Watu wengi tunatumia vipodozi bila hata kufikiria madhara ya sumu zilizomo katika baadhi ya vipodozi. Aina nyingi ya
vipodozi vya viwandani (synthetic beauty products) vimetengenezwa kwa viambato
(ingredients) vyenye sumu (toxins) ndani yake. Sumu hizi huleta uharibifu
kwenye ini na pia huleta saratani (liver-damaging and cancer causing toxins)
vinapotumiwa kwa muda mrefu. Kadhalika vipodozi vya viwandani hutengenezwa kwa
viambata vinavyosaidia ufyonzaji wa vipodozi ndani kabisa ya ngozi kwa lengo la
kuleta uzuri wa ngozi uliokusudiwa kwa mujibu wa kampuni husika ya vipodozi.
Viambata hivi ambavyo kitalaam huitwa ‘penetration enhancers/sorption
promoters/accellerants’ ni pamoja na alcohol (ethanol), glycols (propylene
glycol), sulfactants, nk.
Sasa mtumiaji wa
vipodozi hivi anapopaka kwenye ngozi sumu hupenya ndani ya ngozi na
kusafirishwa kwa njia ya damu kwenda kwenye viungo vya ndani (internal organs).
Mwilini uchujaji hufanyika ambapo ini huusika na hutolewa nje ya mwili na figo uchafu au takasumu (flushed out). Hata hivyo baadhi ya sumu hubaki mwilini na huendelea kuongezeka
kiwango chake kadiri tunavyoendelea kutumia vipodozi. Kwa vile ngozi ndio
kiungo kikubwa katika miili yetu sumu nyingi kukaa ndani ya ngozi. Ndani ya
miili yetu sumu hizi kuchangamana na kemikali za asili za miili yetu na
kusababisha mabdiriko ya ukuaji wa chembe chembe za miili yetu hali inayopelekea
saratani. Madhara mengine ya kiafya yanayosababisha na vipodozi vya viwandani
ni pamoja na mzio (allergies), kutokupata ujauzito (infertility), kuzeeka kabla
ya wakati (aging prematurely), diabetes, na mengineyo ikiwa ni pamoja na
wanawake kuota ndevu! Siku hizi kuna ongezeko kubwa la wanawake kuota ndevu…
Tuwe makini na
utunzaji na kujali ngozi za miili yetu. Vipodozi vya viwandani ni hatari
wandugu zangu. Ngozi ya binadamu kiasi cha ‘square inch’ ina sweat glands 650,
blood vessels 20, chembe chembe 60,000 zinazotengeneza rangi ya ngozi na zaidi
ya 1,000,000 ya nerve endings. Hii ina maana kwamba ngozi ya binadamu ina midomo mingi (skin pores) iliyo tayari
tayari kula chochote kinachogusana nayo kama vile vipodozi. Hapo ndio uone
jinsi gani ngozi inapaswa kuangaliwa sana maana ni rahisi sana kuulisha mwili wako sumu kupitia vipodozi unavyotumia!
Katika nyakati hizi
zipo zaidi ya aina 100,000 za kemikali zinazotumika kutengeneza aina mbalimbali
ya bidhaa tunazotumia kama vile rangi na vipodozi. Bahati mbaya sana ni
asilimia 5 tu ya kemikali hizo zimefanyiwa majaribio ya kimaabara ili kujua
madhara yake kwa afya ya binadamu. Hii ina maana asilimia 95 ya kemikali hizo
bado hazijafanyiwa majaribio ya kitalaam na tunazitumia kupitia vitu kama
vipodozi. Mathalani zebaki (mercury) ilikuwa ikitumika katika vipodozi kwa muda
mrefu mpaka hivi karibuni ilipopigwa marufuku baada ya kufanyika utafiti kuhusu
madhara yake.
No comments:
Post a Comment