Thursday, 13 August 2015

Tiba ya Vidonda vya Tumbo (Peptic Ulcers) Hii Hapa


Image result for stomach pain photos


Vidonda vya tumbo (Peptic Ulcers) kimsingi ni vidonda kama aina nyingine ya vidonda ambavyo huweza kutokea nje ya mwili wa binadamu tofauti ni kwamba vidonda hivi hutokea kwenye kuta za tumbo au kwenye duodenum ambayo ni sehemu (gateway) ya kati ya tumbo na utumbo mdogo. vidonda hivi huitwa Peptic ulcers kwa sababu hujitokeza kwenye eneo ambalo kimeng'enywa (enzyme) kiitwacho pepsin hufanyia kazi wakati wa uyeyushaji wa chakula. Wanaume wako katika hatari ya kupatwa na vidonda hivi mara nne zaidi ya wanawake.


Kwa kipindi cha miaka mingi iliyopita wanasayansi waliamini kwamba tatizo la vidonda vya tumbo husababishwa na stress anazokuwa nazo mtu. Hivi sasa imebainika bayana kwamba chanzo kikubwa cha mtu kupatwa na vidonda vya tumbo sio stress bali ni aina ya bakteria waitwao Helicobacter pylori (H. pylori) au kwa jina lingine Campylobacter pylori. Lakini mtu kuwa na aina hiyo ya bakteria mwilini mwake haina maana kwamba ndio atapata vidonda vya tumbo. Hata hivyo asilimia 75 ya watu waliopatwa na tatizo la vidonda vya tumbo walibainika kuwa na bakteria wa H. pylori.

Sasa tuangalie tiba ya vidonda vya tumbo. Hii ni tiba ambayo mtu yeyote anaweza kuiandaa na kuitumia. 
TIBA YA KWANZA: Anti-ulcer Fruit Cocktail
Vitu vinavyotakiwa ni hivi: Ndizi, Nanasi, matunda ya Blueberries, Mdalasini iliyosagwa kuwa unga, Unga wa karafuu, Unga wa Tangawizi na Asali.
Jinsi ya Kutengeneza: Kata vipande ndizi na nanasi kulingana na kiasi unachohitaji wewe. Weka kwenye bakuli. Weka matunda ya brueberries. Weka unga wa mdalasini, tangawizi na karafuu. Weka asali kiasi kama unatumia asali. Kisha kula huo mchanganyiko.

TIBA YA PILI: Tengeneza juisi mchanganyiko kwa kublendi pamoja juisi ya matunda ya brueberries, juisi ya nanasi na ndizi kisha tia unga wa mdalasini, tangawizi na karafuu. Tumia hiyo juisi katika kipindi cha baina ya mlo wa mchana na mlo wa jioni yaani 'between meal'.

TIBA YA TATU: Anti-ulcer Cabbage Soup
Vitu unavyohitaji: Maji vikombe 3, cabbage ikiyosagwa au katwakatwa, mboga ya celery kikombe kimoja, viazi (potatoes) vilivyokatwa vipande nusu kikombe, bamia zilizokatwakatwa nusu kikombe, kitunguu maji kilichokatwakatwa nusu kikombe, na nusu kikombe kwa kila viungo hivi vikiwa katika hali ya unga: green pepper, red pepper, black pepper, mdalasini na karafuu.
Namna ya kuandaa: Weka maji, cabbage, celery, viazi, bamia, vitunguu na green peppers kwenye chombo cha kupikia supu. Chemsha hadi supu hiyo ichemke. Punguza moto na endelea kutokosa kwenye moto kiasi huku ukiwa umeifunika. Baada ya hapo itie radha supu yako kwa kuweka viungo vyote kama nilivyovitaja hapo juu.

Baada ya kueleza hizo tiba tatu hapo juu hebu nieleze nini kimo katika vitu nilivyovitaja na namna vinavyohusika katika kupambana na vidonda vya tumbo kama ifuatavyo:

Tangawizi (Ginger): Hii ina compounds 11 ambazo zinasaidia kupambana na vidonda vya tumbo. Compounds hizo ni hizi: 6-shagaol, 6-gingerol, 8-shagaol, 8-gingerol, 10-gingerol, ar-curcumene, beta-bisalene, 6-gingediol, betases-quiphellandrene, 6-gingerdione na 6-paradol. Ukitia unga wa tangawizi kwenye asali mbichi na kuchanganya vizuri ni tiba nzuri ya vidonda vya tumbo.

Ndizi (Banana): Ndizi ni rafiki tiba wa muda mrefu wa magonjwa mbalimbali ya tumbo. Ndizi ina anti-ulcer effect.

Cabbage: Juisi ya kabeji (Raw cabbage juice) ni rafiki tiba mzuri kwa kutibu vidonda vya tumbo.Juisi ya cabbage ina compounds mbili ambazo ni Glutamine na S-methyl-methionine ambazo ni anti-ulcer. Profesa Melvyn Werbach, M.D. wa Chuo Kikuu cha California nchini Marekani alifanya utafiti wa watu wenye tatizo la vidonda vya tumbo kwa kuwapa juisi ya cabbage. Matokeo ya utafiti wake ulibaini kwamba asilimia 92 ya wahanga hao walipata nafuu nzuri ndani ya kipindi kifupi cha wiki tatu tu za kutumia juisi hiyo.

Nanasi (Pineapple): Ina compound ya glutamine kama ilivyo kwa cabbage ambayo ina anti-ulcer effects. Kadhalika cabbage ina compound iitwayo bromelain inayosaidia kwenye usagaji wa chakula mwilini.

Red pepper: Watu wengi wanaamini aina hii ya pilipili husababisha vidonda vya tumbo. Ukweli ni kinyume chake. Pilipili hizo zina compound iitwayo capsaicin ambayo hufanya pilipili hiyo kuwa na rangi nyekundu. Compound hiyo husaidia kukinga kuta za tumbo dhidi ya vidonda vya tumbo.

Blueberry: Ina compound iitwayo anthocyanosides ambayo husaidia uzalishaji wa ute ute (mucus) ambayo hufunika kuta za tumbo hivyo kulinda kuta za tumbo dhidi ya asidi za uyeyushaji chakula (digestive acids).



No comments:

Post a Comment