Tuesday 1 September 2015

Zitambue Faida ya Embe Katka Kutibu Magonjwa


EMBE ni tunda la mwembe ambao ni mti wenye ukubwa wa wastani na una rangi ya kijani kibichi kila wakati. Kabla ya kuzaliwa embe mti huu huwa na maua ya rangi ya waridi hadi nyeupe katika vishada vya maua na msimu wake ni kati ya Desemba hadi Aprili.

 Tunda la embe umbo lake hutofautiana, mengi yao huwa na rangi ya kijani, manjano ama nyekundu. Embe inaweza kuiva ikiwa mtini lakini ili kuzuia uharibifu kutoka kwa ndege na popo ambao hula tunda hili, wakulima huamua huvuna mara tu inapokomaa kwa kuangusha ikiwa bado haijaiva. 
Utagundua kuwa embe imekomaa kwa kuiangalia rangi kwani hubadilika kutoka rangi ya kijani hadi ya manjano au nyekundu.
Kuna aina nyingi za embe kama vile embe dodo, embe mali, embe bolibo,  embe nuka,  embe kidney, embe Julie Manzano na  kadhalika.
Watu wengi hupenda kula embe ikiwa imeiva lakini ulaji wake ikiwa bado mbichi ni jambo muhimu sana kiafya.
Nyama ya tunda hili ni tamu pia ina virutubisho kwani ni  chanzo cha upatikanaji wa vitamini A na C mwilini mwa binadamu.
Embe ina kiasi cha wastani cha thiamin na niacin na asilimia 10 hadi 20 ya sukari inayosaidia mwili iwapo mtu anakula tunda hili.
Maembe pia yanaweza kugandishwa, kukaushwa kwa jua na kuweza kutumika siku nyingi zijazo.
Maembe pia yanaweza kuwekwa kwenye makopo viwandani ama kupikwa katika jemu na watu kutumia baada ya muda fulani.
Lakini embe pia hutumika kutengeneza jeli,  pai, achari kama Mango pickle ambayo hupendwa na watu wengi na kwa hakika huwa ghali kutokana na tunda lenyewe kupendwa na watu.
Kuna watengenezaji wa aiskrimu huamua kutumia tunda hili kutengeneza na wengi hupenda kutumia kutokana na harufu yake nzuri.
Watu wengi hutumia tunda hili kutengeneza juisi ama ikiwa yenyewe tu au kwa kuchanganya na matunda mengine. 
Matunda ambayo hutumika kuchanganya na embe ni ndizi, nanasi, parachichi, zabibu, papai na kadhalika.
Kuna wengine hutumia mchanganyiko huo kwa kula bila kusagwa na wengine huamua kusaga na kugeuza kuwa juisi ambayo inaweza kutumika bila kuongeza sukari kwa kuwa matunda hayo yote yana sukari ndani yake.

Baada ya kuangalia manufaa ya kiafya ya tunda la embe katika mwili wa binadamu, sasa hebu tuangalie manufaa ya tunda la embe kama tiba kwa magonjwa mbalimbali katika mwili wa binadamu.
Kuvimba kwa Wengu( Spleen enlargement): Changanya asali kijiko kimoja kwenye utomvu wa embe bivu kiasi cha kikombe cha kunywea chai. Tumia mara tatu kwa siku.
Matatizo ya Ini na Tatizo la Uyeyushaji wa chakula (Indigation): Fyonza embe lililoiva na ukimaliza kunywa maziwa glasi moja.
Kipara (Baldness): Paka kwenye kipara kijiko kimoja cha mafuta ambayo yaliwekwa vipande vya maembe mabichi na kuhifadhiwa kwa kipindi cha mwaka mmoja au zaidi yaani kwa kimombo ‘oil in which raw mangoes have been preserved for over one year’.
Kuepusha Ugonjwa wa Saratani: Kula embe moja au juisi ya embe nusu glasi au glasi moja kila siku asubuhi mara baada ya kula chakula cha kifungua kinywa (breakfast).
Kutibu Tatizo la Upungufu wa Madini ya Calcium Mwilini: Kunywa juisi ya embe (fresh juice) dakika tano kila siku baada ya kifungua kinywa.
Kutibu Vidonda Mdomoni na Kooni, Maumivu ya Meno na Tatizo la Harufu Mbaya ya Kinywa: Pondaponda majani ya mti wa mwembe na weka maji. Uwe ukisukutua kinywa kwa maji hayo.
Kuhara (Diarrhoea), Vidonda vya Tumbo (Ulcers): Saga hadi kuwa unga laini gome la mti wa mwembe. Uwe unachukua unga huo kiasi cha nusu au kijiko kimoja na weka kwenye maji ya kunywa. Uwe unakunywa kulingana na uhitaji wako.


No comments:

Post a Comment