Je, Unafahamu kwamba unaweza kuondokana na tatizo la ugumba kwa kupitia ulaji wa vyakula na kubadiri mfumo wa maisha yako bila hata kutumia tiba yoyote? soma mada hii...
Tatizo
la kukosa kuzaa au ugumba (Infertility) ni hali inayowapata wanandoa (mwanaume
na mwanamke) kufuatia mwanamke kutoshika ujauzito kwa muda wa mwaka mmoja licha
ya kufanya tendo la ndoa na mume wake mara kwa mara ndani ya kipindi hicho. Tatizo
la ugumba (Infertility) huathiri takriban ndoa moja kati ya ndoa sita kwa
wastani. Mwanaume ana asilimia 40 ya chanzo cha tatizo na mwanamke pia ana
asilimia 40. Asilimia 20 zinazobaki zinatokana na vyanzo vingine mbali na
mwamnamke au mwanaume. Kwa wanawake tatizo la kukosa kuzaa hutokana na hitilafu
kwenye mayai au mifuko ya mayai (Ovarian disorders) na kwa upande wa wanaume
tatizo hutokana na matizo yatokanayo na uzalishaji wa shahawa.
Takriban
theluthi moja (1/3) ya tatizo la ugumba kwa mwanamke (female infertility)
hutokana na yai kutokupevushwa ambayo kitalaamu huitwa ‘Onovulation’. Ili yai
lipevushwe na kuwa tayari kurutubishwa na shahawa za mwanaume homoni za
mwanamke zinapaswa kuwa katika uwiano unafaa (balance of hormones). Tatizo la
kutokuwiana kwa homoni (hormonal imbalance) hupelekea mwanamke kushindwa
kutunga mimba.
Tezi
ndogo mbili aambazo ziko katika ubongo ziitwazo ‘hypothalamus’ na ‘pituitary
gland’ husimamia uzalishaji na utendaji kazi wa homoni. Hypothalamus huzalisha
homoni ya masuala ya uzazi iitwayo ‘gonadotropin-releasing hormone (GnRH)’
ambayo huchochea tezi ya pituitary kupeleka meseji kwa mayai ya mwanamke
(ovaries). Ovaries hujibu meseji kwa
kuivisha yai na kuachilia yai hilo kwenye mirija ya uzazi (fallopian tubes) kwa
ajili ya kurutubishwa. Yapo mambo kadhaa ambayo yanaweza kuingilia utendaji
kazi wa hypothalamus hivyo kukwaza tezi hiyo kushindwa kuwasilisha meseji
sahihi kwa tezi ya pituitary. Mambo hayo ni pamoja na hali ya mawazo kutokana
na kukwazwa na mwenzi (emotional stress), mazoezi makali ya viungo, kujibana
lishe (dieting), lishe duni, mwili kuwa na mafuta kidogo (low body fat),
anorexia, matumizi ya madawa (medications) na sumu za kimazingira
(environmental toxins).
Tezi
ya pituitary huchangia utungaji mimba kwa kuzalisha homoni mbili ziitwazo
‘follicle-stimulating hormone (FSH) na ‘luteinizing hormone (LH)’. Homoni hizi
huchochea follicles katika ovaries kupevusha na kuachilia mayai yaliyokomaa kwa
ajili ya kurutubishwa. Pia hutoa amri kwa ovaries kuzalisha homoni ziitwazo
‘Estrogen’ (homoni ya kike) na ‘Progesterone’ (homoni ya kiume). Hitilafu au
kushindwa kufanya kazi sawasawa kwa tezi ya Pituitary huweza kusababisha tezi
hiyo ama kuzalisha kwa kiwango cha juu (over-produce) au katika kiwango cha
chini (under-produce) FSH na LH, hivyo upevushaji wa mayai kushindwa kufanyika.
Tezi
nyingine iitwayo thyroid endapo itatokea kuwa inafanya kazi sana kuliko
ipasavyo (hyperthyroid) au inafanya kazi chini ya kiwango chake cha ufanisi
(hypothyroid) husababisha mwili kushindwa kutumia ipasavyo homoni hivyo kuleta
tatizo la mwanamke kushindwa kutunga mimba. Kila mwanamke ana kiasi kidogo cha
homoni za kiume ziitwayo androgens. Homoni hizi ziko ndani ya damu na kuzunguka
katika mzunguko wa kawaida wa damu. Homoni hizi huzalishwa na tezi iitwayo
Adrenal. Endapo tezi za adrenal zitashindwa kufanya kazi sawasawa hali hiyo
itasababisha upevushaji wa yai kuathiriwa. Uzalishaji mkubwa kuliko kawaida wa
tezi hiyo katika mwili ni dalili kwamba mwanamke husika ana tatizo liitwalo
‘Polycystic ovary syndrome’, tatizo ambalo hupelekea mwanamke kushindwa kushika
ujauzito.
