Tatizo
la uwezo wa kufanya tendo la ndoa linazidi kukua miongoni wa wanandoa na
wapenzi wengi. Takwimu za kitafiti zinaonyesha kuwa karibu ndoa 4 kati ya 10
zenye umri wa miaka 3 na kuendelea zinakabiliana na tatizo hili. Aidha wanaume
6 kati ya 10 wanatajwa kulalamikia upungufu wa nguvu za kiume.
Pamoja
na matatizo mengine kutajwa kuchangia upungufu wa nguvu za kiume na kushuka kwa
msisimko wa tendo miongoni mwa wanandoa, uchunguzi umeonesha kuwa utumiaji
holela wa vyakula hasa vyenye mafuta ni moja kati ya sababu zinazochangia kwa
kasi tatizo hili.
Kwa
kuzingatia hilo, watafiti wa masuala ya uhusiano wa kimapenzi wamebaini aina
mbalimbali ya vyakula ambavyo vina uwezo wa kumuongezea mtu nguvu ya kufanya
tendo la ndoa. Vyakula hivyo ni hivi vifuatavyo:
PILIPILI
Kama tunavyojua wote mara nyingi chakula ambacho kimeungwa pilipili hufanya hata mapigo ya moyo kuwa tofauti na wakati mwingine hata jasho au kamasi hutoka. Ndani ya pilipili kuna kitu kinaitwa capsaicin ambacho hufanya pilipili iwe na hali ya ukali. Capsaicin huwezesha ubongo kutoa homoni ya endorphins ambayo huleta mgusu wa hisia za raha wakati wa kufanya tendo la ndoa.
Pia pilipili husisimua mfumo wa fahamu (nerves) wa ubongo
na katika kufanya hivyo huwezesha kuamshwa haraka kimapenzi (kunyegeka) wakati
wa tendo la ndoa na pia ukiguswa au kubusiwa au kunyonywa au kupapaswa unapata hisia
kila sehemu ya mwili.
MATUNDA
NA MBOGA ZA MAJANI
Ulaji wa matunda na mboga za majani
una matokeo makubwa sana katika hamu ya tendo la ndoa kwa njia nyingi. Kwanza
matunda na mboga za majani hupunguza kiwango cha mafuta na unene (cholesterol). Kuongezeka kwa mafuta mwilini huzuia mzunguko
wa damu kwa kubana mishipa ya damu.
Pia kula matunda na mboga za majani
huhakikisha balance ya uzito kwani unene (obesity) kwa wanaume
kuna matokeo mabaya katika kuzalisha homeni za testoeterone na hatimaye
jogoo kushindwa kuwika na kuwa na pia mwanaume anakuwa na hisia za mapenzi (libido)
kidogo.
Na pia wanandoa wanapozidi kunenepeana ndipo na hali ya
kufurahia au kuwa na hamu ya tendo la ndoa huzidi kupungua. Kitalaam inashauriwa
kula milo (potions) 3-5 za matunda kwa siku.
NAFAKA
ZISIZOKOBOLEWA
Nafaka hasa zisizokobolewa kama
mahindi, ngano, uwele, nk zina nyuzinyuzi (fibre) na sukari ngumu (complex
sugar) ambazo kusaidia kutunza uzito wa mwili. Nafaka husaidia katika
kuzalisha homoni za testosterone kwenye damu. Na pia nafaka huwezesha
mtu kuwa na nguvu hatimaye kwenda masafa marefu wakati wa tendo.
Kula nafaka nzima kama vile brown bread badala ya white bread,
pia kula nafaka halisi badala ya cornflakes ni jambo zuri
linalokuhakikisha afya nejama na mahusiano mazuri ya ndoa yako.
TANGAWIZI
Tangawizi ni kiungo cha mboga
ambacho husisimua sana na kusaidia mfumo wa mzunguko wa damu mwilini. Tangawizi
zinajulikana sana kwa kusukuma damu kwenda sehemu za viungo vya uzazi yaani uke
na uume hivyo kuwa na umuhimu sana katika kuboresha ufanyaji wa tendo la ndoa. Inaweza
kuliwa mbichi, au kuliwa ikiwa imeungwa kwenye chakula au kusagwa na kuwa kama
unga na kutumiwa kama chai.
