Wednesday, 12 August 2015

Unazijua Sababu za Wanawake Kujiingiza Kwenye Usagaji?



Usagaji (lesbianism) ni tabia ya wasichana/wanawake kujiridhisha kimapenzi wenyewe pasi kuhitaji kuridhishwa na mwanaume. Wasichana hawa hutumia vidole, ulimi na hata sex toys (dildo)  wakati wa kufanya tendo hilo. Wengi wa wasichana wanaojihusisha na tabia hiyo hufurahia zaidi tendo hilo tena kuliko hata wakifanya na wanaume na hivyo kuwafanya wajione kwamba hawana sababu ya kuwa na wenzi wa kiume. Sababu kuu ambazo huwafanya wasichana wengi kujiingiza kwenye tabia hii na hata kuona ndiyo mfumo sahihi wa maisha yao ni pamoja na hizi zifuatazo:


• Kuiga kutoka kwa wenzao: wengi wa wasichana ambao wamejikuta wana tabia hii wameiiga kwa wenzao, hasa wanapokuwa kwenye eneo ambalo wapo pekee yao kama vile shule hasa za bweni. Wasichana wengi ambao walisoma shule za bweni ama kuishi maisha ya hosteli walijikuta wanafundishwa tabia hii na wenzao ambao tayari walikuwa wameshaanza tabia hizi kabla ya kuja shule.

 Kutaka kujijua Miili yao: kwa kawaida watoto hupenda kujijua miili yao ilivyo (self exploration), yaani watoto wakiwa wadogo hutaka kujidadisi wawe wa kiume ama wa kike. Mfano mzuri watoto wa kiume wanapokuwa pamoja hata wakioga hujikuta wanachezeana sehemu zao za siri hadi uume unasimama, vivyo hivyo watoto wa kike hupenda kujidadisi kwa kuchunguliana sehemu zao za siri. Tabia hii kwa umri wa udogo huwa haina neno maana huishia hapo lakini wapo wachache ambao tabia hii hawaiachi huiendeleza hadi ukubwani na hivyo kuwa ni sababisho la kujiingiza kwenye mapenzi ya jinsia moja.


• Homoni katika Miili: Hii hutokana na jinsi binti alivyozaliwa. Kuna baadhi ya mabianti ambao wamezaliwa na hormone za kiume na hivyo kujikuta kwamba wana tabia za kiume. Wengi wa mabinti ambao wana tabia hizi kwenye mashule ya bweni huwa na desturi ya kuoa na hivyo kuitana mume na mke na wao huwa na tabia za kukaa kimapenzi mapenzi na hao wanaowaita waume ama wake. Wasichana kama hawa huweza kuwashawishi sana wale ambao ni wasichana wa kawaida hadi kujikuta wanaanza tabia hii ya kusagana wakiwa mashuleni na wakisha ianza basi huwa siyo rahisi kuiacha mpaka nguvu nying zimetumika kumfanya aache.


• Raha itokanayo na tendo lenyewe: wengi wa wasichana /mabinti wanaoshiriki tendo hili huwa wanadai wanaridhika sana kimapenzi wanapofanya hivi ukilinganisha na wakiwa wanafanya na wanaume. Kutokana na tabia hii wengi wa wanwake ambao wako kwenye mahusiano ya kindoa hujikuta wanafanya hii tabia ili tu kuridhika kwasababu wanapofanya na jinsia ya kiume hawaridhiki.

• Maudhi ya mahusiano ya jinsia tofauti (heterosexual): maudhi yatokanayo na mahusiano ya jinsia mbili huwa yanawakinai wengi wa wasichana/ wanawake na hivyo kugeukia upande wa pili ambapo wanaamini kwamba hakuna maudhi hayo. Wanajua wazi kwamba wakiwa wenyewe watabembelezana  na kupeana raha zisizokuwa na maudhi.


• Umbali kutoka walipo wenzi wao: Baadhi ya wanawake ambao waume zao wako mbali nao kwa mauda mrefu wamejikuta wakiwa na mahusiano na jinsia moja kwa kigezo kwamba hawataki kuwasaliti waume zao. Na kwamba wanataka waume zao wakirudi wawakute hawajatumika kabisa. Sikatai usaliti ni mbaya lakini hata huu wa jinsia moja nao ni usaliti tu.

No comments:

Post a Comment