Wednesday, 16 September 2015

Jinsi ya Kushughulikia Tatizo la Ugumba kwa Mwanamke kwa Njia ya Asili


Ugumba kwa mwanamke ni tatizo la mwanamke kushindwa kushika mimba licha ya kushiriki kufanya mapenzi na mwanamume bila kutumia kinga. Tatizo la kutoshika mimba kwa kipindi angalau mwaka mmoja huku mwanamke huyo akishiriki kikamilifu ufanyaji mapenzi na mwanamume huitwa ugumba (Sterility). Ugumba kwa mwanamke (Sterility) sio sawa au haina maana sawa na tatizo la mwanamke kutojisikia au kutokuwa na hisia za kufanya mapenzi yaani ‘Frigidity’.

Zipo sababu nyingi zinazoweza kufanya mwanamke awe mgumba. Mwanamume pia anaweza kuwa chanzo cha ugumba kwa maana kwamba hana uwezo wa kutungisha mimba. Hivyo, ndio kusema mwanaume kamwe hapaswi kumlaumu mwanamke anayeshirikiana naye kimapenzi kuwa ndiye ‘mgumba’ wakati mwanamume na mwanamke kwa pamoja wana asilimia sawa za kuwa chanzo cha ugumba. Ndio maana mwanamume na mwanamke wanapooana na wakashiriki ngono kikamilifu kwa kipindi cha mwaka mmoja lakini hakuna dalili za mwanamke kuwa mjamzito, basi wote wawili wanapaswa kwenda kwa pamoja kwa watalaamu wa masuala ya afya ya uzazi ili kuchunguzwa kwa kufanyiwa vipimo.

Ili mwanamke apate ujauzito mwanamume hukojoa shahawa kwenye uke wa mwanamke. Shahawa husafiri kwenye uke wa mwanamke kupitia mirija ya uzazi (fallopian tube) kwenda kurutubisha yai la mwanamke (ova). Sasa ili mbegu za kiume (sperms) ziwe salama wakati zinasafiri katika uke wa mwanamke lazima majimaji katika uke yawe katika hali ya nyongo (alkaline fluid). Kama majimaji ya uke yakiwa hayako katika hali ya nyongo yaani ni tindikali (acid) mbegu za kiume zitakufa na hakutokuwa na urutubishwaji wa yai la mwanamke.

Ili majimaji ya uke wa mwanamke yawe katika hali inayotakiwa ya alkaline mambo mawili ni muhimu sana. Moja, mishipa ya neva katika uke wa mwnamke iwe inafanya kazi zake sawasawa. Mwanamke mwenye mawazo sana (nervous) sio rahisi kupata ujauzito. Hivyo ili neva ifanye kazi sawasawa mwanamke hapaswi kuwa mtu mwenye mawazo au mwenye kuudhiwa, anapaswa kula milo kamili na anapaswa kuwa na muda wa kupumzisha akili yake (adequate rest and relaxation). Jambo la pili, mwanamke anapaswa kula vyakula vinavyotengeneza alkali katika mwili ambavyo ni mboga za majani na matunda, pia kuepuka kula kwa wingi vyakula vinavyoleta asidi katika mwili.

Sasa tuangalie visababishi vya tatizo la ugumba kwa mwanamke. Visababishi hivyo ni pamoja na mapungufu ya viungo vya uzazi vya mwanamke (physical defects or structural abnormalities of genitals and reproductive organs). Mwanamke anaweza kuwa ama amezaliwa na mapungufu hayo katika mji wa mimba (womb) au njia ya uzazi (fallopian tubes) au aliyapata kutokana na ajari. Sababu nyingine huitwa ‘Physical debility’ yaani mwanamke kutokuwa na afya bora ya mwili kutokana na magonjwa yaliyompata na yakadumu katika mwili wake wa kipindi kirefu (magonjwa sugu). Magonjwa hayo ni pamoja na magonjwa ya zinaa. Kadhalika upungufu wa damu (Anaemia), kukosa choo ipasavyo (constipation) au mwanamke kuwa na uzito mkubwa (obesity) au uzito mdogo ambao hautakiwi kitalaamu yaani kwa vipimo vya Body Mass Index (BMI) huweza kufanya mwanamke asipate ujauzito.

Visababishi vingine ni mwili wa mwanamke kutokuzalisha homoni muhimu za uzazi na kutokupata mzunguko mzuri wa hedhi (lack of normal menstrual cycle) sanjari na matatizo ya kisaikolojia hususan mwanamke anapoudhiwa au anapokuwa na mawazo kutokana na kutokuzaa mtoto mapema (emotional stress, tension, mental depression, anxiety, and fear).

Matibabu kwa visababishi aina ya ‘physical defects’ mwanamke anapaswa kwenda kufanyiwa vipimo na watalaamu wa masuala ya afya ya uzazi na kushauriwa ipasavyo mambo ya kufanya. Matibabu kwa visababishi aina ya ‘physical debility’ huweza kutibika kwa njia za kawaida tu kwa kula vyakula vinavyotakiwa, kujijali na kuuheshimu mwili (yaani usafi na kujikinga na maambukizi) na kufuata sheria za asili (laws of nature).

Mwanamke mwenye tatizo la ugumba ambalo sio la mapungufu katika viungo vya uzazi anashauriwa kuanza matibabu kwa njia ya asili. Kwanza aanze kwa kufunga bila kula kwa siku mbili huku akitumia maji ya kutosha kwa ajili ya kusafisha taka katika mwili. Baada ya hapo ale mlo kamili ambao takriban asilimia 70-80 ya vyakula viwe havikupikwa (in their natural uncooked states) kwa sababu upikaji wa vyakula hupunguza au huaribu viinilishe (nutrients) vilivyomo kwenye vyakula. Mlo uwe na vyakula vya mbegu (seeds, nuts and grains), mboga za majani na matunda. Katika milo hiyo tumia pia maziwa na asali. Mafuta unayotumia katika vyakula yawe yale ya mimea (vegetable oils).

Ili mwanamke awe na mwili wenye afya njema nashauri afuate ratiba hii ya milo. Asubuhi akiamka, anywe glasi moja ya maji vuguvugu yaliyotiwa limao. Kifungua kinywa (breakfast) ijumuishe matunda (fresh fruits) kama apples, chungwa, ndizi, zabibu, na balungi na maziwa glasi moja. Chakula cha mchana ale mboga za majani zilizochemshwa kiasi (zisiive kabisa) na ziungwe kwa mafuta ya mimea au siagi na chumvi kiasi, chapatti mbili au tatu na maziwa (a glass of buttermilk). Katika kipindi cha kati ya mlo wa mchana (lunch) na mlo wa jioni/usiku (dinner) anywe juisi ya matunda (fresh) au juisi ya mboga za majani. Chakula cha usiku, ale saladi nyingi inayotokana na mboga za majani (fresh vegetables) kama nyanya, karoti, viazi sukari (beetroots), na vitunguu na maharage au jamii ya maharage yalipikwa. Wakati wa kwenda kulala, ale apple au maziwa glasi moja.

Mwanamke aepuke kula vyakula vyenye mafuta mengi, viungo vikali, chai iliyokolea sana majani, kahawa, sukari nyeupe (white sugar) na unga mweupe uliokobolewa (white flour). Unywaji wa pombe na uvutaji sigara viepukwe.
Matibabu mengine ambayo husaidia kutibu tatizo la ugumba kwa mwanamke ni kutumuia mzizi wa mti uitwao ‘banyan’. Chukua mzizi huo na ukaushe sio kwa kuuweka juani bali kivulini mpaka ukauke. Baada ya hapo unausaga kuwa unga. Changanya unga huo na maziwa na tumia usiku wakati wa kwenda kulala kwa siku tatu. Usitumie pamoja na chakula au kinywaji chochote wakati wa usiku. Unaweza ku-google ili kuujua mti uitwao banyan. Namna ya kuchanganya: pima kwa uzito, unga wa banyani uwe na uzito mara tano ya uzito wa maziwa.


Tiba nyingine ni mwanamke kula bilinganya (eggplants) zilizopikwa. Ale pamoja na maziwa buttermilk kila siku kwa mwezi mmoja au miezi miwili hivi. Mlo huu huongeza mwilini homoni ya uzazi iitwayo progesterone na pia huongeza uwezo wa mwili kutumia vitamin E inayopatikana kwenye chakula anachokula. Bila kusahau mwanamke ahakikishe anakuwa na uwiano wa uzito na urefu wa mwili unaostahili.    

1 comment:

  1. Kutana na mtaalamu wa mitishamba anatibu ugumba.uzazi nguvu za kiume...kukuza na kurefusha uume...magonjwa ya ini hepatitis b na a..hedhi..presha kisukari ..kansa..cd 4 za ukimwi
    ..kukuza makalio hips na shape kwa dawa asili..mpigie dr kupitia 0744903557 tanga ..

    ReplyDelete