ASALI
Asali ina madini yanayoitwa boron,
ambayo husaidia mwili kutumia homoni ya estrogen ambayo ni homoni
inayohusika na viungo ya uzazi na mapenzi kwa mwanamke.
Pia kuna utafiti unaoonesha kwamba asali huongeza nguvu, kitendo ambacho kitapelekea mwanamke kuwa uwezo na hamu ya tendo la ndoa au libido.
Pia kuna utafiti unaoonesha kwamba asali huongeza nguvu, kitendo ambacho kitapelekea mwanamke kuwa uwezo na hamu ya tendo la ndoa au libido.
KARANGA
Karanga huhusika katika kuchochea mfumo wa mzunguko wa
damu (vascular system). Mzunguko wa damu ulio sawasawa katika uke na uume
huwezesha mwanaume na mwanamke kupata msisimko wa mapenzi haraka hatimaye tendo
la ndoa kuwa murua. Pia karanga zina madini muhimu kama vile magnesium,
asidi ya folic na zinc ambayo ni muhimu sana katika usalishaji wa
mbegu za mwanaume.
CHAZA
(OYSTERS) NA PWEZA
Hawa ni aina ya samaki ambao hupatikana katika maji
chumvi. Huwa na kiasi kikubwa sana cha madini ya zinc na haya madini
ndiyo huhusika zaidi na uzalishaji wa homoni ya testosterone kwa
wanaume.
Pia imethibitika kwamba wanaume wenye ukosefu wa madini
ya zinc huwa na matatizo ya nguvu za kiume. Pia madini mengi ya zinc mwilini huongeza
kiwango cha shahawa kwa wanaume.
SOYA
Pamoja na kuwa na kiwango kidogo
sana cha mafuta (fat) na pia kuwa na kiwango kizuri cha protein,
soya zina phytoestrogens ambayo husaidia sana wanawake ambao wamefikia menopause
kutengeneza homoni estrogen ya ziada.
Husaidia uke kuwa laini (wet, lubricated) mwanamke
akisisimuliwa wakati wa tendo la ndoa.
CHOKOLETI
Chocolate ina phenylethylamine, kemikali ambayo
husababisha hisia (feelings) za furaha wakati wa mwanamke au mwanaume
kufika kileleni (orgasm). Inasaidia sana kula chocolate masaa machache kabla ya
kuanza kufanya tendo la ndoa.
PARACHICHI
Aina nyingine ya chakula ambacho husaidia kuongeza uwezo wa mtu kufanya tendo
la ndoa ni Parachichi. Tunda hili linauwezo mkubwa wa kuzalisha vitamini E
ambayo husaidia katika uzalishaji wa homoni. Inatajwa kuwa watu wanaotumia
tunda hili kwa wingi huwana msisimko mkali wa kimapenzi na kwa upande wa
wanawake husaidia kuongeza majimaji yenye utelezi sehemu za siri na hivyo
kuzuia uwezekano wa kuchubuka wakati wa kujamiiana.
Ulaji wa matunda, mboga mboga na vyakula vya nafaka ni muhimu sana kwa afya na masuala ya nguvu za kiume kwa wanaume. Tusipuuze tafadhali.
ReplyDeleteAngalizo;SOYA SI NZURI KWA MWANAUME
ReplyDeleteDR KANYAS MTAALAMU WA TIBA ASILI ANAZO DAWA ASILI ZA NGUVU ZA KIUME..KUREFUSHA UUME NA KUNENEPESHA UUME..UTI..UGUMBA,,KUZIBUA MIRIJA YA UZAZI..BP..PUMU..KUKUZA HIPS NA MAKALIO KWA DAWA ASILI..NA MARADHI MENGINE MBALIMBALI..MTAFUTE DR KUPITIA 0764839091
ReplyDelete