Showing posts with label Mapenzi. Show all posts
Showing posts with label Mapenzi. Show all posts

Friday, 25 December 2015

Unajua Madhara ya Dawa za Kusimamisha Uume Kwa Muda Mrefu?

bizarre potato stock photoKuna baashi ya wanaume wanatamani wakati wakiwa wanafanya mapenzi na wenzi au wapenzi wao basi mboo zao ziwe zinasimama muda mrefu mathalani masaa matatu au manne au zaidi huku wakimwaga shahawa eti tu wawaridhishe wenzi wao au ili waonekane ni wanaume waliokamilika. Wanaume wengine wamekuwa wakitumia dawa za kusimamisha mboo kama vile viagra au dawa za asili na zingine maarufu kama dawa za kimasai! Napenda nikwambie kwamba hizo dawa zina madhara makubwa kwa urijali wako na uko hatarini kuupoteza hata huo urijali mdogo uliosalia!



Kusimamisha mboo kwa muda mrefu na mara nyingine kiasi cha kufikia mboo inaanza kuuma kutokana na kusimama muda mrefu tayari ni ugonjwa. Kwa maneno rahisi ni kwamba umetumia dawa za kuongeza nguvu ili kuua nguvu chache ulizokuwa nazo. Kitalaamu hali hiyo ya mboo kusimama muda mrefu na kuuma inaitwa 'Priapism'. Priapism hutokea pale mboo inapopoteza uwezo wake wa kuondoa damu iliyoko kwenye mboo hiyo (ambayo hufanya isimame) ili isinyae (in order to become flaccid). Hiyo hali ikidumu kwa muda wa masaa manne husababisha seli za damu iliyoko kwenye mboo kukosa hewa ya oksijeni, hivyo kupelekea tishu katika mboo kufa. Na kadri hali hiyo inavyoendelea hupelekea damu kwenye mboo kuwa na asidi na hivyo kukosa uwezo wa kusafiri au kutembea kwenda sehemu zingine za mwili hususan kwenye moyo! Hapo hali inakuwa mbaya sana!

Kuna wanaume wengine wanaji-overdose viagra au madawa ya kienyeji ili wawe wanaume shababi kwelikweli kumbe ndio wanaua mboo zao. Ndio maana watu wanaotumia madawa hayo baada ya muda fulani hali zao za kiume zinakuwa mbaya zaidi afadhali ya jana! Ndio maana humu katika blog nimesisitiza sana matumizi ya vyakula na viungo kama tiba ya tatizo la ngivu za kiume! Siwashauri kutumia hayo madawa, otherwise, keep using them for your own risk!

Bahati mbaya au vyovyote vile kama umesimamisha mboo masaa kadhaa hakikisha katika kipindi cha ndani ya masaa manne tafuta tiba haraka kwa daktari! Wengine baada ya kutumia hayo madawa na mboo kusimama kama msumari masaa mengi wao hudhani dawa ni kufanya mapenzi masaa mengi na mwanamke ili kuondokana na hali hiyo! Tena wengine ndo hufurahia eti 'leo mwanamke fulani nitamfaidi kweli...'. My brother you are killing yourself'!!! Hutoweza kumkomoa mwanamke kwa kufanya mapenzi! Matibabu ya tatizo hilo ni kunyonya damu kwa kutumia sindano itakayochomwa kwenye mshipa wa damu uitwayo vein kwenye mboo yako! Mwisho nakushauri kula sana vyakula vya asili kama matunda na mboga za majani. Usisahau mazoezi ya viungo. Next time tutaona namna ya kukabiliana na tatizo la nguvu za kiume ingawa nimegusia gusia katika bloga hii katika mada kadhaa!

Monday, 7 September 2015

Mwanaume Ukitumia Aina Hii ya Chai Utakuwa Mwanaume Haswa!

