Tuesday 4 August 2015

Tunda la Pesheni Kwa Tiba na Afya Yako


Pesheni (Passionfruit) licha ya kuwa ni tunda ambalo lina vitamins A na C pia ni tiba kwa matatizo au magonjwa mbalimbali kama vile Kutopata choo na UTI.


  1. Mapesheni mawili, chungwa moja na vipande viwili vya tikiti maji vikitengenezwa juisi kwa pamoja kwa kutumia blender kufanya glasi moja ya juisi na kunywewa asubuhi kabla ya kula chakula chochote ni kinywaji murua kwa afya (good health tonic)
  2. Ulaji wa matunda mawili au matatu ya pesheni pamoja na nyama na mbegu zake za ndani kuupa mwili nyuzi lishe (fibre), calcium na viinilishe muhimu kwa kusaidia kuondokana na tatizo la kutopata choo (Constipation).
  3. Juisi ya pasheni kiasi cha vikombe 2 akipewa mtoto msumbufu au alichengamka kupita kiasi (hyperactive child) hufanya mtoto huyo atulie (calm).
  4. Chai iliyotengenezwa kwa kuchemsha maji yaliyotiwa maua ya mti wa mpasheni hutibu magonjwa ya pumu (asthma), kikohozi cha mfululizo (whooping cough) na matatizo ya mfumo wa hewa (bronchitis). kunywa mara moja hadi tatu kwa siku.
  5. Ukiwa unakabiliwa na tatizo la UTI mara kwa mara au unataka kujikinga na ugonjwa huo jenga tabia ya kula matunda ya pesheni.


3 comments: