Ni tatizo linalotokana na
kuvimba kwa tonsils. Katika miili yetu tonsils husaidia katika mambo mawili.
Moja, kukinga koo dhidi ya mashambulizi ya vijidudu na maambukizi ya magonjwa.
Pili, tonsils zinapovimba ni kiashiria cha maambukizi katika sehemu fulani ya
mwili.
Chanzo kikuu cha tonsillitis
ni uchafu au sumu taka katika mwili ambazo zimeshindwa kutoka mwilini kwa njia
ya kawaida ya mwili kutoa uchafu mwilini kama vile njia ya figo (mkojo), njia
ya ngozi (jasho) na njia ya haja kubwa. Tatizo hilo linaweza kuwa kubwa zaidi
pale ulikuwa na tatizo kubwa la kutopata choo na matokeo yake uchafu ulipokaa
muda mrefu kwenye utumbo mpana,ukafyonzwa kwenye nfumo wa damu.
Matibabu kwa njia za madawa
ya kisasa ni kama huwa zinatibu maua ya tatizo lakini hazing’oi mzizi wa tatizo
hilo. Ndio maana baadhi ya watu wamekuwa wakirudiwa na tatizo hilo mara baada
ya siku kadhaa. Njia bora ya kutibu tatizo hilo ni kusafisha uchafu mwilini kwa
njia za asili na ulaji wa lishe bora (balanced diet). Kwa kuanza funga kula
chakula kwa siku tatu hadi tano huku ukitumia maji na juisi ya machungwa.
Katika kipindi hicho cha ufungaji kula dalili za tonsillitis kama maumivu ya
koo zitatoweka. Katika kipindi hicho kunywa maji ya vuguvugu kiasi cha kutosha
ili kusafisha utumbo mpana. Pia katika kipindi hicho cha mfungo kama utaweza
unakuwa unaweka kitu cha baridi kama
vile barafu chini ya koo kwa interval ya
masaa mawili.
Kadhalika katika kipindi hicho
utakuwa unasukutua koo kwa juisi ya limau. Kama utaweza kupata fenugreek seeds
ni nzuri zaidi kama mbadala wa juisi ya limau. Mbegu hizo unaweza kuzipata
supermarkets kama una access hiyo. Unaweka mbegu hizo kiasi cha vijiko viwili
vya chakula (2 table spoons) kwenye lita moja ya maji kisha unatokosa kwenye
moto kwa nusu saa. Kisha ipua na kuacha yapoe. Utakuwa unasukutua koo kwa maji
hayo. Ni nzuri sana badala ya limau.
Baada ya dalili za
tonsillitis kukoma kula mlo wa matunda yenye majimaji (juicy fruits) tu kwa
siku kama tatu au nne. Matunda hayo ni kama machungwa, mabalungi, pears,
matikiti, zabibu, nanasi, nk. Nanasi ni zuri sana kwa tatizo hilo la
tonsillitis. Baada ya hapo sasa ndipo uanze kula balanced diet. Kwa maana ya
mlo wenye aina zote muhimu za vyakula yaani matunda, mboga za majani, whole
grains and nuts, etc.
Aidha kipindi cha matibabu
kila baada ya siku moja oga maji vuguvugu yenye Epsom salt (Hot Epsom Salt
Bath). Epsom salt utaipata supermarkets. Unakuwa unaweka kiasi kwenye maji
vuguvugu ya kuoga. Ukipona unaweza kuwa unaoga maji ya jinsi hiyo mara moja au
mbili kwa wiki.
Hivyo ndivyo utaweza kutibu
tatizo la Tonsillitis na ukawa mzima bila kusumbuliwa na tatizo hilo mara kwa
mara. Upasuaji wa hospitalini kwa ajili ya kuondoa tonsils ni muhimu kwa nadra
hasa pale hali imekuwa mbaya kiasi cha kuanza kuotwa na vipele vyenye usaha
kooni.
Mwisho nakushauri kutumia
juisi tiba hii: changanya juisi ya karoti, juisi ya viazisukari (beet) na juisi
ya tango (cucumber) katika ratio ya 10:3:3 kwa kufuatisha mpangilio huo wa
juisi hizo. Au juisi ya karoti na spinachi kwa ratio ya 5:3 kwa kufuata
mpangilio huo.
No comments:
Post a Comment