Tuesday 18 August 2015

Faida na Manufaa ya Parachichi katika Kutibu Tatizo la Cholesterol na Afya ya Ini


Image result for avocado photos

Parachichi licha ya kuwa ni tunda lakini pia huweza kuwekwa kwenye fungu la matunda kwa kuwa hutumika kwenye kutengeneza saladi. Parachichi huwa aliivi likiwa bado kwenye mti wa mparachichi yaani parachichi huiva baada ya kuchumwa kutoka kwenye maparachichi. Katika hatua ya kuiva parachichi hubadirika rangi kutoka rangi ya kijani na kuwa na rangi nyeusi.

Ukitaka kujua parachichi bora wakati unanunua tikisa parachichi. Ukisikia linatoa mlio wa kokwa kwa ndani basi hilo sio parachichi zuri. Parachichi zuri halitoi mlio likitikiswa na unaweza kujua limeiva kwa kulibonyeza. Ukitaka parachichi liive haraka liweke kwenye mfuko (paper bag) litaiva ndani ya siku mbili tu.

Parachichi ni tunda lenye kiwango kikubwa cha mafuta (highest-fat fruits) hivyo watu wenye magonjwa ya moyo wanapaswa kujiepusha ulaji wa tunda hili. Hata hivyo ulaji wa tunda hili pamoja na mafuta (moni unsaturated fats) khasa mafuta ya mizeituni (olive oil) huweza kupunguza kiwango cha cholesterol kwa asilimia 8 (8%) and hivyo ni tunda muhimu kwa kupunguza tatizo la ugonjwa wa moyo. 

Inashauriwa kula parachichi moja au mawili kila siku ili kupunguza kiwango cha cholesterol mwilini na pia kusaidia kuliweka ini katika hali njema ya kiafya. Aidha, kabla ya kuchukua hatua za kupunguza cholesterol mwilini ni vema kwanza ukapimwa hospitali ili kujua kama kiwango cha cholesterol mwilini mwako kiko juu au la. Kumbuka asilimia 70 ya cholesterol katika miili yetu hutengenezwa na ini na huwa na kazi muhimu miilini mwetu ikiwa ni pamoja na kuzalisha nyongo inayosaidia usagaji wa vyakula vya mafuta, husaidia ujengaji wa seli za mwili na pia husaidia kutengeneza homoni za mapenzi. Asilimia 30 ya cholesterol hutokana na vyakula tunavyokula hasa vile vyenye mafuta au vyenye asili ya nyama. Aina hii ya cholesterol ndiyo mbaya zaidi inapozidi katika miili yetu.

Mwisho, kama umepimwa na kubainika kuwa una tatizo la kiwango kikubwa cha cholesterol tangeneza aina hii ya juisi: Chukua mboga za parseley na spinach kiasi, karoti 4 na punje moja ya kitunguu swaumu. Katakata kisha weka kwenye blender na tengeneza juisi. Kunywa na baada ya siku kadhaa nenda tena kapime. Kama bado endelea kutengeneza na kutumia juisi hiyo mpaka kiwango cha cholesterol kiwe normal


No comments:

Post a Comment