Hii ni sehemu ya mwisho ya mada kuhusu namna ya kuondokana na tatizo la Fetma (obesity). ukifanya mambo niliyoyaeleza kwenye part 1 hadi part 3 ambayo ndio hii unayoisoma hakika utaondokana na tatizo la unene hata kama tatizo hilo limekuwa sugu licha ya kufanya jitihada mbalimbali za kuliondoa. Sasa endelea....
Chakula au Juisi ya Kukata Tatizo
la Hamu/Uchu wa Vyakula
Ipo njia moja tu ya kuondokana kabisa
na tatizo la hamu au uchu wa vyakula ambayo ni kuondoa taka za asidi mwilini
kwa kuufanya mwili uwe na alkali yaani ‘to alkalize your body to eliminate food
cravings’. Unapaswa ufuate hatua mbili ili kuondokana kabisa na tatizo la uchu
wa vyakula, moja ni kuchagua aina ya vyakula kulingana na uwezo wa mwili wako
kuyeyusha vyakula hivyo (customize your diet to your own digestive metabolism).
Hatua ya pili ni jenga tabia ya ku-alkalize mwili wako mara kwa mara kwa
kutumia mlo wa viazi vyeupe (white potatoes). Ipo aina tatu za milo ya viazi
ambayo nitaileza na jinsi ya kuiandaa. Kila aina ya mlo wa viazi vyeupe una
tofautiana kidogo na aina nyingine kwa upande wa manufaa ya kiafya na pia
hutofautiana kwa muda/kipindi mpaka manufaa yake kuonekana.
- Viazi
vilivyoiva Nusu (Semi-Raw Potatoes)
Manufaa ya aina hii ya mlo wa viazi ni ya muda
mrefu. Unahitaji kutumia mlo huu kila siku kwa kipindi cha miezi 2 hadi mitano
ili kufikia utatuzi wa tatizo la uchu wa chakula au kupunguza tatizo la kupatwa
njaa mara kwa mara. Lakini pia mlo huu hutibu tatizo la gesi au kiungulia ndani
ya kipindi cha wiki chache tu. Kwa watu wenye tatizo la kupatwa na asidi (acid
reflux) huu ni mlo mzuri kwao kwani huyeyushwa vizuri mwilini.
Namna ya
kuandaa: kata viazi
(potatoes) katika vipande vidogo vidogo, ikiwezekana usivimenye maganda yake.
Weka kwenye chombo cha kupikia. Weka maji lakini yasifunike viazi. Pika kwa
kutumia moto usio mkali taratibu mpaka vianze kuwa laini lakini visiive mpaka
ndani. Kisha ipua. Kula viazi na kunywa maji uliyopikia. Usiyamwage hayo maji.
- Grated
Potatoes
Hapa ni kwamba viazi vinakuwa kama vinasagwa au katwakatwa
katika vipande vidogo vidogo kama ambavyo karoti husagwa. Vipande vipande hivyo
vya viazi vina mucilage nyingi na husaidia kukata hamu ya vyakula ndani ya siku
tatu au nne.
Namna ya
kuandaa: Menya viazi kuondoa
maganda yake. Hii hufanya viazi kuachilia mucilage nyingi zaidi. Kisha baada ya
kuvimenya visage kwa kutumia kifaa cha kusagia (grate the potatoes). Kusaga
viazi hufungua fiber za viazi kiasi kwamba joto wakati wa kuvipika hufanya
mucilage kuachiliwa zaidi. Weka vipande vya viazi kwenye ‘an 8-inch frying
pan’. Weka maji lakini usifunike viazi hivyo. Funika. Pika kwa joto la juu
kidogo na pale maji yakianza kuchemka subiri dakika 2-3 kisha punguza joto
(medium to low). Endelea kupika kwa dakika zingine 5-10. Mara nyingine
itakulazimu kuwa unaongeza maji kidogo kidogo hadi viazi viive. Kwa aina hii ya
mlo, viazi huiva kabisa. Lengo sio kutunza (preserve) vimeng’enywa (enzymes) na
vitamin bali lengo ni kupata mucilage nyingi zaidi kadri iwezekanavyo kutoka
kwenye viazi.
Namna ingine ya kuandaa mlo huu: menya kiazi
kimoja kikubwa na kikate/kisage (grate). Weka siagi (butter) vijiko vidogo
vitatu kwenye kikaango (frying pan) na weka kwenye moto hadi iyeyuke. Weka
vipande vya viazi kwenye kikaango. Pika kwa joto la wastani kwa dakika 3 – 4.
Punguza moto na endelea kupika kwa dakika zingine 4 hadi viazi viwe laini.
- Alkalizing
Potato Water
Kunywa maji ya viazi gasi moja au mbili kila siku.
Ukitumia maji hayo kwa miezi miwili au mitatu mfululizo tatizo la njaa
iliyopitiliza (excessive hunger) litatoweka.
Namna ya
Kuandaa: Kata viazi viwili vikiwa
na maganda yake katika vipande (Slices) na weka kwenye chombo cha kupikia. Weka
maji hadi kuvifunika viazi. Chemsha vizi kisha viipue ila usiviondoe kwenye
maji mpaka baada ya dakika 15. Mimina maji ya viazi kwenye chombo kingine.
Viazi unaweza kuvitupa au kuvila maana nutrients tayari zimeondolewa kwenye
hivyo viazi na ziko kwenye maji ya viazi.
