Tunda la papai lina vitamini C na E likiwa
na siri kubwa ya urembo na hutumika
kutengeneza facial za aina mbalimbali. Papai limekuwa likitumiwa kama njia yenye gharama nafuu ya kutunza uso
wako na kumfanya mtu kuwa na ngozi
ya asili.
Bidhaa ambazo zimekuwa zikitengenezwa kwa kutumia tunda la papai ni pamoja na sabuni, lotion, tona, moisturizer, facial peels na nyingine nyingi. Ukitumia facial mask ya papai utakuwa na sura nzuri ya asili na kukupa uonekanaji mzuri wa uso wako. Facial mask hii huweza hutumika kwa watu wa umri wowote na aina yoyote ya ngozi.
Facial mask ya papai inasaidia ngozi ambayo imeshaanza kupatwa na makunyanzi kutokana na umri na pia hukufanya kuonekana mwenye ngozi ya kuvutia kwani huondoa chunusi na makunyanzi.
Ni rahisi kutengeneza facial mask ya papai na ukitumia itakusaidia katika kukabiliana na ngozi iliyoanza kuchoka, kung’arisha ngozi na ni njia nzuri za kuhakikisha kuwa tunakuwa na nyuso nzuri zenye kupendeza na kuvutia ikiwemo.
Mask ya mchanganyiko wa papai yai na yai ni nzuri katika kuhakikisha kuwa unakuwa na ngozi nzuri na nyororo. Njia hii pia husaidia hata wale wenye nyuso za mafuta ambao wamekuwa wakisumbuliwa na chunusi mara kwa mara kwa kufanya ngozi kuwa kavu.
Unaweza kutengeneza aina hii ya mask kwa kufanya yafuatayo:-
Chukua papai likate kisha toa mbegu na halafu lisage kwa kutumia blenda au kupondaponda kwenye kibakuli kwa kutumia kitu kama mchi mdogo wa kinu. Kisha weka mchanganyiko huo kwenye chombo ulichokichagua kama kikombe au bakuli. Vunja yai na koroga kuhakikisha kuwa mchanganyiko huo umechanganyika vizuri.
Safisha uso wako kwa kutumia cleanser au maji ya vuguvugu na uondoe uchafu wote ulioganda usoni. Kisha paka mask kuzunguka uso wako, na unapopaka hakikisha kuwa, mchanganyiko huo haugusi macho yako.
Osha uso wako baada ya dakika 15 kwa kutumia maji ya vuguvugu. Jifute kwa kutumia taulo safi. Unaweza kupaka losheni, tona au moisturizer.
No comments:
Post a Comment