are welcome
Delete