Katika blogu hii nimetoa takriaban mada sita (06) zinazohusu vyakula na aina mbalimbali ya mazoezi ambayo mwanaume akizingatia hakika hatokuwa na tatizo la upungufu wa nguvu za kiume. Mada hizo ni pamoja na: Ongeza Nguvu za kiume kwa Viagra za Asili, Vyakula Vinavyoongeza Hamu na Nguvu ya Kufanya Tendo la Ndoa, Fahamu Aina 7 ya Vyakula Vinavyoongeza Nguvu za Kiume, Vijue Vyakula Hatari kwa Kupunguza Nguvu za Kiume, Fanya Mazoezi Haya kwa Wiki Tatu Kuongeza Nguvu za Kiume na Zifahamu Nutrients na Madini Muhimu kwa Nguvu za Kiume.

Leo nakuletea mada nzuri kuhusu namna ya kutengeneza chai ya viungo vya chakula ambayo mwanaume akiitumia atakuwa na hamu ya kufanya mapenzi na atakuwa na nguvu kubwa za kiume. Chai hii inaboresha shahawa za mwanaume kwa kiwango kikubwa kwa maana ya kuondoa tatizo la mbegu za kiume kuwa na umbo lisilofaa (sperm abnormalities), kuongeza wingi wa mbegu za kiume ndani ya shahawa (sperm count) na kuongeza kasi ya mbegu za kiume kuogelea ndani ya uke wa mwanamke (sperm motility). Chai hii itamfanya mwanaume kuwa rijali haswa kwani atakuwa na hamu kubwa ya kufanya mapenzi (libido), ataweza kuanza na kumaliza tendo bila kuishia njiani hali ambayo inawakera wanawake, inafanya uume kuwa mkubwa na inafanya uume kusimama haswaa kibabe na kufanya mashambulizi maridadi kunako sita kwa sita.

Kabla sijakueleza namna ya kuandaa chai hii napenda niwambie wanaume wenzangu kuwa matumizi ya chai na kahawa yenye caffeine sio nzuri kwao kwani huchangia kupunguza nguvu za kiume na kuzorotisha ubora wa shahawa. Wengi tumekuwa tukitumia chai au kahawa yenye caffeine bila kujua madhara yake kwetu wanaume. Watafiti nchini Italy waligundua kwamba hatari ya mwanaume kuwa na mbegu za kiume zisizo na ubora (unhealthy sperm) huongezeka kadri mwanaume huyo anapozidi kutumia chai au kahawa zaidi kwa siku. Hatari hii pia huwakumba wanaume wanao tumia kilevi (alcohol). Kadhalika wanaume wanaovuta sigara wanakabiliwa na hatari ya kupoteza ubora wa shahawa na upungufu wa mbegu za kiume. Aidha uwezo wao wa kufanya mapenzi (sexual performance) hupungua.

Bila kukuchosha kwa maelezo marefu napenda kukushauri wewe mwanaume kupunguza kabisa au kuachana na unywaji wa chai au kahawa yenye caffeine, uvutaji wa sigara na unywaji wa pombe usiofaa. Badala yake tumia chai hii ya viungo vya chakula. Ifanye iwe ndiyo chai yako kila siku asubuhi na jioni. Mimi binafsi nimeachana na chai au kahawa yenye caffeine. Natumia chai ya viungo na situmii sukari ya kawaida, natumia asali kwenye chai yangu ya viungo. Nimeona mafanikio makubwa sana na nimeona leo nishiriki pamoja na wewe siri ya mafanikio yangu.

Chai ya viungo, changanya viwango sawa vya unga wa viungo hivi: Tangawizi (ginger), kitunguu swaumu (garlic), unga wa haradali (mustard), pilipili manga, mdalasini, sweet basil, coriander na  kungumanga (nutmeg). Viungo hivi vinapatikana kwa urahisi sokoni au supermarket. Matumizi yake: chukua kiasi cha mchanganyiko wa viungo hivyo weka kwenye maji ya moto na weka asali badala ya sukari. Hata ukikosa sweet basil na coriander sio mbaya lakini hivyo viungo vingine ni MUHIMU SANA!


