Monday, 27 July 2015

Urembo wa Ngozi: Fanya Haya Ili Ngozi Yako Ionekane Maridadi na Yenye Mng’aro!






Ngozi ni kiungo ambacho hutenganisha viungo vya ndani vya miili yetu na mazingira yanayotuzunguka popote pale tuwapo yaani ‘interface with the world’. Ngozi ni kiungo kikubwa zaidi ya viungo vingine katika miili yetu ambayo ina uzito kati ya paundi 7 hadi 10 na ina ukubwa wa futi za mraba takriban 20. Kadhalika kwenye ngozi kama kiungo mojawapo cha mfumo wa fahamu ina ‘nerve endings’ kuliko viungo vingine katika miili yetu isipokuwa ubongo tu. Ngozi hufunika na kulinda viungo vya ndani vya mwili na kuvifanya muda wote viwe safi.
Ngozi ni kioo cha hali ya afya zetu. Huzuni, kukosa usingizi, na furaha, vyote hujionesha kwenye ngozi zetu. Aidha ngozi inafanya kazi tatu, ni kiungo cha mfumo wa fahamu, ni kiungo kinachotoa uchafu mwilini kama jasho na ni kiungo kinachorekebisha (regulate) joto la mwili. Watalaamu wa masuala ya afya pia wamekuwa wakiita ngozi kama pafu la tatu (third lung). Asilimi 2 ya hewa ya oksijeni huingia mwilini kupitia ngozi. Na uchafu kama vile jasho hutolewa mwilini kupitia ngozi.

Hivyo tunaona kwamba ngozi ina umuhimu mkubwa sana kwa binadamu. Umuhimu mwingine ni kwamba ngozi ya mwili wako inafanya sehemu kubwa ya urembo wa mwili wako. Watu wengi husan wanawake wamekuwa wakifanya jambo lolote wawezalo kufanya ili kuweka ngozi zao katika hali ya urembo. Hiyo ni pamoja na kutumia losheni, mafuta na cream za aina mbalimbali. Matumizi ya losheni, mafuta au cream haviwezi kufanya urembo wa asili wa ngozi na badala yake matumizi ya vifaa hivyo vimechangia matatizo na magonjwa ya ngozi kwa wanawake wengi.
Ili kujihakikishia kwa asilimia 100 unakuwa na ngozi nzuri inayokufanya upendeze fanya mambo yafuatayo:-
  1. Vaa nguo zenye nyuzi za asili (natural fibers) kama vile nguo za pamba na pia kila siku jipumzishe (relax) ukiwa uchi bila kuvaa nguo yoyote (air baths) kwa angalau dakika 10.
  2.  Fanya mazoezi ya viungo. Mazoezi husaidia kuingiza hewa mwilini na kupeleka nutrients za chakula kwenye seli za ngozi. Mazoezi huongeza joto juu ya ngozi ambalo hupelekea aina nyingi za bacteria wenye madhara kiafya kuuliwa.
  3.   Kula vyakula vinavyong’arisha ngozi. Vyakula hivyo ni pamoja na karoti, maboga (pumpkins), viazi vitamu, magimbi (yams), pamoja na apples, apricots, parachichi, mboga za majani kijani (green leafy vegetables), parsley, maharage ya soya, lentils, shayiri, na yogurt. Kula samaki wenye mafuta muhimu kwa ngozi. Samaki hao ni pamoja na dagaa, salmon, tuna, bluefish na monkfish. Katika saladi hakikisha unaweka pia mafuta ya mimea kama vile olive oil.
  4.  Kunywa maji glasi 8-10 kwa siku ili kusaidia kuondoa uchafu mwilini ambao inaweza kuziba njia ya jasho (pores). Kamua limao au ndimu kupata juisi kidogo ambayo unamimina kwenye maji hayo ya kunywa ili kusaidia damu kutembea vizuri mwilini hivyo kusambaza nutrients kwenda kwenye ngozi. Unaweza pia kuweka siki ya apple (apple cider vinegar) badala ya limao au ndimu.
  5.  Unywaji wa juisi ya mboga kama karoti, viazi sukari (beet), celery, spinach, parsley na tango ambayo umetengeneza mwenyewe  hupelekea ngozi kuwa na mng’aro angavu.
  6.  Kunywa maji ya shayiri (barley water) ili kung’arisha ngozi yako. Jinsi ya kuandaa maji hayo: chukua shayiri safi kikombe kimoja weka kwenye maji (glasi 8-10). Weka kwenye moto kwa muda wa masaa mawili, joto lisiwe kubwa na wala maji yasichemke. Baada ya hapo chuja na maji hayo utakunywa. Shayiri pia unaweza kuila.
  7.   Kuwa makini na matumizi ya vinywaji vyenye kulevya na vinywaji vyenye caffeine kama vile soda na kahawa kwa kuwa vinywaji hivyo vina tabia ya kupunguza maji mwilini (can dehydrate your skin).
  8.  Epuka ulaji wa mara kwa mara au ulaji mkubwa (overeating) wa baadhi ya vyakula ambavyo ukivila mwili unapata shida kuviyeyusha. Kwa maana kwamba mtu anapovila vyakula hivyo mwili hulazimika kupeleka damu nyingi zaidi kwenye tumbo ili kusaidia uyeyushaji chakula hicho. Hali hiyo hufanya sehemu zingine za mwili kukosa damu ya kutosha ambayo inasaidia kupeleka nutrients kwenye sehemu hizo. Vyakula hivyo ni pamoja na vyakula vilivyokaangwa kama chips, refined carbohydrates, vyakula vya bidhaa za ngano, nyanya, citrus fruits kama machungwa na mabalungi, chocolate, strawberries, karanga na siagi yake na vyakula vyenye mafuta mengi. 
  9.  Kama una tatizo la ngozi kuwa na makunyanzi au una pumu ya ngozi (eczema) tumia flaxseed oil. Au tumia unga wa flaxseed vijiko vikubwa (tablespoons) kila siku. Unga huo unaweza kunyunyizia kwenye cereal au kuweka kwenye yogurt na kunywa.
  






No comments:

Post a Comment