Yapo
matatizo mbalimbali ya ovari (Ovarian disorder) ikiwa ni pamoja na makovu
(cysts), tumor, maambukizi, na maradhi yanayoathiri uzazi. Baadhi ya wanawake
hupatwa na tatizo la kushika ujauzito kutokana na mifuko yao ya uzazi (ovari)
kushindwa kufanya kazi kutokana na upasuaji (surgery), majeraha waliyowahi
kupata (injury), mionzi (radiation) au matatizo ya kibaolojia (chromosomal
problems), kuishiwa mayai mapema na kupelekea kuingia katika hali ya kukoma
kuzaa (menopause) kabla ya wakati. Katika hali ya nadra sana baadhi ya wanawake
huzaliwa wakiwa hawana mifuko ya uzazi (ovaries) au kutokuwa na mayai ya
kutosha. Mimba ya mtoto wa jinsia ya kike ikifikia miezi mitano mtoto huyo wa
kike huwa na mayai ya uzazi katika kifuko chake cha mayai (fetal ovaries) zaidi
ya milioni 7. Mtoto huyo akizaliwa na kufikia umri wa kubalehe mayai hayo huwa
mengine yameungana na kufanya idadi ya mayai kupungua hadi laki 3.
Kadhalika
mapungufu ya mji wa mimba (uterus) pia huweza kusababisha mwanamke kushindwa
kushika mimba. Katika hali ya kawaida ya mchakato wa uzazi homoni za
progesterone na luteinizing hormone (LH) huchochea kuta za mji wa mimba
kuongezeka unene (uterine lining thickening) ili kuwezesha yai lililorutubishwa
kujishikiza kwenye kuta. Endapo mji wa mimba (uterus) hauna maelewano na homoni
hizo hali hiyo hupelekea yai kushindwa kujishikiza na hatima yake ni mimba
kutoka (spontaneous abortion or miscarriage). Wanawake wengine wana miji ya
mimba isiyokuwa na maumbile kamilifu (structurally abnormal) na wengine hawana
kabisa miji ya mimba, hali hizi zote husababisha kutokushika ujauzito.
Magonjwa
ya ngono (Sexually transmitted diseases – STDs) kama vile gonorrhea, Chlamydia
na Pelvic inflammatory disease (PID) huathiri hali ya wanawake kushika
ujauzito. Maambukizi haya huweza kudumu katika miili ya wanawake kwa kipindi
kirefu bila wahusika kujitambua hali ambayo huweza kusababisha makovu kwenye
mji wa mimba (scar), kuziba kwa milija ya uzazi (block fallopian tubes) na
kusabisha ‘formation of pelvic adhesions’. Kadhalika maambukizi ya mara kwa
mara ya fangasi (yeast infections) kitalaam ‘Vaginitis’ huweza kuharibu milija
ya uzazi hivyo mbegu za kiume kushindwa kupenya ili zikarutubishe yai. Matatizo
mengine yanayoweza kupelekea milija kuziba ni pamoja na upasuaji wa tumbo au
nyonga (Abnominal or pelvic surgery), Appendicitis, Endometriosis, Ectopic
pregnancies au matumizi ya vifaa vya uzazi wa mpango (IUD contraceptive
device). Matumizi ya vidonge vya majira husababisha ugumba wa muda (temporary
infertility) kwa kipindi cha hadi miezi sita.
Wanawake
wengi hawaelewi kwamba lishe, viini lishe (nutrition) na mfumo wa maisha
kuchangia tatizo la ugumba. Mazoezi makali (Excessive exercises), ‘low –calorie
diet’, ulaji usifaa (eating disorder), fetma (Obesity), matumizi ya aina fulani
ya madawa, mawazo yaliyopitiliza kutokana na kuudhiwa (elevated stress levels)
na matumizi ya mafuta ya kulainisha uke (vaginal lubricants) pia huathiri mfumo
wa uzazi wa mwanamke. Cases nyingi za ugumba husababishwa na wanandoa kushindwa
kufanya timing ya siku za kujamiiana ili mwanamke kupata ujauzito. Katika mwaka
mzima (siku 365) mwanamke ana siku 26 tu za kutungishwa ujauzito. Siku zingine
zinaobaki yaani 339 ni siku potevu (waste days).
Tiba ya Lishe kwa Wanawake Katika Kutibu Ugumba.