Ukitumia hii chai hutodanganywa na watu wanaonadi dawa za kuongeza nguvu za kiume, kuongeza hamu ya tendo au kurudia tendo na ubora wa shahawa kwa maana kwamba hutopoteza pesa yako kununua dawa zao! Isitoshe jiulize Je, hizo dawa au tiba zinazouzwa na watu hao ni salama? Zimehakikiwa na watalaamu wa Chakula na Dawa katika nchi unayoishi? 

Saturday, 29 August 2015

Vijue Vyakula Hatari kwa Kupunguza Nguvu za Kiume

Wanaume wanapaswa kufahamu aina ya vyakula ambavyo si rafiki kwao katika kuongeza kiwango cha homoni ya kiume iitwayo testosterone inayochochea sifa ya mwanaume yaani kuwa na nguvu za kiume. Baadhi ya vyakula visivyofaa kuliwa na mwanaume aliyetaka kuwa na nguvu za kiume ni vile vyenye asili ya homoni ya kike iitwayo estrogen. Hivyo sio kila vyakula vinafaa kwa mwanaume eti ilimradi tu vyakula hivyo vinasaidia kujenga mwili au kujaza tumbo wakati mtu akiwa na njaa.
Vyakula visivyofaa kabisa kuliwa na mwanaume kutokana na vyakula hivyo kupunguza homoni ya testosterone ni hivi vifuatavyo:

Mbegu za Flax (Flax seeds): 
vyakula vinavyotengenezwa kutokana na unga wa mbegu za flax vimekuwa vikisifiwa kwa kuwa Omega-3 fats ambayo ni muhimu katika miili yetu. Hata hivyo mbegu za flax ni mbegu maarufu kwa kuwa na estrogen ambayo ni sawa kabisa na homoni ya estrogen iliyoko katika miili ya wanawake. Flax seeds zina kiwango cha phytoestrogens mara tatu zaidi ya soya. Kama bado unafikiria kula vyakula vilivyo na mbegu za flax ili upate omega-3 achana na wazo hilo. Kama unataka kupata omega-3 kula samaki wenye mafuta mafuta (fish oils) utapata omega-3 ya kutosha.

Licorice:
Huu ni mzizi ambao hutumika hasa kuondoa tatizo la msongo (stress) kwa watu wanaokumbwa na tatizo hilo. Pia mzizi huo hutumika kama sukari kwenye vinywaji kama chai au kahawa badala ya kutumia sukari ya kawaida. Hata hivyo mzizi huu una estrogen ambayo hushusha kiwango cha homoni ya kiume ya testosterone kwa wanaume. Kuna utafiti ulifanywa ambapo wanaume 7 wenye afya walipewa gramu 7 za vidonge vya licorice kila mmoja kila siku. Vidonge hivyo vilikuwa na kiasi cha gramu 0.5 za glycyrrhizic (kiambata kilichomo ndani ya licorice kinachopunguza testosterone kwa mwanaume). Baada ya siku 4 tu kiasi cha homoni ya testosterone kwa kila mwanaume aliyefanyiwa utafiti huo kilipungua kwa kiwango cha nusu ya kiasi cha homoni kwa kila mwanaume kilivyokuwa wakati wa kuanza utafiti.

