Friday, 18 September 2015

Tatua Tatizo la Kunuka Kinywa Chako


Image result for white teeth photos
Afya ya mtu huanzia kwenye harufu ya mwili wake. Hakuna harufu inayoonyesha jinsi gani ulivyo msafi kama harufu ya kinywa. Je ulishawahi kuongea na mtu na ghafla ukajikuta unakosa hamu ya kuendelea sababu kinywa kinatoa harufu mbaya? Nafahamu kero hii inavyokuwa.

Kinywa ni muhimu kufanyiwa usafi wa hali ya juu ili kuhakikisha unapunguza harufu mbaya ya kukinaisha. Harufu ya kinywa, inakera na kuudhi. Kwa bahati mbaya huwa hatujui kama midoyo yetu inatoa harufu mbaya, bali wale tu wanaopata kuvuta hewa itokayo midomoni mwetu. Hii inakuwa ngumu kutatua tatizo sababu unaweza kudhani kila kitu kiko vizuri, kumbe unawapa watu wakati mgumu wakati wa mazungumzo. Harufu mbaya haifurahiwi, hasa ikiwa inatoka kwenye vinywa vyetu. Je nini kinasabisha vinywa kutoa harufu mbaya kiasi hiki? Hizi hapa sababu chache za kufanya kinywa kutoa harufu mbaya.

Kutosafisha vizuri kinywa vizuri

Kwa kawaida unatakiwa kusukutua kinywa chako angalau mara mbili kwa siku - asubuhi na usiku kabla ya kulala. Wakati wa kusafisha kinywa, hakikisha umesugua vizuri ulimi. Meno na fizi havina tatizo sana, bali ulimi ndio sehemu kubwa ambapo bakteria wanajijenga. Vilevile, ni ulimi unaosababisha kinywa kunuka. Ni vizuri kama utasafisha vizuri ulimi ili kuondoa harufu.

Ni vizuri kufahamu kuwa mswaki unatakiwa kubadilishwa kila baada ya muda - angalau kila mwezi. Usitumie mswaki kwa muda mrefu, maana hauwezi kusafisha kinywa chako kwa ufasaha kama inavyotakiwa maana wengine wanatumia mswaki kwa mwaka na zaidi. Je utaacha kunuka kinywa? 

Kutokula chakula vizuri

Harufu ya kinywa inaashiria kutokula chakula na kinywaji kwa muda mrefu. Kuwa na njaa husababisha mdomo kuwa mkavu. Mara nyingi harufu mbaya ya kinywa hupotea mara tu baada ya kula chakula kizuri na mdomo ukiwa una mate ya kutosha. Acha kutumia vyakula na vinywaji vinavyoongeza harufu kali mdomoni na kukupunguzia maji mwilini – mfano pombe, viungo kama kitunguu maji au kitunguu saumu.

Kinywa kikavu

Bakteria hushamiri kwenye kinywa kikavu. Kama hupendi kunywa maji mengi na kinywa chako kinakuwa kikavu mara nyingi basi jua kuwa kunuka kinywa kwako ni jambo la kawaida.

Jinsi ya kutatua tatizo

Hakikisha mdomo haukauki

Kwa kawaida mdomo mkavu hutoa harufu mbaya. Hii ndio sababu kuwa kinywa chako kinanuka sana asubuhi sababu mdomo wako unatengeneza mate machache sana ukiwa umelala. Mate ni adui wa harufu mbaya mdomoni siyo tu sababu inaondoa bakteria na masalia ya chakula, bali mate yana vimengenyo vinavyoua na kuzuia kuzaliana kwa vijidudu kwenye kinywa. Ili kuzuia kunuka, jaribu kufanya haya
  • Kunywa maji mengi ili kuondoa masalia ya chakula na bakteria
  •  Tafuna bazoka, sababu bazoka inasababisha mdomo kuwa na mate mengi. Kuwa makini katika kuchagua bazoka zisizo na sukari.  Sukari ni adui mkubwa wa kinywa chenye afya.

Piga mswaki kabla ya kulala

Kupiga mswaki ni muhimu, lakini wengi tunasahau kuwa mswaki ni lazima kupiga angalau mara mbili kwa siku haswa usiku naasubuhi.  Kupiga mswaki asubuhi ni muhimu ili kuondoa uchafu uliojijenga usiku kucha na hivyo harufu mbaya - lakini siku nzima mdomo unatengeneza mate na kuwa laini.  Hii ni tofauti na usiku. Usiku mdomo hubaki mkavu na mate kidogo, hivyo kuwa rahisi kwa vijidudu kuzaliana na kuharibu mazingira ya mdomoni kwako. Hivyo, ni afya zaidi kupiga mswaki usiku ili kuzuia kushamiri bakteria waharibifu wanaosababishwa na masalia ya bakteria kwenye kinywa chako.  Njia hii itasaidia kuzuia bakteria kuharibu meno na fizi, hivyo kutokuwa na harufu mbaya ya masalia wakati ukiamka.

Kula ndizi au apple

Ndizi au apple husaidia kuondoa harufu mbaya kinywani, lakini ni kwa muda mfupi sana. Ukiwa unahisi mdomo unanuka na unahitaji njia ya haraka, tafuta ndizi au apple, na hapo utakuwa umetatua tatizo kwa muda.

Kula Tango

Maji ya tango yana kemikali zinazozuia kukua kwa bakteria kwenye kinywa. Baada ya mlo mzuri wenye viungo vyenye harufu kali, kata kipande kidogo cha tango, kigandishe kwenye ukuta wa juu wa mdomo wako kwa sekunde 30 huku ukikandamiza na ulimi. Zoezi hili litasaidia kuua bakteria na kuacha kinywa chako kikiwa na afya na harufu nzuri.

Jenga Tabia ya Kupia Mabusu (Kissing)

Ni ukweli kuwa ukifanya kitu chochote kinachosababisha kutoa mate basi unazuia kunuka kinywa. Kissing ni mojawapo ya njia mbadala za kuzuia harufu mbaya mdomoni. Kiss mara nyingi uwezavyo ili kufanya mdomo wako uwe na mate mengi, na hivyo kuzuia kunuka kinywa.

Harufu ikizidi, kamuone daktari

Je harufu yako ya kinywa ni ugonjwa? Basi kamuone daktari. Wakati mwengine harufu ya kinywa hutokana na kuwa na matatizo mwilini na huwezi kuondoa kwa kutumia njia tulizozieleza hapo juu.

No comments:

Post a Comment