Kichwa kinagonga, unaona kizunguzungu, mwili hauna nguvu, unasikia
kichefuchefu, kama unataka kutapika lakini hutapiki, kwa kifupi unajisikia
hovyo kufuatia unywaji wa kupindukia ulioufanya jana! Hali hii inaitwa HANGOVER
au uchovu wa ulevi.
Ingawa hatupendi kuelezwa ukweli au kufikiria madhara ya pombe, lakini ni ukweli ulio wazi kuwa pombe ni dawa ya kulevya. Ina dhoofisha mwili na pale mtu anapokunywa kupita kiasi, mwili hujawa na sumu. Unapokutana na hali hiyo, mwili hujaribu kujinasua kama vile ambavyo kitu chochote kingefanya kinapovamiwa na kitu kigeni.
Njia bora ya kuondokana na uchovu (hangover) ni kunywa kiasi au kuacha kabisa unywaji pombe. Kamwe dawa ya hangover sio kuzimua kwa pombe asubuhi ya siku nyingine! Kama utashindwa kujizuia kunywa pombe na unataka kuondoa uchovu wa ulevi wakati wa asubuhi, ni vyema utengeneza na kunywa mojawapo wa juisi zifuatazo:

1.
Sri lankan Soother
Blend kwa pamoja juisi ya balungi (grapefruit) 600ml (1 pint),
juisi ya ndimu vijiko viwili vidogo (2 teaspoons) na jira (cumin) kijiko kimoja
kidogo. Kunywa kabla na baada ya kunywa pombe. Juisi ya balungi na juisi ya
ndimu pamoja na kuupa mwili vitamins mbalimbali na fructose pia husaidia
kusafisha ini kwa maana ya kutoa na kuyeyusha sumu zitokanazo na pombe. Jira
husaidia uyeyushaji na kusaidia mwili kushughulikia sumu.
2.
Roman Relief
Blend pamoja juisi hizi: juisi ya baggage (250ml), juisi ya
figiri (celery) 250ml na unga wa majani ya coriander (vijiko vidogo viwili). Cabbage
ilikuwa mashuhuri kwa Warumi kama tiba ya kuzuia kulewa na hangover. Cabbage ina
glutamine ambayo hukinga ini dhidi ya madhara ya alcohol. Figiri na coriander
husaidia kupunguza madhara ya alcohol mwilini.
3.
Elizabethan rosemary and
Lemon syrup
Viambata (Ingredients) utakazotumia: Juisi ya limao moja,
maji ya moto (600ml), majani ya rosemary yaliyoshindiliwa kiasi kwenye jagi la
kupimia (measuring jug) na kujaa hadi 600ml na sukari 450g. weka majani ya
rosemary kwenye sufuria (pot) na miminia maji ya moto. Funika na acha kwa muda
wa dakika 10. Chuja kwa kugandamiza hayo majani na weka maji uliyochuja kwenye
chombo kingine. Weka juisi ya limao na sukari. Weka kwenye moto na endelea
kupasha huku ukikoroga sukari hadi iyeyuke kabisa. Baada ya hapo ipua na acha
ipoe. Kisha weka kwenye chupa na funika na kizibo chake. Tumia hiyo tiba vijiko
vikubwa (tablespoon)1-2 hadi hangover ikome.
Katika karne ya 17 Rosemary ilikuwa ikiuzwa kama tiba ya
hangover. Husaidia kuondoa sumu kwenye ini. Limao ni tunda zuri kwa ini and
huupa mwili vitamin C
No comments:
Post a Comment