Bia (Beer): 
Sipendi kusema habari mbaya kwa wanywaji wa bia. Hata hivyo ni vema kusema ukweli kuhusu athari ya bia kwa wanaume. Bia imetengenezwa kwa humle (hops) ambayo kwa kiwango kikubwa inaleta hali ya homoni za kike kwa wanaume (highly estrogenic). Humle (Hops) ina kiasi cha 300,000 IU cha estrogen kwa kila gramu 100 za hops. Kabla ya mwaka 1487 bia ilikuwa ikitengenezwa kwa viambata (ingredients) ambazo zililenga kuifanya bia inaponywewa na mwanaume humfanya mwanaume awe na hali ya uanaume kweli kweli (more aggressive, horny, and socially dominant). Hata hivyo baadaye Kanisa liliingilia uzalishaji wa bia na kutaka bia itengenezwe kwa viambata ambavyo vitamfanya mwanaume awe mpole au mtaratibu na sio mtu wa maguvu na ubabe ( to make men more feminine and sensitive). Hapo ndipo likazaliwa wazo la kutengeneza bia kwa kutumia humle (hops). Siku hizi bia hutengenezwa kwa viambata vitatu, hops, maji na malt.

Soya (Soy):
Ina kiwango kikubwa cha Isoflavones ambayo ni kiuhalisia ni estrogen. Ulaji wa soya ni sawa na kula kidonge kimoja cha uzazi wa mpango (birth control pill). Kwa kuelewa zaidi madhara ya soya kwa wanaume soma hapa http://www.anabolicmen.com/soy-and-testosterone/



Spearmint:
Hutumiwa zaidi kama kiambata kwenye chewing gums, candies, na breath freshener au kwenye majani ya chai (herbal tea). Spearmint pia in akiwango kikubwa cha estrogen.



Lima beans:
Yana homoni za kike (estrogen) iitwayo inositol ambayo hupunguza kiwango cha homoni ya kiume (testosterone) kwa wanaume.



Whole grains:
Image result for whole grains images

Ina gluten ambayo huongeza prolactin ambayo hupunguza kiasi cha testosterone.

Soda:
Unapenda kinywaji baridi yaani soda? Je unajua soda zimechangia sana tatizo la watu kuwa na unene au uzito uliopitiliza (obesity)? Tukiachana na suala la obesity hebu tuongelee kuhusu namna soda zinavyopunguza homoni za kiume (testosterone). Chupa za plastiki ambazo hutumiwa na makampuni yanayotengeneza soda zimetengenezwa kwa phthalates ambayo hufanya plastiki ziweze kukunjwa katika umbo lolote (flexibility). Phthalates ni estrogen! Kawaida ili kuondoa phthalates kwenye chupa za plastiki makampuni yanapaswa kuziacha chupa hizo zikae kwa mwaka mmoja bila kuweka soda ndani yake. Hata hivyo makampuni hayo mara tu baada ya kutengeneza chupa hizo huweka soda ndani yake na kuzipeleka sokoni kwa walaji. Unajua nini kinatokea? Phthalates inaingia kwenye soda unayokunywa!!! Maana yake kama wewe ni mwanaume unaingiza homoni za kike mwilini mwako na matokeo yake unapunguza homoni za kiume!

Fast food:
Wewe ni mwanaume unapenda kula chakula kwenye Mgahawa wa Fast Food? Ngoja nikupe maneno kwa nini usiwe na upungufu wa nguvu za kiume wakati unafakamia vyakula Fast Food. Ukienda Fast Food unaagiza vyakula vya nyama iwe ni beef au kuku au burger na unaagiza na soda then unaona mambo safi, sio? Haya hiyo nyama au kuku imetokana na wanyama waliofugwa na kulishwa junk grains na kupewa madawa kama antibiotics na homoni za kukuzia wanyama ambavyo vyote hivyo vina asili ya homoni za kike (estrogen). Nyama hizo zinakaangwa au kupikwa kwa mafuta ya mimea kama vile soybean oil au sunflower oil ambayo yana estrogen! Baada ya hapo unashushia soda ambayo ina phthalates (homoni ya kike). Kwa ulaji huo unategemea kunako sita kwa sita uwe ‘super man’?!!   

Thursday, 27 August 2015

Fanya Mazoezi Haya kwa Wiki Tatu Kuongeza Nguvu za Kiume!

