Saturday, 8 August 2015

Zifahamu Nutrients na madini muhimu kwa Nguvu za Kiume



Siku hizi wanaume wengi wamekumbwa na tatizo la ukosefu wa nguvu za kiume kwa maana ya kutokuwa na uwezo wa kusimamisha uume wakati wa kufanya mapenzi, kushindwa kuendelea kusimamisha hadi mwisho wa tendo na kushindwa kurudia tendo hadi kuwaridhisha wenzi wao. Kadhalika wengine wamekuwa na tatizo la mbegu zao za kiume kutokuwa na umbile bora (sperm abnormalities) linaloziwezesha kusafiri kwa kasi ya kutosha katika uke wa mwanamke (sperm motility). Aidha wengine shahawa zao zina mbegu kidogo (low sperm count). Mwanaume anapomwaga shahawa wakati wa kufanya mapenzi shahawa hizo hupaswa kuwa na mbegu za kiume kiasi cha milioni 50 kwa kila milimita moja ya shahawa. Endapo kiasi hicho kitapungua chini ya miioni 20 uwezo wa uzazi (fertility) wa mwanaume huwa na kasoro. Matatizo yote hayo yanatokana na wanaunaume wengi kutokula vyakula sahihi au ulaji wa vyakula hivyo kwa kiwango kidogo ikilinganishwa na mahitaji ya mwili (Recommended Daily intake).


Tunaweza kupima ukweli kwamba matatizo hayo yapo kwa kiwango kikubwa kwa wingi wa matangazo ya madaktari na waganga wa tiba za asili au tiba mbadala yanayotolewa kwenye magazeti na mabango katika vituo vya magari au daladala na njia mbalimbali katika maeneo ya mijini. Swali la kujiuliza mababu zetu mbona hawakuwa na matatizo haya? Mbona walioa wake wengi na walimudu kuwatimizia haja zao za kimapenzi na walizaa watoto wengi? Nini kimesababisha jamii yetu imekumbwa na matatizo hayo? Jibu la maswali hayo ni rahisi sana! Tumeondoka kwenye mfumo wa asili wa ulaji vyakula vya asili na tumeingia kwenye mfumo wa ulaji vyakula visivyo vya asili au vilivyoondolewa uasili wake.
Sasa tuangalie viinilishe (nutrients) na madini yanayohitajika katika mwili wa mwanaume ili mwanaume huyo awe lijali na mwenye nguvu za kiume za kutosha.  

  1. Antioxidant Nutrients
Upungufu wa vitamin E, vitamin C na selenium huwa na athari kwenye uzalishaji na uogeleaji wa shahawa (sperm motility). Tafiti zimeweza kuonyesha kwamba vitamin E kiasi cha vipimo vya kimataifa (International Units - IU) 100-200 kwa siku huboresha afya ya shahawa za mwanume asiyeweza kumzalisha mwanamke (infertile man) na kumwongezea uwezekano wa kumtia mimba mwanamke. Kadhalika vitamin C huongeza wingi wa mbegu za kiume kwenye shahawa (sperm count) na uwezo wa shahawa kuogelea ndani ya uke wa mwanamke (sperm motility). Tafiti pia zimeonyesha kwamba selenium husaidia uogeleaji wa shahawa.
Mahitaji (Recommended Dietary Allowances – RDA) ya vitamin C ni miligramu 90. Mwanaume anayevuta sigara anahitaji miligramu 125. Vyakula vyenye vitamin C ni pamoja na matunda jamii ya machungwa (citrus fruits), cantaloupe, kiwi, maembe, strawberries, broccoli, cauliflower, pilipili nyekundu na juisi ya nyanya. Vitamin E RDA ni 15 IU (natural source) na 22 (synthetic). Vyakula muhimu ni pamoja na ngano, karanga na jamii zake, mafuta ya mimea, mbegu zisizokobolewa (whole grains). Selenium RDA ni 15 micrograms. Vyakula muhimu vyenye selenium ni pamoja na samaki, seafood, kuku, organ meats, whole grains, karanga na jamii zake (nuts), vitunguu, uyoga, vitunguu swaumu.

  1. Vitamin B12
Upungufu wa vitamin B12 hupelekea lower sperm counts na impaired sperm motility. Vyakula muhimu vyenye B12 ni pamoja na nyama, kuku, samaki, maziwa na bidhaa zake, mayai, soya na maziwa ya mchele (rice milk).

  1. Zinc
Madini ya zinc ni muhimu sana kwa masuala ya uzazi na uzalishaji wa shahawa. Wanaume wenye matatizo ya uzazi wana upungufu wa madini ya zinc. Upungufu wa madini hayo pia hupelekea wanaume kuwa na kiasi kidogo cha homoni za kiume (low testosterone levels). Wanaume wenye shida hiyo wakipewa madini ya zinc huwa na ongezeko la mbegu za kiume (increased sperm counts) na uwezo wa kutia mimba. RDA ya zinc ni miligramu 11 kwa siku (wanawake huitaji miligramu 8). Vyakula muhimu ni pamoja na pweza na chaza, dark turkey meat, lentils, ricotta cheese, tofu, yogurt, spinach, broccoli, green beans, na juisi ya nyanya. Hakikisha kwamba pamoja na madini ya zinc pia unapata madini ya copper kiasi cha miligramu moja kwa siku kwa kuwa madini hayo hufanya kazi kwa pamoja kwa kutegemeana.

  1. L-carnitine  

Husaidia kuongeza sperm count. Utafiti mmoja uliofanywa ulibainisha kwamba gramu 3 kwa siku za L-carnitine kila siku kwa muda wa miezi mitatu uli-saidia kuongeza sperm count na sperm motility kwa wanaume 37 kati ya 47. L-carnitine hupatikana kwenye nyama na maziwa.

No comments:

Post a Comment