Kuwa na Uzito Unaostahili Ili kupata
Ujauzito
Uzito wa mwili unaathiri
uwezo wa mwanamke kupata ujauzito. Kama una uzito mkubwa kuliko upasavyo kuwa
(Obese) seli za mafuta katika mwili huzalisha homoni nyingi ya estrogen ambayo
hukwaza uwezo wa kutunga mimba. Kiwango cha juu cha estrogen hupeleka ujumbe
kwenye ubongo kusitisha kuchochea development of follicles. Hali hiyo hufanya
kutokutokea kwa upevushaji wa mayai. Hali hii huwapata zaidi wanawake wenye
tatizo la ‘Polycystic ovary syndrome
(PCOS)’. Tafiti zimeonyesha kwamba
wanawake wenye uzito mkubwa (Obese) wakipunguza uzito wao kufikia kiwango
kinachotakiwa hali ya upevushaji wa yai hurudi tena na mwanamke kushika
ujauzito.
Mwanamke kuwa na uzito mdogo
kuliko kawaida mafuta mwilini ambayo ni muhimu kwa upevushaji wa mayai nayo
huwa katika kiasi kidogo na homoni zinazohusika na uzazi huathirika kiutendaji
kazi na matokeo yake ni mwanamke kuwa mgumba.
Matumizi ya Caffeine na Alcohol na Uvutaji
Sigara
Tafiti zimedhibitisha kwamba
utumiaji wa caffeine zaidi ya 300 milligrams kila siku (sawa na kinywaji cha
kahawa vikombe 2) husababisha uchelewaji wa mwanamke kutunga ujauzito. Utafiti
uliofanywa katika Chuo Kikuu cha Johns Hopkins kuhusu wanawake waliotumia
caffeine zaidi ya 300 milligrams dhidi ya wale waliotumia caffeine chini ya
kiwango hicho. Matokeo yalibainisha kwamba utungaji mimba kwa mwezi kwa
wanawake waliotumia caffeine zaidi ya 300milligrams kwa siku ulipungua kwa
asilimia 25.
Utafiti uliofanywa katika
Chuo cha Harvard School of Public Health
walifanya utafiti kwa wanawake zaidi ya 4000 waliotumia alcohol na kubaini
kwamba wanawake waliotumia kilevi kiasi cha chupa mbili kwa siku waliathiri
uwezo wao wa kupata ujauzito kuliko wale ambao hawakuwa wakitumia kabisa pombe.
Ndio kusema kwamba kadiri mwanamke anavyotumia kilevi zaidi ndivyo tatizo
linazidi kuwa kubwa.
Tafiti zimethibitisha kwamba
wanawake wanaovuta sigara huku wakijaribu kupata ujauzito huchelewa kupata
ujauzito. Kadhalika uvutaji sigara kwa wanawake huathiri afya na utendaji kazi
wa ovari na kufanya uharibifu kwenye mayai ya uzazi na kuathiri homoni ya kike
ya estrogen. Hivyo wanawake wanaotaka kutunga ujauzito na huku ni watumiaji wa
sigara wanashauriwa kuacha uvutaji wa sigara.
Vitamin B12.
Upungufu wa Vitamin B12 kwa
mwanamke husababisha tatizo la kupata ujauzito. Wanawake walio katika umri wa
kutunga mimba wanapaswa kutumia 2.4 micrograms za vitamin B12 kila siku. Aina
hiyo ya vitamin hupatikana kwenye vyakula vitokanavyo na wanyama (animal foods)
au kwa kutumia vidonge vya vitamin mbalimbali (Vitamin B complex).
Vyakula vilivyo na vitamin
B12 ni pamoja na nyama, kuku, samaki, bidhaa za maziwa, mayai, soya na maziwa
ya mchele (rice milk).
Tiba Mbadala (Herbal Remedies)
Chasteberry ni mmea tiba
muhimu kwa wanawake kwa masuala mbalimbali yahusuyo uzazi. Mmea huo hutibu
pamoja na matatizo mengine, kukosa mzunguko wa siku za hedhi ( Absence of
menstrual periods – Amenorrhea), kutokuwiana kwa homoni (hormones imbalance),
menstrual irregularities, na lower excessive level of prolactin. Nchini
Ujerumani mmea huo uliweza kutibu wanawake 10 kati 15 waliokuwa na tatizo la
kutokupata siku za hedhi. Mwanamke mwenye matatizo ya hayo hapo juu anashauriwa
kutumia 175-225 milligrams kwa siku. Tiba hii haileti matokeo ya mara moja kwa
haraka bali huchukua takriban miezi 5-7 kuona matokeo ya tiba. Aidha kwa
mwanamke ambaye amekosa siku zake kwa kipindi cha zaidi ya miaka miwili
itamchukua miezi 18 kuona matokeo chanya ya tiba hiyo. Mara tu baada ya kupata
ujauzito mwanamke anapaswa kuacha kutumia tiba hii.
No comments:
Post a Comment