Kuna jambo linanishangaza sana, utakuta mwanaume anapata muda wa kukaa kitako muda wa dakika tisini au zaidi akiangalia mpira, au masaa manne, matano na wengine wanakesha kabisa katika baa wakinywa na kula tu, lakini wanasahau kabisa kutenga muda tena mdogo tu kama dakika tano mpaka nane kwa siku kwa ajili ya kuimarisha nguvu za kiume kwa kufanya mazoezi ya kuongeza nguvu za kiume.

Mwanaume anefanya mazoezi ya kuimarisha misuli ya uume hawezi kuwa sawa na mwanaume asiyefanya mazoezi haya sio tu katika kuimarisha nguvu zake za kiume lakini pia kuweza kujitawala katika tendo la ndoa na kuweza kumfikisha mwanamke katika raha ile inayotakiwa.
Mazoezi  haya yakifanywa kwa dhati yanaweza kumpa mtu matokeo mazuri sana ilimradi afuate utaratibu atakao takiwa aufuate.
Hizi ni miongoni mwa faida zinazopatikana kwa kufanya mazoezi haya ni hizi zifuatazo:
Kwanza humpa uwezo mwanaume kuweza kusimamisha uume wake kwa muda mrefu zaidi kuliko ambavyo alikuwa anaweza kuusimamisha  kabla ya kufanya mazoezi haya.
Pili mazoezi haya hufanya mtiririko wa damu kwenye uume uwe mzuri hivyo kuufanya uume uwe na nguvu na kuondoa kabisa tatizo la nguvu za kiume.
Tatu humpa uwezo mfanyaji wa mazoezi haya kukawia kumwaga mbegu hivyo kumpa nafasi mwanamke aweze kufikia katika kilele chake pasi na kumkatishia njiani.
Vifaa Unavyohitaji
1.   Mafuta ya mizeituni (Olive Oil) au mafuta ya nazi au Alizeti au mafuta ya mgando (gel)
2.   Jiko  lolote ili upate mvuke wa kutosha unaweza kutumia jiko la mchina, stove, au hata la mkaa lakini isiwe moto mwingi uwe kiasi tu lengo ni mvuke
3.   Kitambaa kisafi na laini na maji safi ya uvuguvugu

Namna ya kufanya mazoezi ya Kuongeza nguvu za kiume
1. Loweka kitambaa chako katika maji ya uvugu vugu kisha anza kwa kuusafisha uume wako kwa kitambaa laini cheye maji ya uvugu vugu kama unauchua uume kwa kuuvuta mbele. Fanya zoezi hili kwa dakika tatu.

2.  Pakaa mafuta yako kwenye viganja vyako viwili vya mikono yako kama vile unataka kujipaka mafuta mwilini.

3.  Weka viganja vyako ili vipate mvuke wa moto kutoka katika ama jiko la mchina, stove au kitu chochote utakachotumia. Ukiona viganja vimepata joto kiasi cha kutosha siyo mpaka uungue mikono, kisha

4.  Kamata uume wako ukiwa unauchua kwa kuuvuta mbele kwa nguvu kidogo sana ukianza na mkono wa kulia alafu wa kushoto au kushoto halafu kulia vile utakavyoona inafaa. Joto kwenye mikono likiisha rudisha mikono yako uipashe tena ili ipate joto kisha rudia  kuuvuta vuta tena uume kwa muda wa dakika kumi.
Kumbuka
Mazoezi haya hufanywa mara mbili asubuhi tu mtu ukiamka na wakati ukitaka kwenda kulala na ni kwa muda wa wiki tatu. Utaona matokeo yake.



Thursday, 13 August 2015

Yajue Madhara ya Kufanya Mapenzi kwa Kutumia Mdomo (Oral Sex)

image
Utafiti uliofanywa na Shirika la Afya Duniani (WHO) nchini umeonyesha asilimia 20 ya saratani ya koo husababishwa na ngono ya mdomo maarufu kama ‘Oral Sex”. Utafiti huo unaonyesha saratani ya koo pia huambukizwa kupitia njia mbalimbali ikiwemo ulaji wa vyakula vyenye pilipili, pombe kali, vitu vyenye uchachu pamoja na kurithi kutoka kwa wazazi.