Dondoo:
Ulaji wa kipande cha kiazi kibichi kabla ya kula
chakula kinacholetea tatizo la gesi au asidi tumboni (hyperacidity) kutasaidia
kukuepusha na tatizo la uyeyushaji chakula tumboni (indigestation).
Kula kipande cha kiazi kibichi baada ya kuwa
umepatwa na tatizo la gesi (acid reflux) kutasaidia kuondoa tatizo hilo katika
mfumo wa mwili wako unahusika na usagaji na uyeyushaji wa chakula.
Ulaji wa kipande cha kiazi baada ya kunywa chai au
kahawa husaidia kukata asidi kinywani.
Aina ya milo ya viazi ambaye nimeieleza hapo awali
inasaidia sio tu kukabiliana na tatizo la asidi inayopelekea mataizo ya uzito
ulizidi au utapiamlo (obesity) bali pia kukabiliana na matatizo yatokanayo na
mfumo wa chakula (digestive disorders) kama vile vidonda vya tumbo (ulcers),
colitis, diverticultis na Crohn’s disease.
Mimea, matunda na juisi kwa ajili
ya tiba ya tatizo la uzito wa mwili
Pamoja na maelezo niliyokwisha kueleza
kuhusu suala hili la uzito au unene kupindukia napenda pia nikueleweshe baadhi
ya mimea, matunda na juisi kwa tatizo hilo kama ifuatavyo:
- Parachichi
(Avocado). Husaidia
kupunguza rehamu (cholesterol) mwilini na kuzuia uharibufu wa ini (liver
damage preventative). Kula tunda moja au mawili kila siku.
- Ndizi
(banana). Hupunguza
tatizo la kuongezeka uzito, kukosa choo na vidonda vya tumbo. Kula ndizi mbivu
kila siku.
- Iliki
(Ginger root). Hutibu
tatizo la kukosa hamu ya kula na tatizo la kutofanya kazi ipasavyo kwa
mfumo wa uyeyushaji chakula mwilini. Itumie kama chai na pia weka kwenye
chakula unachokula kama kiungo (spice).
- Zabibu
(Grapes). Hupunguza unene
na kuimarisha afya ya mwili. Tengeneza juisi ya zabibu na itumie kutwa
nzima huku ukiwa umefunga kula chakula na pia unapaswa kunywa maji glasi
4-5 wakati ukiwa kwenye mfungo huo. Fanya hivyo siku moja kwa wiki na siku
6 zingine kula mlo kamili (balanced meals).
Juisi ya zabibu pia husaidia kutibu magonjwa ya
moyo (Heart diseases), kiharusi (strokes) na shambulizi la moyo (heart attacks)
na kuziba kwa mishipa ya damu (Arteries anti-clotting). Kwa tiba ya magonjwa
hayo kunywa glasi moja ya juisi hiyo iliyotengenezwa kwa zabibu nyekundu (red
grapes). Ili kuongeza kasi ya matibabu ya matatizo hayo kula saladi
iliyonyunyizwa mafuta ya mizeituni (olive oils) na kunywa juisi ya zabibu
nyekundu.
- Kiwi
(kiwifruit). Hutibu
tatizo la kukosa choo (constipation and bowel movements). Ulaji wa matunda
2-4 yakiwa na maganda yake hupelekea kupata choo katika kipindi cha ndani
ya masaa 24.
- Linseed: hutibu tatizo la kukosa choo.
Saga mbegu za linseed kufanya unga. Asubuhi kabla ya kula chakula chochote
kunywa maji glasi moja yaliyowekwa unga wa linseed kijiko kimoja cha
chakula. Vivyo hivyo kunywa glasi mija ya maji yenye linseed saa moja
baada ya kula chakula (main meal).
- Mapesheni
(passionfruit). Hutibu
tatizo la kukosa choo, kutuliza akili (calming effect) na kuzuia
maambukizi ya njia ya mkojo (Urinary tract infections –UTI). Kula matunda
2-3 pamoja na mbegu/nyama zake za ndani kila siku.
Unywaji wa juisi iliyotengenezwa kwa mchanganyiko
wa mapesheni 2, chungwa moja na vipande viwili vya tikiti maji, asubuhi kabla
ya kula chochote ni kinywaji safi kwa kuimarisha afya ya mwili wako.
- Prunes. Hutibu tatizo la kukosa choo na
hupunguza rehamu mwilini. Kula fresh prunes asubuhi kabla hujala chochote
na masaa mawili baada ya kula chakula cha usiku. Ukikosa fresh prunes
nunua prunes zilizokaushwa (hupatikana supermarkets) na ziloweke kwenye
maji hadi zilainike na zile.
- Tikiti
(watermelon). Husaidia
kupata choo na pia huzuia uharibufu wa ini (liver damage preventative).
Kunywa glasi moja ya juisi asubuhi nusu saa kabla hujala chakula chochote.
- Juisi ya kupunguza uzito iitwayo
‘Thai Tango’. Weka kwa pamoja
kwenye blender: papai lililomenywa gramu 100, pears mawili yaliyomenywa na
kukatwa vipande, juisi ya ndimu moja, maji ya mchele (rice milk) 200ml na
unga kidogo wa iliki. Blend pamoja kutengeneza juisi.
No comments:
Post a Comment