Saturday 24 October 2015

Utafanya Nini kumsaidia Mama Aliyejifungua Anayevuja Damu Nyingi?


Wanawake ni mama zetu. Kila binadamu amezaliwa na mwanamke baada ya miezi tisa ya kukaa ndani ya tumbo la uzazi la mwanamke. Licha ya mwanamke kukabiliwa na kipindi kigumu cha kutunza ujauzito kwa miezi tisa hadi kujifungua lakini mwanamke anakabiliwa na hatari ya kuvuja damu nyingi wakati wa kujifungua. Katika hali ya kawaida ya kujifungua mtoto mwanamke hapaswi kuvuja damu zaidi ya vikombe viwili yaani 240ml ya damu.
Endapo itatokea mwanamke kuvuja damu nyingi msaidie kwa kufanya mambo yafuatayo:

  1. Chukua unga wa pilipili iitwayo kwa kiingereza 'Cayenne pepper' kiasi cha robo kijiko cha chai weka kwenye maji moto glasi moja. Tia asali na limao. Mnyweshe kila baada ya dakika kumi.
  2. Mfanyie masaji ya tumbo kwa upande wa chini. Fanya masaji hiyo kwa kuzungusha vidole au viganja kwenye tumbo kama unachora duara kwenye tumbo (firm but gentle circular motion). Hii itasaidia mji wa mimba (uterus) kuwa mgumu na hivyo kupungua uvujaji damu! 

No comments:

Post a Comment