Saturday, 8 August 2015

Zifahamu Sababu za Uke wa Mwanamke Kutoa Harufu Mbaya




Wanawake na watu wengi hudhani kuwa harufu mbaya itokayo ukeni ni matokeo ya uchafu na kutojisafisha vizuri… Matokeo yake huongeza jitihada katika kujisafisha bila mafanikio ya kuondokana na tatizo hili. Kihalisi, badala kusuluhisha, unapojisafisha zaidi ni unaongeza tatizo badala ya kutatua. Japokuwa ni kweli mara nyingine inaweza ikawa ni sababu ya uchafu… Ila mimi naamini walio wengi huwa wanazingatia usafi… Ndo maana nimeona leo tupeane mawazo juu ya tatizo hili, na kujua namna ya kujikinga.


VISABABISHI

i. Bacteria

Tatizo hili husababishwa na Bakteria kwa asilimia kubwa. Kwa asili, ukeni huishi jamii ya bacteria waitwao Lactobacillus ambao jukumu lao kubwa ni kufanya mazingira ya uke kuwa katika hali nzuri. Kutokana na njia mbaya za kusafisha uke, hasa kujisafisha kupindukia, ama kwa kutumia sabuni zenye dawa, husababisha bacteria hawa kufa kwa wingi na mahala pake kuchukuliwa na aina zingine za bacteria ambao huzaana kwa wingi na kusababisha tatizo hili.
Pia kwa wale wanaojamiiana kinyume na maumbile, kuna hatari ya kuhamishia bacteria wanaoishi kwenye njia ya haja kubwa na kuwahamishia ukeni ambapo watazaliana na kukuletea madhara haya.

ii. Kuvu(fungus)
Hii mara nyingi huambatana na uchafu mzito utokao ukeni mfano wa maziwa mgando(mtindi)

iii. Magonjwa ya zinaa(STIs)
Kwa asilimia kubwa husababisha na Chlamyidia na kisonono(gonorrhoea). Yote mawili hutibika kirahisi, ila husababisha madhala makubwa zaidi yasipotibiwa kwa wakati. Tukio baya ni kuwa mwanamke anaweza akawa na magonjwa haya na asione dalili yoyote. Ila mara nyingine mwanamke anaweza kujisikia maumivu anapokojoa, na mara nyingine mkojo unakuwa kama una ukungu, vikiambatana na harufu mbaya.

iv. Maambukizi ya via vya uzazi vilivyo ndani ya nyonga[Pelvic Inflammatory Diseases(PID)]
Hii husababishwa na bacteria waambukizwao kwa njia ya ngono wanapofanikiwa kufika kwenye tumbo la uzazi na hata pia mirija ya mimba na hata kokwa(ovaries), hasa chlamydia. Mara nyingi mwanamke anaweza asijisikie chochote hadi pale atakapojisikia maumivu yasiyokwisha ya tumbo(chini ya kitovu), au itakapoingiliana na utungaji wa mimba. Na kama atajisikia, mara nyingi huwa ni maumivu ya nyonga, harufu mbaya, uchafu mzito ukeni, homa, maumivu wakai wa kukojoa na hata maumivu wakati wa kujamiiana.
Tatizo hili lisipotibiwa mapema laweza kusababisha utasa, ama mimba kutunga nje ya mji wa mimba.

v. Kansa ya uke na kansa ya shingo ya kizazi
Asilimia chache sana ya wanawake inaweza ikawa ni kutokana na kansa ya shingo ya kizazi ama ya uke. Hapa ndipo inapoonyesha kuwa tatizo hili siyo la kufumbia macho, na umuhimu wa kuwahi kwa wataalam wa tiba kwa uchunguzi wa mapema na kabla tatizo halijawa kubwa.

vi. Uchafu
Usipokuwa msafi kwa kiwango kikubwa utakuwa unakaribisha wadudu kuzaliana na kukuletea madhala. Pia unatakiwa kuwa makini wakati wa hedhi, na pia uchaguzi wa pedi, kwani kuna pedi ambazo zina kemikali za kukata harufu zinaweza kukudhuru.

