Wednesday 30 September 2015

Tibu Ugonjwa wa Shinikizo la Damu Na Magonjwa Mengine Kwa Kitunguu Swaumu


Image result for garlic photos

Kitunguu swaumu (Garlic) mpaka sasa kimeripotiwa kuwa na matumizi 125 ya kitabibu kwa binadamu. Matumizi yafuatayo ya kitunguu swaumu ndio yamefanyiwa utafiti wa kitalaamu wa kitabibu:

  • Kupunguza tatizo la damu kuganda katika mishipa ya damu (reduce blood clotting) na ugonjwa wa shinikizo la damu (blood pressure): tafuna punje ya kitunguu swaumu kila mara au tumia unga wa kitunguu swaumu kwa kuweka kiasi kwenye maji ya moto au chai na kunywa.
  • Kuzuia Saratani ya Tumbo (Stomach cancer): Kula mara kwa mara kitunguu swaumu husaidia kuepusha kupatwa na saratani ya tumbo.
  • Kinga ya Mwili (Immune system): Ulaji wa kitunguu swaumu husisimua utendaji kazi wa macrophages utendaji kazi wa T cells.
  • Husaidia kukakamaa kwa mishipa ya damu ya Arteries (Atherosclerosis), kupunguza cholesterol (blood lipids) na tatizo la mzunguko wa damu mwilini (peripheral vascular disease): Tumia mafuta ya kitunguu swaumu au tafuna punje za kitunguu swaumu mara kwa mara.
  • Kutibu Minyoo aina ya Threadworms: Saga punje kadhaa na weka kwenye glasi ya maziwa ya vuguvugu/moto na kunywa asubuhi kabla hujala chakula chochote.
  • Miguu kufa ganzi (Leg numbness) na Sciatica pain relief: Saga punje kadhaa za kitunguu swaumu au chukua kisi kidogo cha mafuta ya kitunguu swaumu weka kwenye glasi ya maziwa moto. Kunywa mara 1 - 3 kwa siku hadi utakapopata nafuu.

No comments:

Post a Comment