Saturday, 24 October 2015

Huduma Ya Kwanza Kwa Mtu Aliyekula Au Kunywa Sumu


Mtu anaweza kula au kulishwa sumu katika mazingira mbalimbali. Kuna watu wengine huamua kujaribu kukatisha maisha yao kwa kunywa sumu kutokana na sababu mbalimbali za kimaisha. Lakini vyovyote iwavyo katika maisha yako au ya ndugu, jamaa na rafiki kukatisha maisha kwa kula au kunywa sumu sio suluhisho la kukimbia matatizo ya maisha bali ni kuingia kwenye matatizo makubwa mno kwani huko roho itakapokwenda ni MAJUTO MAKUU!

Endapo itatokea mtu amekunywa sumu au amekula chakula chenye sumu muwahishe hospitali au kituo cha afya haraka kama utaona hali hizi: kuwa na kichefuchefu, kutapika au kuharisha, damu kwenye kinyesi, kukosa mkojo, mate kuwa machache mdomoni na yenye mnato au macho kuingia ndani.

Wakati unafanya harakati za kumpeleka kwenye kituo cha afya, mpe tiba mojawapo ya hizi: Pia ukiona sumu sio kali sana maana mara nyingine tunaweza kula chakula lakini baada ya muda fulani tunasikia matumbo yanauma au tunaharisha, tumia tiba hizi:

  1. Changanya siki aina ya 'Apple cider vinegar' kijiko cha chai (15ml) kwenye maji ya moto au vuguvugu kiasi cha kikombe kimoja (230ml) kisha mpe anywe. Rudia kila baada ya masaa 2 - 3.
  2. Saga mkaa kisha chukua kiasi cha unga wa mkaa (500mg - 1g) changanya kwenye maji kikombe kimoja (230ml) mpe anywe. Rudia kila baada ya masaa 2- 3.
Kwa tumbo linalouma kutokana na sumu au chakula chenye sumu alichokula mtu anywe chai iliki au peppermint ili kutuliza tumbo. peppermint au iliki ni viungo vya vyakula vinavyopatikana sokoni au suppermarket. Apple cider vinegar ina matumizi mengi sana katika maisha yetu ya kila siku hivyo ni bidhaa muhimu kuwa nayo nyumbani kwako!

No comments:

Post a Comment