JINSI YA KUJIKINGA

• Usiwe unaosha ukeni kupita kiasi kwani husababisha kuondoa bacteria wa asili wa ukeni(Lactobacilli) na kukaribisha bacteria wenye madhala.

• Pia epuka sabuni zenye dawa(antibacterial soap) usafishapo ukeni, kwani hii pia huua bacteria wa asili wa ukeni.

• Hii haimaanishi usiwe unasafisha ukeni. Usafi ni muhimu, kwani uchafu pia hukaribisha vimelea vya magonjwa.

• Kama tatizo limeshajitokeza, wahi haraka kwa wataalam wa tiba wakufanyie uchunguzi na kujua ni kipi kati ya vilivyotajwa hapo juu kilichosababisha. Daktari atakuchunguza na kujua kama ni bacteria, fungus ama ni dalili za awali za kansa na kuchukua hatua mapema kuepusha madhala zaidi.

• Kumbuka kujisafisha kupindukia si suluhisho kama tatizo limeshajitokea, kwani kunaweza kuzidisha tatizo badala ya kusuluhisha.

Zifahamu Nutrients na madini muhimu kwa Nguvu za Kiume



Siku hizi wanaume wengi wamekumbwa na tatizo la ukosefu wa nguvu za kiume kwa maana ya kutokuwa na uwezo wa kusimamisha uume wakati wa kufanya mapenzi, kushindwa kuendelea kusimamisha hadi mwisho wa tendo na kushindwa kurudia tendo hadi kuwaridhisha wenzi wao. Kadhalika wengine wamekuwa na tatizo la mbegu zao za kiume kutokuwa na umbile bora (sperm abnormalities) linaloziwezesha kusafiri kwa kasi ya kutosha katika uke wa mwanamke (sperm motility). Aidha wengine shahawa zao zina mbegu kidogo (low sperm count). Mwanaume anapomwaga shahawa wakati wa kufanya mapenzi shahawa hizo hupaswa kuwa na mbegu za kiume kiasi cha milioni 50 kwa kila milimita moja ya shahawa. Endapo kiasi hicho kitapungua chini ya miioni 20 uwezo wa uzazi (fertility) wa mwanaume huwa na kasoro. Matatizo yote hayo yanatokana na wanaunaume wengi kutokula vyakula sahihi au ulaji wa vyakula hivyo kwa kiwango kidogo ikilinganishwa na mahitaji ya mwili (Recommended Daily intake).

Friday, 7 August 2015

Je Unajua Maana na Umuhimu wa Uvaaji Shanga kwa Mwanamke?

Image result for uvaaji wa shanga kiunoni
Shanga zimeanza kuvaliwa tokea zamani na kipindi hicho nahisi zilikuwa zinavaliwa kwa sababu ya urembo zaidi,au zilikuwa zinavaliwa kama sehemu ya mavazi ya mwanamke wa kiafrika lakini sidhani kama zilikuwa zinavaliwa kwa ajili ya mambo ya kupeana Raha na Utamu.Ili kuepusha Post isiwe Ndefu sana ukachoka kuisoma,nikaona itakuwa jambo la busara nikimix Umuhimu na Jinsi ya kuzitumia kuliko kuelezea mara mbili,kwa hiyo zifuatazo ni sababu,umuhimu na jinsi ya kuzitumia shanga za kiunoni wakati wa kupeana Raha na Utamu: