Niliwahi kuulizwa swali lifuatalo na dada mmoja kupitia mtandao:
"Ninapo ingia siku zangu natokwa damu sana na tumbo linaniuma
sana
Naomba nisaidie maana huwa inapelekea hadi kulazwa hospitali".
Naomba nisaidie maana huwa inapelekea hadi kulazwa hospitali".
Wapo wanawake wengi wanaosumbuka kama huyo dada aliyeniuliza hilo swali. Ningependa niende moja kwa moja kuelezea tiba ambazo mwanamke anaweza kutumia ili kutataua matatizo hayo.
Kwa Tatizo la kutoka damu nyingi sana:
Tiba ya kwanza, chuma maua ya
mgomba (kabla hayafikia hatua ya kuwa ndizi) kisha chemsha na ule pamoja na
maziwa ya mgando (curd). Maua ya mgomba huongeza progesterone hormone na kutibu
tatizo la kutoka damu nyingi wakati wa siku zako.
Tiba ya pili, tengeneza juisi
ya viazi sukari (beet) na utumie 60-90ml mara tatu kwa siku ukiwa katika siku
zako.
Tiba ya tatu, chukua gramu 6 za coriander (tafuta Kiswahili chake ila
supermarket na sokoni zipo) weka kwenye lita moja ya maji safi. Chemsha hadi
maji yabaki nusu lita, ipua kwenye moto na kunywa maji yangali vuguvugu.
Kwa tatizo la maumivu makali wakati wa hedhi:
Siku
mbili kabla ya kuanza hedhi anza hii tiba. Chukua mbegu za ufuta (sesame seeds) nusu
kijiko cha kidogo (teaspoon) weka kwenye glasi ya maji moto koroga na kunywa ikiwa bado vuguvugu.
Kunywa mara mbili kwa siku hadi kipindi cha hedhi kimalizike.
NAOMBA KUJUA KAMA MBEGU IZO ZA UFUTA ZIWE ZIMESAGWA AUA LAA
ReplyDelete